Nilivyowaona tu leo wanaingia pale Uwanjani hasa vyumbani huku wakiwa wanashangilia kizembe kizembe na kuimba nyimbo za Mafirauni fulani hivi wa Bongo Fleva nikajua mapema tu kuwa tayari nuksi imeshatukuta na hatuna chetu. Halafu kuna Vichezaji fulani hivi viwili vya Serengeti Boys vilikuwa vimeshaanza kujiona kama vile akina Messi na Ronaldo kwa kuwa na mapozi ya hovyo hovyo na kuota majipu ( kuanza kuringa na kujisikia ) kana kwamba wameshafika Kombe la dunia.
Warudi tu kwakweli tuendelee tu kula nao bamia, kisamvu, matembele yetu na maharage kwani ndicho tunachokiweza na siyo mpira. Mnatusumbua tu kila siku katika Radio na Tv kuwa tuwachangieni halafu tunajinyima mnaenda huko mnaishia tu kumbwela mbwela. Tena TFF na Malinzi kesho asubuhi tu nakuja Karume hapo Ofisi zenu za TFF kuchukua Pesa yangu ya mchango kwani nilitoa ili Timu ifanikiwe na siyo iishie njiani kama hivi. Kesho nataka Pesa yangu tafadhali!