Hatimaye nimetimiza miaka 30 ila sina mbele wala nyuma naombeni ushauri

endelea kupambana, usikate tamaa kuna wengine walitoka kwenye 50's/60's huko
Happy birthday
 
Maamuzi ya kutokuwa na mbele wala nyuma yako mikononi mwako,jitambue kwanza mbele yako(malengo yako) ni ipi na nyuma yako(msingi Wa kufikia malengo yako) ni ipi.Kwa sababu hauna mbele ndio sababu ya kuliwa nyuma,na utabakia hauna mbele wala nyuma.
 
Pole sana mkuu, usikate tamaa endelea na mapambano.

Mwangalie Dr Shika aliyumba lakini karudi kwenye mstari ndani ya siku kadhaa tu.

Never give up bado kijana!
 
Uza smart anzisha mradi wa kuku, acha kuchati ,na kununua bando , fanya kazi yoyote ya halali kwa bidii ,achana na watu walio na hali kama yako ,badili marafiki kaa na walio fanikiwa, amka asubuhi na mapema, kwa njia hio utafanikiwa na MUNGU akubariki Amina.
 
Kila mja ana muda wake wa kufanikiwa,jitathimini anza upya ukiwa na malengo mazuri utatoboa.Sala pia ni kitu cha muhimu.Usisahau.
 
Jamani leo ni birthday yangu

Nimetimiza miaka 30 lakini sina mbele wala nyumaa

Vyuma vimekaza hadi sasa sina mbele wala nyuma

Naombeni ushaurii
Kama huna mbele wala nyuma, nenda kiubavuubau kama Kaa. Kaa anakwenda kiubavu ubau na bado anaishi
 
Nakueleewa sana ndugu
Kuna wimbo mmoja wa kinaijeria unaimba
" to be a man you have to be succesful make sure you get monii (money), you haso(hustle) ooh and God will.bless you ooh
 
Japo m mwenyewe cna mbele but bado kuna miaka 5 hapo!!
 

Attachments

  • kiruc.+20171018_181540.jpg
    7.4 KB · Views: 33
Hahahaha pole sana mkuu, si cheki kama vile ni kitu kizuri ila la muhimu umejitambua cha muhimu ni kufanya maamuzi stop wasting time amuakufanya kwa dhati kitu chochote kitakacho kusidia maishani utafanikiwa tu. Kuliko kuendelea kujihesabia miaka.
 
Komaa tu ndugu, mafanikio hayana umri, siku yako ikifika utatoka tu mura.
 
Usiogope ukifikisha 50 utapata umbo la nyuma. Anyway komaa tu bro hii ni bongoland
 
Simple;
1)Amua ni nini unataka kufanya.
2)Jifunze namna kinavyofanyika, then
3) Kifanye.

Ni kama unanawa!
 
Jamani leo ni birthday yangu

Nimetimiza miaka 30 lakini sina mbele wala nyumaa

Vyuma vimekaza hadi sasa sina mbele wala nyuma

Naombeni ushaurii
Selaah Mtukuze na Kumuabudu Mungu, Ukioa inaweza kukupa changamoto, so unaweza anza kuweka mtoto mzuri ndani ukiona mnaenda poa unaoa kabsa.

Kama unatembea mistari ya ziggy punguza step pia msela.

Heri ya mfanano wa siku ya kuja kwako duniani, hukuja bure, una ridhik yako ila elewa, "a world ain't a cake".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…