Baada ya siku kadhaa za maandamano ya kutaka kuvunjwa kwa kilichokuwa Kikosi Maalumu cha Kuzuia Wizi (Special Anti-Robbery Squad maarufu kama SARS) nchini Nigeria, IGP wa Polisi jana Jumapili ametangaza rasmi kuvunjwa kwa kikosi hiko.
SARS, ambacho kilikuwa kitengo maalumu chini ya jeshi la polisi toka 1992, kwa muda mrefu kimekuwa kikilaumiwa kwa unyanyasaji, ukamataji pasipo kufuata sheria, utesaji na hata mauaji.
Maandamano ya sasa yakichagizwa na wasanii wakubwa wa muziki (kama anavyoonekana wizkid katika video), yalizuka baada ya video moja kusambaa ikiwaonesha askari wa SARS wakimpiga risasi hadi kumuua mwanamume mmoja katika jimbo la Delta ya Kusini.
Ujumbe wa ofisi hiyo kupitia mtandao twitter, unasema kuwa kikosi maalumu cha kukabiliana na waporaji kinachojulikana kama SARS kimevunjiliwa mbali mara moja.
Kusoma na kuelimika pia ndio kitu kikubwa kimewasaidia hawa Wanaigeria ,Wanaigeria wengi wasomi na wameelimika, Sasa wasanii wa Bongo kwa kweli tuwaache tuu waendelee kuvalishwa makofia ya kijani.
Kusoma na kuelimika pia ndio kitu kikubwa kimewasaidia hawa Wanaigeria ,Wanaigeria wengi wasomi na wameelimika, Sasa wasanii wa Bongo kwa kweli tuwaache tuu waendelee kuvalishwa makofia ya kijani.