Hatimaye uongozi sikivu wa Simba SC, waazimia kuboresha kikosi

Hatimaye uongozi sikivu wa Simba SC, waazimia kuboresha kikosi

Mahitaji ya Simba kwa sasa ni:-
1. Beki wa pembeni aliyekamilika anayeweza kucheza kushoto na kulia bila wasiwasi ili kuwasaidia Shomari na Mohamed Hussein. Hapa Gadiel atolewe kwa mkopo.
2. Kiungo mkabaji wa kimataifa ambaye pia awe na uwezo wa kucheza kama mlinzi wa kati pale atakapohitajika. Hapa kati ya Akpan na Outara mmoja atoe nafasi.
3. Mshambuliaji mmoja wa kati wa kimataifa mwenye kujua kufunga tu. Hapa Dejan ameshaondoka nafasi ipo wazi.
4. Kiungo mshambuliaji mmoja wa kimataifa mwenye kasi wa kumsaidia Chama hasa pale anapokosekana uwanjani. Hapa kwa kweli Okwa ligi ya bongo imemshonda vibaya mno kwani bora hata Chikwende walau kidogo alionyesha uwezo wake. Lakini kwa Okwa ameshindwa kabisa na si dhambi akiondoka kujaribu sehemu nyingine na wala haitakuwa ajabu akifika huko akawika kwani ndio maajabu yenyewe ya mpira.
 
Mleteni manzoki, beki wa kati, beki wa pembeni na kiungo mkabaji.
Hili neno "kiungo mkabaji" ni upotoshaji mtupu, hakuna mchezaji wa kiungo ambaye eti yeye kazi yake ni kukaba tu! Hii sio kweli kwani kila mchezaji uwanjani ana jukumu la kukaba na hata kipa kuna wakati anaweza kuwajibika kukaba.

Sasa haya mambo ya kusema kiungo mkabaji ni mambo ya kiswahili swahili tu na hata kwenye soccer terminologies hakuna kitu kama hicho.
 
Back
Top Bottom