Hatimaye nimeachana na mchepuko wangu

Status
Not open for further replies.
Hizi mada zimekua nyingi mno.
Nadhani watu wengi tunapitia mapito magumu sana kwenye mapenzi, wale tunaopata jukwaa la kusemea walao ndio tuna sema hapa.

Lakini wapo wengi sana wanapitia ya kupitia huko kwenye mapenzi moja kwa moja ama isiyo moja kwa moja.

Maana yake nini? Au tufanyeje? Tuachane na mapenzi?
Au turudi nyuma na kuangalia tulipo kosea?
Mbona wazee wetu hawakuwa na haya tulio nayo sasa?

Binafsi ni wakati sasa wa kutafakari kama kuna umuhimu wa mapenzi maishani mwangu, haijalishi nimeoa au la! Ila natafakari upya kuhusu umuhimu wa mapenzi kwa ujumla wake.

Natumaini maisha yenye furaha na amani yanawezakana nje ya mapenzi, natumaini.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…