Mtu yeyote anayeamini katika TAIFA KWANZA kama wewe ana maswali mengi ya kujiuliza kuhusu uteuzi huo. Huyo bwana atakuwa anagonga marupurupu yote ya U-Waziri Kiongozi Mstaafu (ukiacha monthly pension) kutoka SMZ, na analamba mishahara na marupurupu yote ya U-waziri wa Mambo ya Ndani kutoka SJMT. Anayeelewa zaidi atatueleza. Kilichosababisha uteuzi ni kuiepusha Zanzibar na msukosuko wa baada ya Uchaguzi, si unakumbuka mbio zake ziliishia Dodoma? Maslahi ya "Wananchi wanyonge wa Tanzania" hayakuzingatiwa katika uteuzi wake wa sasa. Pinda alipaswa aorodheshe uteuzi wa Nahodha kuwa miongoni mwa "Maamuzi magumu."