Ilipoishia
Caryn: "Ooh nice, jibu zuri sana...Mimi maamuzi niliyoyachukua nilikusimamisha kazi, unajua ni kwanini nilikusimamisha kazi?"
BM: "Hapana, sifahamu"
Caryn: "Pengine ulikuwa na mentality ya kwamba bila ya wewe mambo hayaendi, so niliamua kukusimamisha makusudi ili kukuonesha kwamba bila ya uwepo wako mambo yanaweza kwenda tena vizuri tu"
Caryn: "We unadhani kwanini nilitaka kwenda na wewe Zanzibar? Kama ulikuwa hujui mimi nilienda kule kwa ajili ya kutengeneza Back up, Kila ninachokifanya mimi lazima niwe na Backup plan"
Dah! sikuwaza hili Jambo, Aisee kumbe Ile trip ya Zenji niliyoenda na Caryn kumbe mwenzangu alienda kutengeneza network yake, so kwenye Ile trip alijuana na maagent na maafisa wa TRA, hadi ZBS kote huko mawasiliano anayo, Yani Dah niliishiwa nguvu nyie nikakosa hata cha kuongea
Caryn: "Halafu mm najua kama unaiibia Kampuni ila nilijifanya mjinga nikatulia, kona zote unazopita mimi nazijua, kama utabisha mimi ushahidi ninao"
Muendelezo
(Episode 18, SEASON 2)
Mwezi mmoja baada ya Mwaka mpya 2023 kuingia yani mwezi February ndio ukawa mwezi wa kutimiza Ile miezi sita niliyopewa ya kumuongoza kijana wa Buguruni
Nakumbuka ilikuwa siku mbili kabla ya Valentine day nilienda na Kijana wa Buguruni kwa Mzee, hii ndio Ile siku ya Judgement
Tulivyofika kwa Mzee tukakaribishwa vizuri japokuwa mimi ni mwenyeji hapa nyumbani ila Kijana yeye ndio mara yake ya pili kuja kwa Mzee, tukala msosi na story mbili tatu pale Dinning table baada ya kumaliza kula Mimi, Kijana wa Buguruni pamoja na Mzee tukaelekea Backyard
Mzee: "Okay, so umesema mnataka kufungua Workshop"
BM: "Ndio Mzee"
Mzee: "Una uhakika kijana yupo vizuri? tusije tukatupa Pesa zetu"
BM: "Naamini yupo vizuri Mzee"
Mzee: "Hebu nipishe niongee nae kwanza nitakuita nikimalizana nae"
Mzee anataka kuongea mambo gani tena ambayo sipaswi kuyasikia? Nilijiuliza tu moyoni ila niliwapisha kama Mzee alivyotaka, Nikarudi Sebuleni na Dada wa kazi Michelle hayupo wala Càryn, sio kwamba wametoka tu mara moja then wanarudi, hapana! Wote wawili hawaishi hapa nyumbani siku hizi Mzee alishawatimua
Pale sebuleni nikaona hamna issues Dada mwenyewe anaangalia tamthilia gani sijui za Maisha Magic nikaamua kutoka zangu tu nje kupiga story na mlinzi
Mlinzi: "Karibu Kiongozi"
BM: "Aah, mm sio Kiongozi bhana viongozi wapo Bungeni huko"
Mlinzi: "Sasa bro unataka nikuiteje maana majina yote unayakataa"
BM: "Niite kama ulivyoniita sasa hivi Bro hiyo inatosha, hayo majina yako unavyopenda kuniita Mkuu, Kiongozi, sijui Boss hapana aise"
Mlinzi: "Sawa Bro, uko poa lakini?"
BM: "Yeah niko Poa, ivi ni kwaajili gani wewe hawakubadilishi hapa kama walivyokuwa wanawafanyia wale wa mwanzo"
Mlinzi: "Ni kama Mzee alikataa, kwanza wakinibadilisha kituo na kazi yenyewe ya ulinzi naacha"
BM: "Kwanini"
Mlinzi: "Najua siwezi kupata sehemu yenye masilahi kama hii"
BM: "Unajua kuna mwenzako Mzee alimchukua kampeleka town kwenye Kampuni yake Sasa hivi anakula mia nne" (400k)
Mlinzi: "Mimi siwezi kukubali"
BM: "Na kwanini ukatae? hii ndio dream job yako nini bro!"
Mlinzi: "Sasa huyo anaelipwa laki nne mimi hanifikii hata kidogo japokuwa kimshara hatujapishana sana kimatumizi ndio kuna tofauti"
BM: "Wewe unalipwa shilingi ngapi kwani?"
Mlinzi: "Mimi nalipwa mara mbili ndani ya mwezi mmoja"
BM: "Ndio shilingi ngapi si useme"
Mlinzi: "Kampuni inanilipa laki mbili na nusu na Mzee Kila mwezi ni lazima anipe laki 2"
BM: "Kwahiyo Mzee wangu kwa mwezi jumla unapokea mia nne unusu (450k), hamjapishana sana hata hivyo"
Mlinzi: "Sasa mimi katika hiyo laki nne na nusu naweza kutumia elfu hamsini tu pekee laki nne yote nika save, kwasababu mimi kula free na kulala sidaiwi kodi"
BM: "Duh! kweli unaupiga mwingi sana, ukiwa hapa kwa haraka haraka mtu anaweza kukuona kama unapoteza muda ivi"
Mlinzi: "Ningekuwa na elimu kubwa kidogo hapo sawa hata nikisema nije kujichanganya kwenye hizo Kampuni zenu lakini kwa elimu yangu siwezi kutengeneza pesa kama ninavyotengeneza nikiwa hapa"
BM: "Hujui Kuna kazi za madili? watu hawaishi kutegemea mshahara siku hizi"
Mlinzi: "Si mpaka upate sasa hayo madili"
Simu yangu ikaita, kucheki [emoji1702] ni Mzee, nilivyopokea akanambia naweza kwenda ameshamalizana na Kijana, Ikabidi niachane na Mshkaji (mlinzi) pale Parking area nikarudi kwa Mzee Backyard
BM: "Vipi Kijana kaenda wapi?"
Mzee: "Nimemruhusu akakae sitting room"
BM: "Ooh Okay"
Sasa Mzee bhana zumuni la kuniondoa kumbe alikuwa anataka kumuhoji baadhi ya vitu kijana kutaka kujua maisha yake kiujumla kwa sasa yanaendaje
Mzee: "Nimependa hukumuambia kijana kwamba kufeli kwake ndio kufeli kwako kwasababu kama angejua angefanya vitu under pressure"
Mzee: "Ila pia nimependa wazo la kumpatia ujuzi, umefikiria kwa utofauti kidogo hukutaka kufanya kwasababu tu ya ahadi iliyopo mbele yako bali umemfikiria zaidi kijana pamoja na maisha yake, nini anapenda nini hataki,"
Mzee: "Akili uliyotumia kufanikisha ni kubwa kwasababu unaweza kufanikisha Biashara kukua ndani ya miezi sita lakini ugumu ungekuja kwenye sustainability tena kwa kijana ambaye hana elimu ndio ingekuwa worse zaidi though ina depend na aina ya Biashara pia"
BM: "Nimefurahi kusikia hivyo Mzee sikutegemea kwakweli kama mapokeo yatakuwa ya namna hii"
Mzee: "Lakini umejidhihirishia kwamba yuko vizuri kwenye kutengeneza hizo vitu? wasiwasi wangu ndio upo hapo"
BM: "Kijana yupo vizuri, si umeona hata picha Mzee"
Mzee: "Picha haitoshi kupima uwezo wake, itabidi kabla sijaamua kufanya maamuzi yoyote ya kiuwekezaji inabidi nimpe kazi anitengeneze mimi kwanza, niwe mteja wake wa kwanza nikiridhishwa ndio tunaweza kufikiria kufanya hayo mengine"
Dah! mtihani juu ya mtihani nilijua mambo yameisha kumbe ndio Kwanzaa yanaanza,
Kazi aliyopewa Kijana sasa ni ya kutengeneza Sofa set flani ivi Mzee alituoneshea kwenye picha, hii siku kabla ya kuondoka kijana aliulizwa materials yote yanayohitajika ili kukamilisha hiyo kazi
Kijana akataja vitu vyote vinavyohitajika hadi vifaa ikiwemo Mashines za kushonea pamoja na makololo yote, na Mzee akavinunua vitu vyote, milioni 4+ ilikatika
Vitu vyote vikapelekwa kwa Mzee kwasababu kazi ilitakiwa ifanyike huko, Mzee alichokifanya akaenda kuprint Ile picha akaibandika ukutani kule Backyard ili kijana acheze nayo
Ilivyofika tarehe za mwishoni mwa mwezi February kijana ameshamaliza kazi, Mzee aliniita kwake chakusikitisha ni kwamba Baba yake Caryn hakuzipitisha sofa zilizotengenezwa na Kijana Buguruni
Mzee: "Hata hivyo kijana amejitahidi sana, tangu nampa hii kazi nilijua kabisa hatofikia viwango ninavyovitaka lakini pia sikutegemea kama angefanya kitu kizuri namna hii"
BM: "Yeah, amejitahidi"
Mzee: "Kwa ushauri wangu arudi tu hapo alipokuwa anajifunza kazi ili aendelee kupata ujuzi na Experience zaidi..."
BM: "Sawa Mzee haina shida"
Basi Mzee akanambia nichukue zile sofa niziuze na Pesa itakayopatikana niongezee Ada pamoja na matumizi ya kawaida ya wale watoto (wadogo zake na Kijana wa Buguruni) na vile vifaa vyote akapewa Kijana kwaajili ya matumizi ya Kazi zake
Jumamosi ya tarehe 25 mwezi wa pili juzi kati tu hapa nakumbuka tena niliwaahidi kuleta muendelezo jumapili yake yani tarehe 26 lakini sikufanikiwa kwaajili ya hii safari watu wakanimaindi
Ubaya wakati naondoka sikuwajulisha humu ila wakati niko Mwanza ndio nikaweka wazi kwamba nimesafiri na hiyo ni baada ya kuona mapovu yamezidi kuwa mengi kwasababu sikuweka muendelezo siku niliyowaahidi
Anyway, Mzee ni kama alinishtukiza flani kwenye hiyo safari akanambia nijiandae tunaenda Mwanza,
Tukaanza safari ya kuelekea Mwanza, nakumbuka tuliondoka Dar mida ya saa tano usiku tukafika Dodoma saa kumi alfajiri, (Mzee ndio anapiga gia hapo) tulipofika Singida tukapaki sehemu tukaenda kunywa chai
Tumemaliza kunywa chai Mzee akanirushia funguo kwamba mimi ndio niendeshe, sikupinga kwanza chuma yenyewe nilikuwa naitamani tangu tunatoka Dar
Mzee: "Najua hujawahi kuendesha safari ndefu kwahiyo kuwa makini zaidi hasa hasa haya mabus muda huu tutapishana nayo mengi"
Nikamuambia Mzee haina shida, nikakaa kwenye Steering ya Lexus LX 570 chuma ya Mwaka 2018, ndio kwa mara ya kwanza naendesha LX 570, kwakifupi kilometers zilizobaki kutoka Singida hadi Mwanza nilizimalizia mimi na tukafika Mwanza saa sita mchana na Dakika zake
Tukaimalizia Ile siku ya jumapili hotelini Jumatatu yake Mzee akaonana na watu wake sikuwahi kuwaonaga ila hao watu wanadili na madini kwanza mipira yao sio ya kitoto,
Kama kuna huyo mmoja alikuja pale hotelini na Land Rover Discovery ya 2022, hadi nikaanza kumpeleleza Mzee kuhusu huyo jamaa mwenye Discovery Mzee akaniambia yule mshua kumbe anadili na mambo hayo hayo ya madini sema kazi zake amebase sana Kenya na Nyamongo Tanzania
Wale wengine wawili wao wanafanya tu Biashara ya kuyauza hayo madini, mipira yao wale wawili ilikuwa sio ya kutisha sana mmoja alikuwa na Jaguar na mwingine alikuwa na VXR V8
Halafu kitu kingine nilichogundua kuhusu hii Trip ya Mwanza, Mzee alikuwa ni mtu sana wa Starehe au pengine hadi sasa ni mtu wa starehe ila hadi akutane na kampani kama hivi
Nakumbuka siku 2 kabla ya kuondoka Mwanza wale rafiki zake Mzee walifanya matusi pale Mwanza, Usiku mmoja tulihama viwanja vitatu tofauti
Tulianza na City Link ipo maeneo wanaita Buswelu, kwanza wakati tupo kwenye gari tunaenda huko City Link Mzee akaniuliza
Mzee: "Huwa unatumia pombe"
BM: "Ndio lakini si mara kwa mara"
Mzee: "Usiogope kama ni gari nitaendesha mwenyewe"
BM: "Yeah, huwa natumia lakini sio mara kwa mara"
Mzee: "Ooh, sawa lakini hata kama ukinywa kunywa kwa kiasi, usinywe kwa kuiga hadi ukapitiliza maana pombe tunazokunywa sisi ni Kali sana"
Mimi moyoni nikajisemea hizo hizo kali ndio nzuri kwasababu mimi mwenyewe huwa situmii Bia, siku nikiamua kunywa vitu vyangu huwa ni mwendo wa JJ tu yani Jagermeister au Jameson
Tukafika City Link Ukiachana na ile Crew ya Mzee pia kuna vijana wengine wanaofañya kazi migodini waliongezeka, vijana wadogo tu lakini ndinga zao si haba, wanapush Crown na hizi BMW 3 series ndio niliziona kwa sana
Ila kwenye Ile Crew ya Mzee yule mshua mwenye Land Cruiser VXR V8 haku-show up, wale wengine wawili walikuja, mwenye Jaguar alikuja na Jaguar yake na yule Mshua wa Discovery yeye alikuja na Prado TX ya white na sisi tuko na gari yetu tu ile Ile Lexus
Pale City Link Washua walipaona kama pamepoa, tukahamia kiwanja kinaitwa Kwatunza Beach sasa hapa ndio watu wakaanza kupiga sherehe, watu tulikuwa wengi kidogo ilibidi tujigawe katika makundi manne (Meza 4)
Mimi nilikaa kwenye Meza ya Washua, Hennessy zikaanza kushushwa, kwenye Ile meza ya Washua alikuwepo na jamaa mmoja mweupe ana ukaribu sana na yule mshua wa Discovery halafu huyu mshua wá Discovery ndiye aliyekuwa analipia Bills za meza zote 4
Tukapiga gambe na nyama choma, tulikaa kama masaa mawili tukaondoka pale Tunza, sasa wakati tunaelekea tulikopaki magari yule mshua wa Discovery akamwambia yule jamaa wa white aje kupanda kwenye Lexus ya Mzee halafu Mzee akapande Prado TX ni kama walikuwa na mazungumzo yao Confidential
Sasa wakati tupo kwenye gari yule jamaa wa white (Chawa wa mshua wa Discovery) Tukaanza kupiga story
BM: "...Kwahiyo unaniambia kila weekend haya ndio matusi mnayoyafanya"
Chawa: "Sio kila weekend lakini weekend ambazo zinamkutia Mwanza yule jamaa sio chini ya milioni 5 anazimaliza ndani ya usiku mmoja"
BM: "Duh! Milioni 5 anamalizaje kwa usiku mmoja"
Chawa: "Si kama vile ulivyoona, kwanza ukienda nae sehemu yeyote ya Bata hawezi kukuruhusu ukalipia bill, siunaona kama Leo yupo na Wababe wenzake lakini yeye ndio anasimamia show"
Chawa: "Ivi unajua ukiachana na zile meza zingine 3 walizokaa washkaji Kuna meza zingine 2 walikuwa wamekaa mademu tu yeye ndio alikuwa analipia"
BM: "Mademu zake sio?"
Chawa: "Mademu wenyewe unadhani wote anawagonga basi, pale anagonga manzi mmoja tu"
BM: "Kwani yeye hizi pesa anazipata kirahisi aje?"
Chawa: "Acha kabisa inafika mahala mtu anatumia pesa zake lakini wewe ndio unaumia kwa kuzionea uchungu"
Jamaa aka Chawa akanambia kuna siku walienda Club Elevate Malaika na Mshua wa Discovery (ambako ndipo tulipokuwa tunaelekea muda huo) Sasa walivyofika hapo Elevate Mshua akatoa maagizo kwamba Kila meza wahudumu wapeleke Martell mbili mbili halafu Bill ni kwake
Chawa anakwambia alimuambia Mshuâ.....ngoja nimnukuu maneno yake maana alinichekesha sana "Nilimuambia bro hii Pesa yote si Bora ungemtumia Mama, akanijibu Mama yake kashamtumia ikabidi nikaushe tu"
Kwanza Chawa anakuambia kwa mahesabu ya haraka haraka siku hiyo meza zilikuwa zaidi ya 30 halafu anakuambia hata kàma meza moja Ina mtu mmoja au wawili basi Martell zinashushwa 2 kama alivyoagiza utajua mwenyewe unamalizana nazo vipi
Basi Bhana tukafika Malaika Hotel. sasa mimi nikawa naifuata TX Chawa akanambia "Bro usimfuate yule ww Park zako tu huku kwenye Parking ya kawaida"
Nilivyohoji Kwanini Mshua pekee ndio kaingiza Gari ndani Chawa akanambia kwamba Ile ndio kawaida yake Kila anapoenda pale, Gari yake ni lazima iingie ndani kabisa sehemu wanayokaa watu, Chawa anakwambia eti mshua akimwagilia moyo basi anataka na gari yake awe anaiona
Ilibidi tupaki huku Regular ambako pia usalama upo wa kutosha tu.
Çhawa: "Oya tukifika tuikatae meza ya Washua twende tukajichanganye wana"
BM: "Kwanini?"
Chawa: "We unadhani kwanini kwenye gari wametaka kuwa peke yao, sometimes inabidi ujiongeze ujue kucheza na akili za hawa watu ili siku nyingine kwenye mitoko yao wasikupunguze"
Nikaona logic ya kile anachokiongea lakini sasa nikaona namna alivyoongea ni kama amenichukulia mimi kama Chawa mwenzake kwa maana ya kwamba na mimi ni Chawa kwa Mzee
Tukachoma ndani kweli tukaikataa Ile meza ya Washua tukaenda kujichanganya kwa wana ambao tupo nao msafara mmoja, Mshua wa Discovery akaja kwenye Meza yetu akatuambia Kila mtu aagize kinywaji chake na hakuna kushea na mtu, Yani kama unaagiza Jameson basi hiyo ujue ni ya kwako hakuna kushea na kama haikutoshi ruksa kuongeza
Mimi kwavile mwanzo nilianza na Hennessy sikutaka mambo mengi nikaagiza hiyo hiyo Hennessy, Jamaa mwingine akaagiza Martell, mwingine akachukua Absolute Vodka, yule Chawa sasa kumbe hatumii pombe kabisa ila ukimuona vibe lake sasa utadhani kapiga chuma la Jameson peke yake
Chawa akawa anapiga zake Bavaria, tukapiga maji hadi mida ya saa nane usiku tukaondoka, ila yule jamaa aliyeägiza Jagermeister hamuezi amini aliimaliza peke yake sisi wengine tuliobaki tuligawa pombe zetu na kumbuka huko tulipotoka tulianza kupiga Mma
Kesho yake tulipumzika ila cha kusikitisha ni kwamba hadi tunaondoka Mwanza sikuonana na Annie uzuri sina lawama katika hilo sababu wakati naenda sikumjulisha
Hatimaye tukafika Dar, tulivyofika town hatukuenda moja kwa moja nyumbani tukapitia Car Wash flani ipo maeneo Mikocheni Sasa Wakati gari inaendelea kuoshwa Mzee akanishtukiza na habari nzito kidogo japo haikuwa exclusive kwangu
Mzee: "BM nataka uende ukasimamie Kampuni kule China.....siunajua (Jina) mwezi wa sita anahamia Marekani"
BM: "Mzee ww unahisi nitaweza kweli?"
Mzee: "Ndio maana nataka uende mapema ili hii miezi miwili iliyobaki (Jina) awe anakuelekeza baadhi ya mambo"
Kwakufupisha story Mzee nilimkatalia safari ya kwenda huko china kwa kumpa sababu za uongo na kweli, Kwanza Mzee hakuamini kama ningeweza kuikataa Ile offer lakini hata hivyo mimi mwenyewe nimeikataa ofa huku nikiitamani ni kwa vile tu nilikuwa Sina namna nyingine zaidi ya kuikataa
Turudi kule tulipoishia episode iliyopita (episode 17) ili kujua kwanini nilikataa kwenda China
Itaendelea