Hatimaye Yanga yakabidhiwa kwa Manji aiendeshe kama club Binafsi

Hatimaye Yanga yakabidhiwa kwa Manji aiendeshe kama club Binafsi

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Wanachama Yanga wamkabidhi Yusuf Manji aiendeshe Yanga kama klabu binafsi, mikataba ya kumkabidhi nembo kusimamiwa na Baraza la Wadhamini.

Katika mkutano huo unaofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kipindi hiki, Manji amesema amepeleka ombi la kuikodisha Yanga kwa miaka 10.

“Nitaikodisha kwa asilimia 75 na 25 inabaki kwa wanachama. Nataka kuikodisha timu na nembo, majengo ya klabu yanabaki kuwa mali ya wanachama.

“Katika miaka 10, ikipatikana faida 25 inakwenda kwa wanachama na klabu na 75 kwangu. Kama itakuwa ni hasara basi inakuwa hasara yangu, hakuna hasara upande wa wanachama au klabu,” alisema.

Manji amesema masuala ya timu kuhusu usajili, mishahara, uendeshaji kama safari na gharama nyingine zitakuwa chini yake

Wakati huo huo, Wajumbe watatu wa Kamati Utendaji ya Yanga Ayoub Nyenzi, Hashim Abdallah na Salum Mkemi wavuliwa uanachama wa klabu hiyo.
 
Huu mwendokasi wa awamu hii kiboko, yani team mnaiendesha zaidi ya miaka 50 afu unakuja kumpa mtu ndani ya dk 10 tu yani vuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuup!!!!!!!!!! anyway muda ndo rafiki wa kweli.

mkuu hao wanahofu mno....baada ya Mo kuwekeza Simba. vyura nao wamekurupuka ili wapate cha kusema
 
Anaikosisha kwa sh ngp? I mean mtaji wake alioweka ni sh ngp?

Hyo asilimia 75, inathamani ya sh ngp? Isije kuwa manji anataka kuwauza yanga? Ikitokea tim ikashuka daraja je atafanyaje?

Yanga haja fikiria kwA umakini, kunahasara kuliko faida, hayo maamzi ya mwendo kasi yatakuja kuighalim yanga

Think
 
Am Young Dar African Sports Club,

Ila hapa naona tumeliwa mchana kweupeee, Unajua nini....?

Tunamkabidhi timu mtu for nothing..!!!, Hatujui anataka kuwekeza nini? Hatujui anataka kufanya biashara gani? Hakuna mkataba unaomfunga kwamba anatakiwa kujenga Uwanja wa Timu labda ndani ya kipindi hicho...!!!! Mkataba kwamba anatakiwa kununua angalau wachezaji wa kiwango fulani ndani ya kipindi husika hakuna...!!! Kwamba anatakiwa kuwekeza kiasi fulami kila mwaka ndani ya kipindi hicho hakuna....!!!!!!

Yaani mtu akienda huko kishumundu kutununulia kina Kibwanguso kama wachezaji wa Yanga, ni sawa tu....!!!! Hakuna cha kumbana..!!! Hapana.

Hapa tumeliwa kweupe hata jogoo hajawika!

Hii ni nafuu sana kwa watani zetu hapo ambao Mo amewaambia atawapa Bl 20. Na hata igusa hiyo wala faida yake ambayo itapatikana baada ya kukopeshwa hela hizo. Hii maana yake nini? Siku huyu mtu akiamua kuondoka Simba itakuwa imepata Bl20 na faida iliyopatikana baada ya kukopeshwa fedha hizo.

Huyu bwana ni mtu mjanja sana, Aliwekeza bure kabisa kwenye Club kwa kipindi cha karibu miaka sita sasa akilenga kupata hiki anachoomba leo, Ambacho binafsi ninaamini ni kikubwa kulinganisha na kile tutachopata kwa miaka hiyo kumi. Nembo tu ya Club inazaidi ya thamani ya trilioni moja...!!!!

Unajua nini......
Akimua kuuza maji tu yenye nembo ya club ya yanga angalau kwenye mechi moja tu ya club ya Yanga huku akifungia maji mengine kuuzwa kwenye mechi husika unajua fedha itakayopatikana? Achia mbali hilo akiamua kuuza tu Opener za soda zenye nembo ya club ya Yanga kwa miaka hiyo kumi unajua itapatikana bei gani?

Hapa sijazungumzia Jezi, Skafu, Soksi, Kofia, Miruza, Laba, Six........ Oooopssss

Ngoja niishie hapa mimi........!!!!!

BACK TANGANYIKA
 
Huu mwendokasi wa awamu hii kiboko, yani team mnaiendesha zaidi ya miaka 50 afu unakuja kumpa mtu ndani ya dk 10 tu yani vuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuup!!!!!!!!!! anyway muda ndo rafiki wa kweli.
umesahau yale ya edo na ukawa. watwanataka mabadilikooo
 
Am Young Dar African Sports Club,

Ila hapa naona tumeliwa mchana kweupeee, Unajua nini....?

Tunamkabidhi timu mtu for nothing..!!!, Hatujui anataka kuwekeza nini? Hatujui anataka kufanya biashara gani? Hakuna mkataba unaomfunga kwamba anatakiwa kujenga Uwanja wa Timu labda ndani ya kipindi hicho...!!!! Mkataba kwamba anatakiwa kununua angalau wachezaji wa kiwango fulani ndani ya kipindi husika hakuna...!!! Kwamba anatakiwa kuwekeza kiasi fulami kila mwaka ndani ya kipindi hicho hakuna....!!!!!!

Yaani mtu akienda huko kishumundu kutununulia kina Kibwanguso kama wachezaji wa Yanga, ni sawa tu....!!!! Hakuna cha kumbana..!!! Hapana.

Hapa tumeliwa kweupe hata jogoo hajawika!

Hii ni nafuu sana kwa watani zetu hapo ambao Mo amewaambia atawapa Bl 20. Na hata igusa hiyo wala faida yake ambayo itapatikana baada ya kukopeshwa hela hizo. Hii maana yake nini? Siku huyu mtu akiamua kuondoka Simba itakuwa imei

Hakuna afadhali hao wahindi wameona kuna fursa,wanataka kufanya biashara na watapata hela nyingi sana kwa mgongo wa hizi timu
 
Back
Top Bottom