Nawashangaa wanaoishangaa CHADEMA leo!
CHADEMA ya principles iliondoka na Dr. Slaa toka 2015!
Tuliposema CHADEMA imekufa wengi hawakuelewa, kufa ni process, ila turning point ilikuwa 2015 'kugeuza gia angani'
Kwa hiyo matendo, matukio na matokeo mbalimbali yaliyoendelea baada ya 2015 ndiyo kifo chenyewe, uchaguzi wa 2020 umethibitisha hilo.
- Kumkumbatia na kumsafisha 'fisadi' Lowasa, tena kwa kumpa tiketi ya Urais! Alafu BAVICHA wanaimbishwa kwamba ni bora kushirikiana na shetani ili kuingia ikulu!
- Kufumbia macho udikteta wa Mbowe kwa kutoa maamuzi yake binafsi badala ya taratibu za chama! Alafu BAVICHA wanaimbishwa kwamba. hanunuliki!
- Mtu moja kung'ang'ania uenyekiti kwa miaka 20! Chama kinachojinasibu cha demokrasia! Na kufukuza au kupelekea kujitoa wote waliothubutu kuonyesha nia ya kugombea uenyekiti wa taifa, alafu BAVICHA wanaimbishwa kwamba hao ni wasaliti!
- Ubadhirifu wa mali za chama wa mwenyekiti alafu BAVICHA wanaimbishwa kuwa huyu ni mwamba na haongeki!
- Wabunge, madiwani, viongozi wa ngazi mbalimbali kujitoa kwenye chama kwa kueleza mapungufu makubwa ya mwenyekiti! Alafu BAVICHA wanaimbishwa kwamba wamenunuliwa!
- Kubwa zaidi chama kuziacha sera zilizovuta watu Kama kupinga ubadhirifu, rushwa, kuahidi kuleta maendeleo, kujenga barabara, reli, kuimarisha usafiri wa anga, Bandari, kupeleka na kupunguza bei ya umeme kwa wananchi wengi, kuimarisha matibabu! Alafu kinageuka kuwa watetea mafisadi, watumishi wazembe, wezi na wahujumu uchumi na KUPINGA MAENDELEO eti ni MAENDELEO YA VITU! Alafu mnategemea mtachaguliwa na wananchi! Wananchi siyo wapumbavu kiasi hicho! Kwa ufupi CHADEMA imejiua yenyewe!