Haya umemsikia Raisi wako alicho kisema leo kuhusu Corona it means Jiwe alikuwa Analipeleka Taifa shimoni .
MATAGA kweli akili hamna yaani mlikuwa mna interact kabisa ule ujinga wa Jiwe !? [emoji3][emoji3]
Hamna cha ujinga tokea watangaze third wave kwa nchi za ulaya ,nchi nyingi za Ulaya zimeandamana kupinga Lockdown.
US mwezi napo mwezi wanne wanaifungua baadhi ya majimbo,mfano lakers na clippers mechi watakazo cheza April 15,mashabiki wataanza kuruhusiwa ila idadi hawaja taja.
Na ukitizama US still bado wanadondoka so huu ugonjwa upo na utaendelea kuwepo so kujifunza kuishi nao.
Kuhusu chanjo tunarudi kule kule aliposema Magu "Tusubirie huku tukiangalia ufanisi wa hizi chanjo kwa nchi nyingine then tuagizie".Hizi chanjo hata ukitumia ziku kudhuru hata ukifungua kesi madai hulipwi.Astrazaneca nchi nyingi wamezisitisha kwanza kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 60 sababu ya kuganda kwa damu,Pfizer nazo CNN juzi wametangaza zinatoa kinga kwa miezi sita.
Brazil nae juzi kachukua chanjo iliyo tengenezwa Russia (Sputnik V efficiency 92%) 10 mil dozi,ambayo inchi nyingi za ulaya wanaikandia kwa ajili ya kuwapa raia wake.Tusubirie hii majibu yake kwa watu wa Brazil,japo huu ugonjwa nao ushaingia siasa za Kimagharibi na Russia.
Na hapo bado hatujui -ve side effects za mda mrefu za hizi chanjo,tuombe Mungu huko mbele zisilete madhara.
Kenya wameagiza dozi za Astrazaneca zaidi ya laki 8 ila kwa mujibu wa BBC swahili wauguzi wengi wamekataa kuchoma,wamewapa wagonjwa sasa sijajua na hawa wauguzi wa Kenya nao ni Mataga?.
Ktk swala hili la Corona hata mkiponda Magu na watu wanao msapoti,ila ukweli Magu alikuwa mbele ya Muda,kwani usishangae kuna siku EU na WHO wakatangaza tenth wave of Covid sasa sijui itakuwa mwaka gani.