GE2025 Hatma maelezo ya mashahidi wa siri Kesi ya Lissu kusomwa 'live' kujulikana leo Agost 18, 2025

GE2025 Hatma maelezo ya mashahidi wa siri Kesi ya Lissu kusomwa 'live' kujulikana leo Agost 18, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Agosti 18, 2025 imepanga kutoa amri kuhusu kurushwa mubashara kwa maelezo ya mashahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Pamoja na hilo, pia mahakama hiyo inatarajiwa kusikiliza maelezo ya mashahidi pamoja na idadi ya vielelezo vitakavyotumiwa katika shauri hilo wakati wa usikilizwaji wake.

Hatua hiyo ilikuja kufuatia Jamhuri kuieleza Mahakama kuwa kurushwa mubashara maelezo ya mashahidi kunaweza kuathiri uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu wa Agosti 4, 2025 uliobariki taarifa za mashahidi ambao ni raia katika kesi hiyo kupewa usiri.

Soma > Mahakama Kuu yapigilia msumari uamuzi kufichwa kwa mashahidi wa Jamhuri katika kesi ya Tundu Lissu

Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga alieleza kuwa kurusha mwenendo huo moja kwa moja ni sawa na kufanya uchapishaji wa ushahidi, jambo ambalo litakuwa kinyume na amri ya Mahakama inayolenga kulinda usalama na utambulisho wa mashahidi hao.
WhatsApp Image 2025-08-18 at 08.52.42_32ff4419.jpg


1755498095716.png
Lissu alipinga hoja hiyo akisema kuwa, Jaji alikataza kile ambacho kitamfichua shahidi, ambapo alisisitiza uamuzi wa Jaji Mtembwa kuwa ulieleza kuzuia utambulisho wao kutotolewa hadharani pamoja na anuani za makazi yao.

Hivyo Lissu alipinga na kuomba Hakimu kutokubali ombi lililowasilishwa na Mawakili wa Jamhuri ili kesi hiyo endelee kuwa mubashara (live).

Wakati wa usomaji wa maelezo ya mashahidi wa siri, kesi ya Lissu haitakuwa ‘Live’, vyombo vya habari navyo marufuku kuripoti.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Agosti 18, 2025 imetoa amri ya kukubali ombi la Jamhuri la kutoirusha mubashara (live streaming) mwenendo wa usomaji wa taarifa za mashahidi wa siri (committal proceedings). Imeelezwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuongeza uwezekano wa mashahidi hao, ambao utambulisho wao unafichwa, kujulikana.

Aidha, mahakama imetoa amri ya zuio kwa vyombo vya habari au mtu yeyote kutochapisha mwenendo huo bila kibali rasmi cha mahakama, au hadi pale itakapotolewa amri nyingine itakayotengua zuio hilo.

Hakimu ameeleza kuwa urushaji wa moja kwa moja (live streaming), usambazaji au aina yoyote ya uenezaji wa taarifa kuhusu mwenendo wa usomaji wa mashahidi wa siri unaweza kuathiri maelekezo ya Mahakama Kuu yanayotaka mashahidi hao wabaki kuwa siri ili wasiweze kutambulika.

Amesema taarifa hizo zitasomwa mahakamani mbele ya mshtakiwa, jambo litakaloheshimu msingi wa mahakama wa uwazi.

Hata hivyo, ameelekeza upande wa Jamhuri kuhakikisha kuwa taarifa za mashahidi wa siri zinahaririwa katika kiwango ambacho hakiwezi kusababisha utambulisho wao kujulikana, kama ilivyoelekezwa na mahakama.
 
Lissu aachiwe bila masharti,kesi ya Kijinga hii iliyoletwa na watawala waoga wa kushindana kwenye kura
 
DUNIA Haina Siri wapendwa, watoa ushahidi watajulikana mara tu baada ya kutoa ushahidi kwa majina Yao na sura zao.
Wachawi
Mapepo
Binadam wenzao
Naviumbe visivyo onekana Kwa macho, ndio chanzo Cha Taarifa.

Niko pale.......! Mtanibia
 
Duh hatari sana politico
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Agosti 18, 2025 imepanga kutoa amri kuhusu kurushwa mubashara kwa maelezo ya mashahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Pamoja na hilo, pia mahakama hiyo inatarajiwa kusikiliza maelezo ya mashahidi pamoja na idadi ya vielelezo vitakavyotumiwa katika shauri hilo wakati wa usikilizwaji wake.

Hatua hiyo ilikuja kufuatia Jamhuri kuieleza Mahakama kuwa kurushwa mubashara maelezo ya mashahidi kunaweza kuathiri uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu wa Agosti 4, 2025 uliobariki taarifa za mashahidi ambao ni raia katika kesi hiyo kupewa usiri.

Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga alieleza kuwa kurusha mwenendo huo moja kwa moja ni sawa na kufanya uchapishaji wa ushahidi, jambo ambalo litakuwa kinyume na amri ya Mahakama inayolenga kulinda usalama na utambulisho wa mashahidi hao.

Lissu alipinga hoja hiyo akisema kuwa, Jaji alikataza kile ambacho kitamfichua shahidi, ambapo alisisitiza uamuzi wa Jaji Mtembwa kuwa ulieleza kuzuia utambulisho wao kutotolewa hadharani pamoja na anuani za makazi yao.

Hivyo Lissu alipinga na kuomba Hakimu kutokubali ombi lililowasilishwa na Mawakili wa Jamhuri ili kesi hiyo endelee kuwa mubashara (live).
Mashahidi kufichwa haikuwa Ombi la Mahakama ila la Serikali.Kama Hakimu,Wakili mkuu Nassoro na mawakili wa Serikali hawajafichwa,iweje Mashahidi pekee wanafichwa?
 
Ama kweli hii ni serikali ya kihuni, kwann inataka mambo ya sirisiri?!.
Hii ni serikali au genge la wahuni
 
Lugha ya kiingereza pia itumike moja kwa moja katika kesi hii na hakimu, mshitakiwa, upande wa jamhuri.

Maana naona leo tarehe 18 Agosti 2025 jinsi kesi hii hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi mkuu ya Kisutu jijini DSM Tanzania anavyopata taabu sana kutumia lugha ya kiswahili, kwani kiswahili siyo lugha rasmi ya kisheria Tanzania kufafanua mambo mazito ya muendelezo na mchakato wa kesi hii ya kihistoria .

Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom