Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Najivunia sana watu Kama wewe.Elimu uliyoipata inatosha kukufikisha unakotaka kwenda. Maisha ni kuchagua na maadam umechagua biashara na una ridhiko la moyo na furaha, ndo maisha yenyewe hayo.
Najua utaendelea kuinuka na hata kuwa mmojawapo wa matajiri wakubwa hapa Bongo na pengine hata Afrika, lakini hata ikitokea biashara zikayumba hutajutia uamuzi wako, na utasimama tena na kusonga mbele.
Hao uliowaacha kwenye udaktari huko siku moja utawaajiri wawe madaktari wa familia yako. Ndo maisha!
Hongera kwa elimu uliyo ipata Ajira yenyewe hakuna.Habari za wakati huu wana JF
Leo naomba kushare jambo nanyi, coz naamini kuna watakaojifunza kitu hapa. Mimi ni kijana wa miaka 25, jinsia ya kiume. Nilianza elimu yangu ya msingi mwaka 2004 na kuhitimu mwaka 2010.
Nilibahatika kujiunga na masomo ya Elimu ya upili mwaka 2011 hadi 2014 nikiwa katika shule flani ya kata. Matokeo yalikuwa mazuri kwa upande wangu, Kwani nilipata ufaulu wa Alama "A" kwa masomo matano (physics, chemistry, biology, English na Mathematics) na B kwa masomo manne(history, kiswahili, Geography na civics).
Nilibahatika kujiunga na kidato cha tano mwaka 2015 katika shule moja Mkoani Dodoma, kwa masomo ya Physics Chemistry and Biology. (PCB).
Nilisoma kwa bidii sana kwani nilitamani kufanya maajabu zaidi. Mwaka 2017 nilitunukiwa zawadi ya kuwa mwanafunzi bora katika somo la Biology kwa kanda ya Kati. Kiukweli nilikula bata kwa siku tatu nikiwa na mkuu wa mkoa, afisa elimu mkoa pamoja na baadhi ya wanafunzi wenzangu walofanya vizuri kwa masomo mengne. Hii iliniongezea nguvu ya kupambana na CHANDS, BS, ROGER, UP, NELKON na vitabu vingine vya kunijenga kitaaluma.
Mwezi mei 2017, nilihitimu elimu yangu ya kidato cha sita na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya ulinzi na uzalishaji mali katika kambi ya jeshi ya RUVU JKT kwa mujibu wa sheria. Nilipata mafunzo hayo kwa muda wa miezi mitatu.
Matokeo yangu ya kidato cha sita yalikuwa hivi: Physics B, Chemistry B Biology A, Bam C na GS C. Hivyo nilikuwa na div 1 ya points 5.
Nilichaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kusomea fani ya Udaktari (Medical Doctor) mwezi November 2017.
Nilianza vyema nikiwa na furaha sana kufikia level hiyo ya elimu.
Nikiwa mwaka wa kwanza nlipata rafiki alokuwa mwaka wa 5. Alinisihi sana kujiongeza ktk kubuni njia yyte ya kunipa kipato nikiwa chuoni kwani yeye alikuwa na saluni ambapo alifanya kazi kwa muda wa ziada na alifungua duka la vipodozi mtaani Ng'ong'ona, maarufu Kama UJASI kwa wanaopaelewa. alitengeneza pesa ndefu sana kwa muda mchache.
Kidogo na mimi nilianza kuumiza kichwa kujua ntafanya jambo gani nikajipatia kipato nje ya fedha za mkopo. Nilifanya research juu ya biashara ya nguo za kiume na nilianza kidogo kidogo kuagiza mzigo na kuuza kwa kutembeza hostel. Nilifanya hivyo kwa muda wa miezi sita na nikaona mwanga kwa mbaliiii kwani mzigo uliisha haraka na ni kwa faida nzuri tu. Mtaji uliongezeka kutoka 1.2M hadi 3.6M kwa muda huo. Nlifungua frem na kuanza rasmi safari ya two in one. Yaani huku masomo na huku biashara..... Nlipata msimamizi ambaye aliisimamia vizuri biashara na ilipaa vizuri.
Nilimaliza mwaka wa kwanza nikiwa na GPA ya 3.2 na niliendelea mbele. Mwaka wa pili ulikuwa ni mwaka mzito sana kwangu, kwani masomo yalichanganya kwa kasi ya ajabu sana huku akili yangu ilishatekwa na biashara. Nilijikuta nikizingatia zaidi biashara kuliko masomo. Nilikuza scale yangu ya kibiashara, nikafungua duka la viatu vya kiume palepale mtaani.
Biashara ilipamba sana moto, kwani nilikuza msingi hadi 12M ndani ya mwaka mzima. Tulifanya mtihani wa kumaliza mwaka wa pili, na hapo nilihisi kuwa sitofanya vyema coz mitihani yote ilikuwa na maswali ambayo sikujua hata nijibu kitu Gani. Hivyo nilibeti tu, na nlisubiri maajabu ya Mungu, kunibeba or kunibwaga.
Kipindi chote cha likizo nilitumia muda wangu wote kariakoo kutengeneza channels na wafanyabiashara wakubwa. Matokeo yalitoka na yalikuwa hv: GPA 1.5 DISCONTINUED reason: GPA is below an average.
Binafsi sikustuka kivile coz nilishajiandaa kisaikolojia toka siku nakumbana na mitihani ilokuwa na maswali yasokuwa na mujibu kichwani mwangu. Nilijitahidi sana kuuzuia moyo wangu kupata taswira halisi ya hatima ya matokeo mazuri ya kidato cha nne na sita. Niliwashirikisha marafiki zangu wachache katika Hili, na niliendelea na biashara kwa spirit ya juu zaidi.
Mpaka sasa namshukuru Mungu coz amenipa moyo wa kukubali yalotokea, na amenifungulia njia zaidi, kwani nimeadvanc kwa kiwango cha juu sana. Kwa sasa nina duka la simu za aina zote, na naendelea na biashara ya nguo na viatu.
I hope wa kujifunza jambo kajifunza.
Muwe na wakati mwema wana JF.
www.jamiiforums.com
Atakuwaje na wasiwasi wakati A'level cheti PCB 1-5 Chuo chochote anaenda ht km ndoto zake zikiwa medicine anaweza omba upya vyuo vingine. Hukufeli sababu ya masomo magumu bali sababu ya muda mwingi kutafuta pesaHongera kiongozi[emoji122].. Fanyia kazi huyo ushauri wa kusomea kadegree chochote hata Uchumi au Management