Hatimaye! Unaweza kufanya malipo mtandaoni kwa M-Pesa

Hatimaye! Unaweza kufanya malipo mtandaoni kwa M-Pesa

Hivi unaweza kupokea hela toka nje kupitia hiyo MasterCard ya Voda?
 
yeeees hizi ndo colaboration kali za makampuni tulizokuwa tunazitaka sasa bado paypal na benk za tanzania tuweze kupokea mitonyo kwa paypal
 
Hii ishu imerahisisha sana maisha. Nimejiunga mchana. Jioni hii nimelipa dollar 25 google play kwa kuitumia. Voda wametisha. wafanye tu kuitangaza.
ni kama kiasi gani za kitanzania zilikatwa na mpesa kwenye hiyo dollar 25?
 
Hapana, hela unaweka through M-PESA, then unaiamishia kwenye M-Pesa MasterCard.
step za kuhamishia pesa mastercard mkuu..maana mie nisha tengeneza mastercard tayari..nataka ku purchase ebay nimechoose payment kwa mastercard nimejaza kila kitu ila nadhani inakuwa kama salio hamna hv inanionyesha hv
20180927_204352.jpeg
 
Ukiitaja banc ABC napata kiunhulia kikali, wanavaa masuti kama watu wa maana ole wako uingie kwenye 18 zao!
 
Wakuu naomba msaada wenu najaribu kulink mpesa mastercard na apple pay ili niweze kulipia apps nipata respond kuwa “invalid info” aliyeweza please anisaidie
 
BancABC kwa kushirikiana na MasterCard, wamezindua huduma mpya iitwayo M-Pesa-Mastercard ni ya kwanza na ya kipekee Tanzania itakayomuwezesha mteja wa M-Pesa kuweza kulipia huduma na bidhaa mitandaoni katika tovuti mbali mbali Duniani zinazopekea malipo kwa MasterCard. Kupata huduma hii ya Virtual Card piga *150*00# chagua lipa kwa M-Pesa, chagua M-Pesa MasterCard, kutengeneza kadi yako. Utapata Card Number, Expiration date pamoja na CVV Number ndani ya sekunde chache tu!

hawa abc bonge la benki.ni shawahi cheza kamali mtandao mpunga ukatumwa bila kuzuiliwa kama benki nyengine
 
Haya ndo mambo tunataka sasa, Jev vipi kulink hio Virtual card na paypal inakubali mana Sellers wengi amazon na ebay wanapokea via PayPal, na vipi kuhusu kupokea malipo kwa PayPal imeanza au bado?
naomba hili swali lijibiwe.
 
nafikiri wanaweka dola 25 bure mi nimefanya miamala bila kuweka imekubali ebu wakuzi waje kutuambia ni vipi apo iyo ela tunarudisha vipi
Mimi nimejaribu hii kitu Kwa kuweka Tsh.15200 na nikanunua kitu cha USD 6.06 AliExpress na wamekata tsh tsh.14422.33 nikabakiwa na tsh 777.67.
Hapa namaanisha exchange rate zao zinacheza kwenye 2379.93 Kwa Dollar au kuna makato Fulani hayako wazi
 
naomba hili swali lijibiwe.

Kuhusu kupokea malipo kwa paypal sina uhakika sina ila binafsi kwa kweli nilitakiwa kulipwa ila sikuweza fanikiwa kupokea pesa yangu kwa hiyo paypal, ikabidi nibadili payment method ndio nikapokea mpunga wangu. Ila kwenye kufanya malipo naitumia sana paypal sioni tatizo, ishu ni kupokea ela ndio nilikwama hapo.
 
Back
Top Bottom