Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Hatimaye serikali ya maridhiano kupatikana na ndiyo maana bwana mkubwa mpaka leo hajateuwa mawaziri.

Ni hatua nzuri kwa Mama Tanzania kupata serikali ya Muungano wa Tanzania ikiwa na mawaziri kutoka CHADEMA pamoja na wabunge ndani ya Bunge la Muungano kupitia maridhiano baada ya uchafuzi wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 2020.

Ni kiashirio kuwa hakutakuwa tena na uchafuzi wa chaguzi wala kusigina tena katiba siku zijazo.

Ila mbinyo toka Jumuiya ya Kimataifa, Vyama vya Upinzani, Wadau watetezi wa Haki za Binadamu na Demokrasia utaendelea kuwepo pamoja na serikali ya maridhiano kuundwa ili kuhakikisha serikali ya CCM Mpya inatekeleza maridhiano hayo kwa Vitendo kuanzia 2020 kuelekea 2025 kama Mwenyekiti wa BAWACHA mh. Halima Mdee alivyotuhakikishia leo bila kupepesa macho.
Mwenyekiti wa BAWACHA Mh. Halima Mdee akiongea leo 24 November 2020 ktk video hapa chini

Uchafuzi wa uchaguzi Mkuu 28 October 2020 umefungua mlango wa timu kubwa zaidi ya watetezi na wadau toka nje kuingia na kuibana serikali ya Tanzania chini ya CCM Mpya iliyotaka kuua kabisa demokrasia , uhuru na haki ya waTanzania kushiriki ktk vyombo vya maamuzi kama Bunge na nafasi za uwaziri ktk serikali ya maridhiano.
Esther Matiko mbunge wa Viti Maalum akijibu maswali mara baada ya kuapishwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mh. Esther Matiko ni mmoja wa wabunge 19 wa Viti Maalum kupitia chama cha CHADEMA walioweza kufika Dodoma leo tarehe 24 November 2020 kuapishwa baada ya uchaguzi Mkuu wa 28 Oktoba 2020 kukamilika.

WaTanzania waliogoma kujitokeza kupiga kura kwa wingi, wale pia walioshiriki kufanya uchafuzi ili washinde bila kusahau waliogoma kujitokeza katika maandamano ya amani kwa kuwa hawakujitokeza kupiga kura tumewapatia suluhisho kuhakikisha Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu ujumbe wake unaendelea kusikika ndani ya Bunge, serikalini na Wadau wa Maendeleo nje kutupatia sapoti kuendeleza angano hili la CHADEMA kwa wananchi bila kujali vyama.

More info :
Nusrat Hanje naye ameingia bungeni kuwakilisha CHADEMA kama mbunge wa Viti Maalum leo jijini Dodoma
FB_IMG_1606162812872.jpg


24 November 2020 pichani :

Hii ndio taarifa iliyotufikia usiku huu, kwamba Mhamasishaji wa BAVICHA Twaha Mwaipaya na Katibu Mkuu wa Bavicha Mh Nusrat Hanje , leo wameachiwa huru na Serikali ya Tanzania , huku ikidai haina haja ya kuendelea na kesi hiyo, hii ni masaa machache kabla ya kusomwa hukumu ya maombi yao ya haki ya dhamana .

Hafla ya wabunge wa viti maalum kupitia CHADEMA wakila kiapo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano 24 /11/20
 
Bila shaka ni maamuzi ya uongozi wa chama, kama taarifa hii ina ukweli.
 
Back
Top Bottom