2019
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 3,130
- 4,735
Kwenye mtandao wa kukata tiketi za treni ya Deluxe kutoka Dar es Salaam hadi Arusha ni rasmi imekufa. Nakumbuka usafiri huu ulisaidia sana changamoto ya usafiri hasa kwa watu wa kipato cha chini na cha kati.
Hata mimi nilipanda baada ya kuona inasifiwa sana na ilikua na vibe la kweli
Nauli kutoka Dar hadi Moshi daraja la 3 ilikua 16500,kila msafiri aliweza kumudu tofauti na mabasi ambayo ni zaidi ya 40,000.
Mradi huu ambao kabla ya kufufuliwa na Magufuli ulikuwa umekufa kwa miaka zaidi ya 30,rais Magufuli akapambana na kuurudisha pamoja na kukarabati vituo vyote vya mkoloni na kujenga vya kisasa.
Nini kimeuwa ruti hizi? Tukisema ni hujuma za wenye mabasi na malori tutakosea? Au ni uzembe wa serikali tutakosea?
Kwanini mpaka sasa shirika la reli liko kimya kutangazia umma kuwa hiyo ruti imekufa?.
USHAURI WANGU KWA SERIKALI
Kwa kweli nikizoom hali ya sasa ya watumishi wengi serikali si makini kwenye usimamizi. Rejea hali ya mabasi ya haraka (mwendokasi) mradi wa Mbagala umekamilika lakini hakuna magari. Iyo hali ya trc hata SGR muda utaongea tu n.k
Serikali kupitia TRC itoe kibali au ibinafsishe hiyo reli iendeshwe na kampuni au taasisi ya binafsi naamini mambo yatakuwa mazuri sana.
View: https://youtu.be/2dUbS5zZkK0?si=ptd_kKrdlvRH8-RZ