Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Kwa maslahi ya Taifa ni jambo jema sana hawa kina Mdee wakirudi Bungeni.
Pia wasiishie hapo tu Lissu apewe cheo kama Magufuli alivyomuhaidi na Maalim Seif akubali maridhiano maisha yaendelee.

Wapinzani wajipange upya hasa katika kudai tume huru.
 
Daaaah, katibu mkuu aite press aeleze nini kimejiri!
Hii kitu mbona imekuwa ghafla hivi? Kuna nini kinaendelea?
Wewe nini? Aite press ili iweje?

Hongera sana CHADEMA mmeonesha ukomavu wa kisiasa, msiwasikilize watu wa sampuli hii ni wafitini sana.
 
Daaah!! Njaa mbaya.[emoji2][emoji2][emoji119][emoji119]
Hii ndio kukuonyesha kuwa, wanasiasa na vyama ni njaa tu.. hakuna kingine... kwa utaratibu wao huu, wasishangae kukosa kuungwa mkono na Watanzania, kwani wanajua kabisa hawa ni njaa kali tu.
 
Nasisitiza, mnaoendelea kuwaamini wanasiasa mjitathmini tena. Mwanasiasa akija ndani akakuambia jua limezama toka nje uhakiki kwanza. Futseke zao!

Hahahaha tumefikia apo
 
Wewe nini? Aite press ili iweje?

Hongera sana Chadema mmeonesha ukomavu wa kisiasa, msiwasikilize watu wa sampuli hii ni wafitini sana.
Aeleze nini kimejiri na kwanini ilikuwa siri!Hata waandishi wa habari walikuwa hawajui spika kawaitia nini!
 
Acha upumbavu wako wewe ndiyo hujielewi sisi CHADEMA hatupendi unafiki Wanachadema wakila pesa za CCM tunaongea ukweli, huu upumbavu wa kufanya siasa biashara ndiyo umemfanya Lissu kuondoka mapema kwenda huko maana anamjua mwenyekiti wa CHADEMA ni mpenda pesa mbele ya pesa anaweza kufanya lolote ili mradi alinde ruzuku yake
 
Nawashangaa wanaoishangaa CHADEMA leo!
CHADEMA ya principles iliondoka na Dr. Slaa toka 2015!

Tuliposema CHADEMA imekufa wengi hawakuelewa, kufa ni process, ila turning point ilikuwa 2015 'kugeuza gia angani'

Kwa hiyo matendo, matukio na matokeo mbalimbali yaliyoendelea baada ya 2015 ndiyo kifo chenyewe, uchaguzi wa 2020 umethibitisha hilo.

- Kumkumbatia na kumsafisha 'fisadi' Lowasa, tena kwa kumpa tiketi ya Urais! Alafu BAVICHA wanaimbishwa kwamba ni bora kushirikiana na shetani ili kuingia ikulu!

- Kufumbia macho udikteta wa Mbowe kwa kutoa maamuzi yake binafsi badala ya taratibu za chama! Alafu BAVICHA wanaimbishwa kwamba. hanunuliki!

- Mtu moja kung'ang'ania uenyekiti kwa miaka 20! Chama kinachojinasibu cha demokrasia! Na kufukuza au kupelekea kujitoa wote waliothubutu kuonyesha nia ya kugombea uenyekiti wa taifa, alafu BAVICHA wanaimbishwa kwamba hao ni wasaliti!

- Ubadhirifu wa mali za chama wa mwenyekiti alafu BAVICHA wanaimbishwa kuwa huyu ni mwamba na haongeki!

- Wabunge, madiwani, viongozi wa ngazi mbalimbali kujitoa kwenye chama kwa kueleza mapungufu makubwa ya mwenyekiti! Alafu BAVICHA wanaimbishwa kwamba wamenunuliwa!

- Kubwa zaidi chama kuziacha sera zilizovuta watu Kama kupinga ubadhirifu, rushwa, kuahidi kuleta maendeleo, kujenga barabara, reli, kuimarisha usafiri wa anga, Bandari, kupeleka na kupunguza bei ya umeme kwa wananchi wengi, kuimarisha matibabu! Alafu kinageuka kuwa watetea mafisadi, watumishi wazembe, wezi na wahujumu uchumi na KUPINGA MAENDELEO eti ni MAENDELEO YA VITU! Alafu mnategemea mtachaguliwa na wananchi! Wananchi siyo wapumbavu kiasi hicho! Kwa ufupi CHADEMA imejiua yenyewe!
 
Loud and clear
 
Ila mkuu wakati mwingine nakuonaga kama kichaa nimegundua nilikuwa nafikiria kwa mihemuko nisamehe mkuu,

Wewe unaonaga kile ambacho wengi hawewezi kukiona kwa wakati.

Nimejifunza kitu.
Shukuru Mungu macho yako yamefunguka.
 

Nadhani wamekwelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…