Hatimaye nimepata kazi kupitia JF

Kuna siku nilitaka kuuliza vipi Mzee kazi ulipata?
 
Hongera mkuu mimi kama mwenyekiti wa majobless wa JF nakutakia kila raheri
 
Hongera sana,

Uzi wako wa mwanzo ulivyouelezea feels like tupo wote kazini tunafanya kazi, kumbe working culture ya mashirika yasiyo ya kiserikali/donor funded ni ile ile.

Ungekuwa haujamention kuwa Dr KJ ameshafariki akili yangu ingejiridhisha kuwa ni mkuu mmoja mmiliki wa NGO moja (ila yenyewe wana miradi ya afya), same same personality, typa psychopath, yet extremely intelligent and a very good lobist. Aliwahi kulob pesa za kufund tafiti za ugonjwa A zitumike/zipunguzwe kwenye ugonjwa B ambao ni threat kuliko ugonjwa A na meza ikapinduka huko kwa wakubwa 👏🏻

Uzi wako mzuri sana kwa job seekers.
 
Mkuu, nimejaribu nikucheki PM (sijafanikiwa) baada ya kusoma comment hii vizuri ili nichukue baadhi ya madini toka kwako baada ya mengine kuyapata kwa TAI DUME ni kuhusu mashirika na utendaji wa kazi kiujumla.
 
Huu uzi ulinifanya nikazisome zile episode zako zote, nilitumia masaa mengi kweli hadi usiku mnene maana sikutaka niachie njiani[emoji2][emoji2][emoji2]

Nimejifunza mengi sana kwenye episodes ila lililonivutia sana ni kitendo cha kuwa Humble kwa kila mmoja hata humfahamu.

Vipi Mswedy bado unawasiliana naye?

Baada ya Dr KJ kurejea kwa Muumba, ofisi yake iliendelea au iliondoka na muhusika?

Sistaa Duu bado yupo kwenye lile shirika?

Yule Dada aliyenasa mtego kule Kibondo naye je?

Umesema umekanyaga kila Wilaya iliyopo hapa Nchini. Wilaya ya Singida Vijijini uliwahi kufika kwenye vijiji gani?
 
Umejipangaje!!?

Kama connector wa job akataka kimasikhara utamwepukaje!!?

Just kidding kijana!!
 
Wengne hawatasem ila me ntasema tu!

Hukujaribu kimasihala??
 
Mkuu hongera sana sana mkuu huyo mdada abarikiwe sana kwakweli am happy for you mkuu nilikuwa nasikitika sana kuona ulivyo na uwezo mkubwa na maarifa makubwa hivyo halafu una hangaika namna hiyo huna kazi wakati watu wa “hovyo” (jokes) wana kazi nzuri na hawana uwezo hata wakuzitetea…

Hakika Mungu ni mwema sana sana muda wako ulifika!
Naungana na mtoa mada hapo juu kukuomba usivuke mipaka ukamtongoza huyo dada maana ndio utakuwa umejiachisha kazi(zingatia hili)
 
Hongera sana ila huyo dada awe dada yako usianze vurugu vurugu kumsumbua kwa hata kama yeye akikutaka uwe na hekima Mungu kamtumia yeye maana ndugu zako wote na marafiki walishindwa kukupa ajira
 
Shida umesoma episodes bila kusoma comments
Ukawa unarukia episode mpya,unaskip comments.

Hayo yote uliyouliza,na mengine zaidi tulimuuliza na alishayajibu,tena na zaidi.
Rudi tena kasome ..comments pia ni nzuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…