Hatimaye WANAWAKE walalamikia MBINU ZA UZAZ WA MPANGO

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
9,728
Reaction score
1,204
Katika kipindi cha dira ya dunia cha BBC nimewasikia baadhi ya wanawake wa Dar es salaam wakilalamikia mbinu za uzaz wa mpango kuwa zina madhara kwao,,,,wengi wameonesha kusikitika na kujutia madhara wanayoyapata na wanailaum serikali kwanin inahamasisha????
Mmoja nimemsikia akisema alikosa kuona siku zake(kupata hedhi)na akawa anapata maumivu ya KIUNO,yupo aliyesema ingawa ameacha kutumia hadi sasa hajapata mtoto tena na haish kuhisi kichefichefu,
Swali kwa wataalam(madaktar)naomba sana mtuambie JE NJIA ZA UZAZ WA MPANGO KWA WANAWAKE KIAFYA ZIKOJE????
 
Kampeni nyingi za Uzazi wa mpango za kisasa, zimekaa KIBIASHARA zaidi na kimaslahi zaidi kuliko ukweli na uhalisia wa madhara yake..
 
Kampeni nyingi za Uzazi wa mpango za kisasa, zimekaa KIBIASHARA zaidi na kimaslahi zaidi kuliko ukweli na uhalisia wa madhara yake..

hussein mwiny alipohojiwa amesema kuna athar ndogondogo tu
 
Kusema kweli madhara ni makubwa tu, mpango wa uzazi umetufanya tuhangaike hospitali kibao mpaka muhimbili kupima sperms na mifumo ya uzazi kuona kama tuko sawa kwa miaka 3 tukitafuta mtoto hatimaye tukafanikiwa.

Kiukweli hizi nyia zina madhara sana, zaidi ya hapo wife ameota kitambi ambacho kukitoa imekuwa kazi kwelikweli
 
not good at all,though sijawahi kutumia ila naona wanavyohangaika watumiaji,ni heri kutumia njia za jadi kama kuhesabu kalenda n.k
 
Ni kweli sana hawa wake zetu wana vitambi mpaka vinachosha, kwa ajili ya hii mipango ya uzazi mwanzo nilidhani ni vile vidonge vya Contraceptive lakini sasa bora kutumia mpango wa jadi
 
Kampeni nyingi za Uzazi wa mpango za kisasa, zimekaa KIBIASHARA zaidi na kimaslahi zaidi kuliko ukweli na uhalisia wa madhara yake..


Hapo red sikubaliani na wewe manake huwa zinatolewa bure!
 
Sishauri kabisa kutumia hayo mavidonge yao,chondechonde wanawake mtumie tu njia ya asili,nilishuhudia dada mmoja katika Television za ughaibuni,wanasema alikuwa mzima kabisa wa afya njema,lakini hata wewe ungemuona ungesikitika sana,maana alikuwa ni kama taahira na chanzo ni hizo dawa.Hapa ninapoishi kuna dada mmoja alipoteza fahamu kwa masaa kadhaa,katika uchunguzi Drs wakamwambia aache kutumia hizo dawa.Aisee hizo dawa hazifai kabisa
 
Watz wengi wana akili za mbayuwayu.
 
Unaposema kibiashara unamaanisha nini? Manake huduma ya uzazi wa mpango ni bure kwenye hospitali zote za serikali!
Kampeni nyingi za Uzazi wa mpango za kisasa, zimekaa KIBIASHARA zaidi na kimaslahi zaidi kuliko ukweli na uhalisia wa madhara yake..
 
Njia za jadi ndo hazina madhara otherwise think twice before opting those method
 
njia hizi zina madhara makubwa. mimi niliwahi kutumia vidonge vya kuhishia rangi ya ugoro nilikonda nikafanana mzimu, usiku nikilala nilikuwa najisikia kama nahishiwa pumzi.kama vile nakufa.mume wangu alikuwa anapata shida sana hamu ya tendo la ndoa ilinihishia.nilipoamua kuacha kutumia hivyo vidonge hiyo hali ikaisha.
 
Tumia kalenda , changaya uchunguzi wa ute jumlisha pattern ya joto, na usisahau kuwa na kondom kama mtataka ku.... Wakati wa danger days
 
Lazima hali hizo zitokee kwa baadhi ya Wanawake kwa sababu madawa hayo yanapoingia mwilini huenda kinyume na homoni za binadamu .Kila chenye faida kina hasara zake na kila chenye hasara kina faida zake.
 
Wengi wetu hapa tunatoa ushuhuda wa ATHARI ZA HII KITU,KWANINI SERIKALI INAHAMSISHA KUTUMIA,?NA KWANINI BADO WATU WANATUMIA????@WADAU
 
Ni kweli sana hawa wake zetu wana vitambi mpaka vinachosha, kwa ajili ya hii mipango ya uzazi mwanzo nilidhani ni vile vidonge vya Contraceptive lakini sasa bora kutumia mpango wa jadi

na matangazo ndo yanazid kuhamasisha,mzee yusuph na mkewe nao wanatumia uzaz wa mpango,si wanamuonesha kwenye maruninga yao,,,,,,inakuaje mtu mwanamke aliyetimia akose hedhi????nae anaish tu bila shaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…