ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Familia ya Nyalong ilitangaza mahari ya binti huyo kwa kumpiga mnada kulingana na tamaduni za jamii ya Wadinka
Ushindani huo uliwavutia wanaume sita na mshindi kutoa ng’ombe 520 na magari matatu aina ya V8
Mawakili wa kike wametaja tukio hilo kama ya kuwadunisha wanawake na kuwatumia kama kitega uchumi
Nyalong Ngong Deng, binti bikira wa Sudan Kusini mwenye umri wa miaka 17 kutoka eneo la Awerio ambalo zamani lilikuwa jimbo la Eastern Lakes ameolewa rasmi baada ya kuwavutia wanaume sita waliojitahidi kuwahi kumnyakua.
Nyalong alifunga ndoa na tajiri Kok Alat kwenye harusi ya kufana katika ukumbi wa Freedom jijini Juba siku ya Ijumaa, Novemba 9 na kutamatisha shughuli ya familia ya msichana huyo kumtafutia mume.
Nyalong aliketi karibu na mumewe akionekana kutekwa na mawazo mengi wakati wa harusi yao.
Mtu angeweza kuona hasira na hisia kuwa familia yake ilimsaliti kutokana na alivyokuwa kwenye hafla hiyo.Kabla ya harusi yake, familia ya Nyalong ilimpiga mnada kwenye zoezi la wiki mbili ambalo liliwavutia watu maarufu nchini humo.
Mumewe aliwashinda wapinzani wake watano waliotaka kumuoa Nyalong kulingana na tamaduni za jamii ya Wadinka kwa kutoa ng’ombe 520, magari matatu aina ya Toyota V8 na KSh 1 milioni.
Kamishna wa zamani wa jimbo la Aweria ambaye kwa sasa ni naibu wa gavana wa jimbo jipya la Eastern Lakes alikuwa mmoja wa waliowania kumpata kipusa huyo.
Katika tamaduni ya Wadinka, mwanamume yeyote anayetaka kumuoa msichana lazima aidhibitishie familia ya binti kuwa ana uwezo kwa kukidhi mahitaji ya msichana wao.
Wanaowania kumpata msichana huhojiwa kwanza kabla ya kupambana na mshindi kupewa mke.
Mawakili wa kike nchini Sudan Kusini wameitaka serikali ya nchi hiyo kuchunguza tukio hilo na kuwachukulia hatua wahusika wa mnada huo wa binti.
Mawakili hao walisema kuwa tamaduni hiyo ya Wadinka ni sawa na kutumia wasichana kama kitega uchumi.
Pia soma
www.jamiiforums.com

Picha: Mrembo Nyailong ambaye mahari yake ni ng'ombe 520 na magari 3
Urembo wa binti huyo wa miaka 17 kutoka Awerial lililokuwa likiitwa Lake State Sudan Kusini umewashangaza wengi na hata matajiri wamejitokeza kuomba uchumba. Kufikia mwisho wa Alhamisi, Oktoba 25, wanaume sita tayari walikuwa wameitembelea familia ya Nyalong Ngong Deng wakitoa ahadi za posa...