Elections 2010 Hatimaye Zitto atangaza kugombea Ubunge kwao

Elections 2010 Hatimaye Zitto atangaza kugombea Ubunge kwao

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
Hatimaye Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amefuta wazo la kuwania ubunge katika majimbo ya Geita, mkoani Mwanza na Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kutangaza rasmi kwamba, atatetea kiti hicho katika Jimbo lake la sasa.

Zitto ambaye alilidokeza Nipashe suala hilo mjini hapa juzi, alisema uamuzi huo angeutangaza katika mkutano wa hadhara, uliotarajiwa kufanyika nyumbani kwao, Mwandiga, Wilaya ya Kigoma, mkoani humo jana.

Alisema kuwa amefikia uamuzi wa kuendelea kugombea ubunge, baada ya kutafakari ushauri kutoka kwa watu mbalimbali, wakiwamo wazee wa Kigoma, washauri, viongozi wa chama na marafiki zake.

Alisema awali mapenzi yake yalikuwa atoke katika siasa ili afanye kazi anayoipenda ya kufundisha, kutafiti na kuandika, lakini umma ukamsukuma kufikiri upya.

“Nilipoamua kuwa nitagombea, nikapenda niwe ama Kinondoni au Geita. Wazee wa Kigoma, washauri wangu, viongozi wa chama na marafiki wakanishauri nigombee Kigoma. Sasa nimeamua kugombea Kigoma Kaskazini,” alisema Zitto.

Miongoni mwa watu waliomshauri Zitto kwenda kugombea kwao, Kigoma, ni pamoja na Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema.

Spika Sitta alimshauri Zitto suala hilo bungeni, Aprili 6, mwaka huu,

Spika Sitta alimtaka Zitto kuachana na wazo la kutaka kwenda kugombea ubunge katika Jimbo la Geita, badala yake akagombee nyumbani kwao Kigoma.

Spika Sitta alitoa ushauri huo muda mfupi kabla ya kumruhusu Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri, kujibu swali la nyongeza lililoulizwa bungeni na mwanasiasa huyo kijana kuhusu tatizo la maji linalowakabili wananchi wa Geita na vitongoji vyake.

“Kabla sijamruhusu Mheshimiwa Naibu Waziri kujibu, ningependa kumshauri Mheshimiwa Zitto agombee kule kwao, mambo ya Geita awaachie wenyewe,” alisema Spika Sitta na kusababisha karibu ukumbi mzima wa Bunge kuangua kicheko.

Katika swali lake la nyongeza, Zitto alitaka kujua serikali inachukua hatua gani za haraka kuhakikisha Halmashauri ya Wilaya ya Geita inapata maji ya kutosha ili kumaliza tatizo la maji kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Zitto aliuliza swali hilo, baada ya Mbunge wa Geita, Ernest Mabina (CCM), kuuliza swali la msingi akitaka kujua lini mji wa Geita na vitongoji vyake vitapewa maji ya uhakika.

Baada ya Mwanri kujibu swali hilo la Mabina kwa niaba ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji, alisimama na kuuliza swali la nyongeza kwa kuwahurumia wananchi wa Geita kutokana na tatizo la maji linalowakabili, kitendo ambacho kilimfanya Spika Sitta kumpa ushauri huo.

Siku sita baadaye, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Werema, aliungana na Spika Sitta, kumshauri Zitto kuachana na wazo la kutaka kwenda kugombea katika Jimbo la Geita, badala yake akagombee nyumbani kwao Kigoma.

Jaji Werema alitoa ushauri huo kwa Zitto, wakati akijibu hoja za wabunge, akiwamo Zitto waliochangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa Mwaka 2010, bungeni, Aprili 30, mwaka huu.

Jaji Werema alitoa ushauri huo wakati akimshukuru na kumpongeza Zitto kwa kutoa mchango mzuri katika mjadala wa muswada huo.

“Mheshimiwa Zitto nakushukuru sana kwa mchango wako mzuri. Wapo watu wanakunyemelea usigombee Kigoma. Na mimi nakushauri Kigoma. Kigoma ni kwenu kwa sababu titi la mama ni tamu hata kama ni la mbwa,” alisema Jaji Werema.

Jaji Werema na Spika Sitta walitoa ushauri huo, miezi michache, baada ya Zitto kukaririwa na vyombo vya habari akitaja majimbo matano ya uchaguzi yaliyoko Tanzania Bara na kusema anasubiri kupata taarifa za kutosha kupitia utafiti alioelekeza kufanywa na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) juu ya jimbo mojawapo atakalogombea katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.

Majimbo hayo ni Kigoma Kaskazini, Kigoma Mjini linalowakilishwa na Peter Serukamba (CCM), Kahama (James Lembeli-CCM) na Kinondoni (Iddi Azan-CCM).

Kutokana na hali hiyo, Machi, mwaka huu, ujumbe wa wazee wa Geita, walikwenda Kigoma kuomba Zitto akagombee jimboni mwao (Geita) kwa madai kwamba, ana uwezo wa kuwawakilisha.

Hata hivyo, katika majadiliano yaliyochukua siku kadhaa, wazee wa Kigoma walikataa ombi la wazee wa Geita na kuwataka wasubiri hadi baada ya miaka mitano.

Wakati huo huo, habari tulizozipata jana jioni kutoka Kigoma zilieleza kuwa mkutano huo uliahirishwa hadi kesho baada ya kumalizika kwa ziara ya Rais Jakaya Kikwete anayetarajiwa kuwasili mjini humo leo.


CHANZO: NIPASHE

My Take: Hivi Geita alikuwa anafuata nini? Madini?
 
Wazee wa Kigoma + Wazee wa Geita + Wazee wa Dar es Salaam = >????
 
Nampongeza Mhe Zitto kwa kuwa amefanya uamuzi wa busara
 
Hivi why Kila mgombea anashauriwa na wazee??? hakuna hata mmoja atakaeshauriwa na Vijana????? anyway mi natakia kila la Kheri Zito......
 
Namtakia kila la heri Zitto. Naamini atakuwa focused kwa maswala ya jimboni na taifa bila kuyumbishwa
 
Back
Top Bottom