Hatimaye, wamekubali! Harambee Stars warejea kambini baada ya mgomo

Hatimaye, wamekubali! Harambee Stars warejea kambini baada ya mgomo

Wakaguongo

Member
Joined
Sep 23, 2026
Posts
95
Reaction score
38


Baada ya kususia mazoezi kwa takriban wiki moja kutokana na madai ya kutolipwa posho zao, Timu ya Taifa Harambee Stars hatimaye imewasili Nyayo Stadium kuanza maandalizi ya kufuzu AFCON 2027 dhidi ya Eritrea, Siku ya Jumamosi September 26.

Kwa hiyo watakuwa na 'session' moja pekee ya mazoezi, ambayo ni leo kabla ya mechi kesho saa kumi alasiri katika uwanja wa Nyayo. Yaani ni sawa wamerudi lakini muda wa maandalizi ya pamoja umebaki mchache sana.

Hili litaathiri vipi ubora wa kikosi hicho na Je, unadhani Harambee Stars wamepata kile walichokuwa wanadai, au wameamua tu kurudi kambini huku masuala mengine yakisubiri kufanyiwa kazi?

Pia soma: Harambee Stars wagoma kufanya mazoezi, posho na maslahi ya wachezaji zazua mvutano
 
Back
Top Bottom