Ilipoishia
Ilivyofika Weekend, Jumapili asubuhi Caryn akanitaka niongozane nae kwenda kwao, nilimkatalia sababu nilikuwa na misele yangu mingine, japokuwa sikwenda kwa Mzee karibia wiki tatu sasa inakaribia
Mimi nikaenda kwenye misele yangu na Caryn akaenda kwao, ilivyofika jioni tukakutana Nyumbani, namuuliza "vipi Mzee na Bi Mkubwa hawajambo?"
Caryn: "Yani bora hata hatukwenda wote"
BM: "Kwanini?"
Caryn: "Nisikilize kwa makini, siku yoyote kuanzia leo Dad atakupigia simu uende nyumbani, sasa kabla hujaongea na Dad nataka tukubaliane kitu kimoja"
BM: "Kitu Gani?"
Muendelezo
(Episode 23, SEASON 2)
Caryn: "Anyways, tuachane na Dad kwanza, ivi nikuulize ikitokea opportunity ya kwenda kufanya kazi na kuishi abroad utakubali?"
BM: "Hapo itategemea na nchi yenyewe"
Caryn: "Like UK, German or China"
BM: "Kwa hizo nchi ulizozitaja, kazi itakuwa ni kuhangaikia visa tu maana passport ipo tayari"
Nikiwa na maana ya kwamba Niko tayari kwenda bila ya kupoteza muda, nilivyojibu vile Caryn akatulia kama sekunde kadhaa halafu akanambia
Caryn: "Okay, sio mbaya but hiyo ni best option kwa mtu aliyeshindwa maisha kwao, ila kwa wewe sidhani kama ni sahihi kufanya hivyo coz you're doing well over here"
BM: "Lakini pia kwenda kuishi nje ya nchi haimaanishi kwamba umeshindwa maisha hapa Tanzania, japokuwa huo ni uhalisia kwa wengi lakini sio wote"
Caryn: "Okay, I'll go straight to the point, Dad anataka uende China, ukasimamie Kampuni huko ila..."
BM: "Subiri kwanza haina haja ya kuendelea....Do you know how it feels for a star to drop out of the sky and land right at your feet, that's how I felt, that's how I'm feeling right now after breaking hiyo news"
Caryn: "I don't think it's good idea"
BM: "Why?"
Caryn: "As I Said, hiyo ni best option kwa mtu anayejitafuta lakini sio wewe"
BM: "Unajua sikuelewi, kwahiyo wewe unatakaje?"
Càryn: "That is the question I have been waiting for you to ask"
BM: "Enhe! Nakusikiliza"
Caryn: "Usikubali kwenda"
BM: "Kwasababu gani za msingi?"
Caryn: "Utanielewa badae, ila kwasasa Mzee akikuita we mkatalie"
BM: "Caryn skia mimi sio mtoto unajua, so we niambie ni kwanini nikatae hii offer, sitaki disappointment hapo badae coz hiyo badae unayotarajia nikuelewe naweza nisikuelewe"
Caryn alivyoona niko serious, akanipa sababu zake kwanini anataka nisiende china na nikamuelewa kwakweli lakini pamoja na kumuelewa bado Ile offer nikawa naitaka ila ndio hivyo nitafanyaje tena
Tangu siku hiyo nikawa nasubiri simu ya Mzee lakini hola, weekend iliyofuata nilienda kwa Mzee kusalimia maana imepita kitambo kidogo sikwenda, nilivyoenda nikaonana na Mzee na kupiga nae story mbili tatu huku nikitegemea approaching yake kama Càryn alivyoniambia
Nakumbuka hii siku nilikaa na Mzee sitting room (sebuleni) tulikuwa tunaangalia Television tukaona taarifa Kuna jamaa Nigeria kahukumiwa kwenda jela kwasababu Kuna raia wawili wamekutwa wamefariki na chanzo Cha kifo unaambiwa ni msosi waliokula kwa huyo jamaa, Ile taarifa ikanikumbusha mbali kidogo, ilinikumbusha Ile siku nilivyogawa chakula kwa wale watoto wa mitaa
Nikamuambia Mzee "Ukute jamaa (aliyehukumiwa kwenda jela) hakujua kama chakula kina sumu lakini mahakama ndio ishaamua"
Mzee: " Na ndio maana Mungu anatuhukumu kwa Nia (Intent)
Mzee akaendelea kusema "Inabidi ujifunze kufanya ipasavyo kuliko kufanya Mema au Mabaya kwani anayefanya Mema si Mwema, anayetenda Mabaya si Mbaya.
Mwema ni yule asiyewaza mabaya, anayefanya Mema akiwa anawaza vibaya ni Mbaya, anayefanya mabaya akiwa anawaza Mema ni Mwema"
BM: "So kwa Mungu yule jamaa hana kesi"
Mzee: "Hana kesi, kama alikuwa hajui kama chakula kina sumu, lakini kwa Duniani ni tofauti, wataku-judge kwa matokeo ya matendo yako"
Tukaendelea na mazungumzo na hadi tunamaliza Mzee hakugusia swala la China wala Gwanzuu,
Jumamosi ya mwisho ya mwezi wa pili Mzee akanivutia waya, akanitaka nijiandae kwaajili ya safari na safari yenyewe ni siku hiyo hiyo, basi master nikajiweka sawa sasa wakati najiandaa nilikuwa na Caryn yeye ndiye aliyenichana kwamba safari ni ya kwenda Mwanza
Tukafunga nyumba tukaondoka, nikiwa sipo hata nikienda tu hapo Zanzibar Caryn huwa halali kwangu huwa anaenda kwao au kwa Dada yake, na katika kufanya hizo movements humkuti amebeba begi la nguo kwasababu nyumba zote hizo ana nguo na kila kitu chake anachohitaji kukitumia
Tumefika kwa Mzee Ile tunaingia ndani Tukawakuta Mzee na Bi Mkubwa wanaongea, tukasalimiana baada ya kuitikia salamu zetu Mzee akamuuliza Bi Mkubwa "Ivi ushaenda kupaona kwa wanao wanapokaa?" Bi Mkubwa akajibu alivyojibu, Mimi na Mzee tukatoka nje
Mzee: "BM tangu wakina Michelle waondoke, ujio wako hapa nyumbani umekuwa wa kusua sua"
BM: "Ni majukumu tu Mzee"
Mzee: "Oh! kama ni majukumu yanakufanya uwe busy basi ni vizuri maana unajua kuwa Available everywhere and Anytime inapunguza heshima, siku zote Distance inatengeneza hadhi, Mungu yupo mbinguni hebu angalia distance hiyo nani hata muheshimu (wote tuna muheshimu)
BM: "Mzee kwahiyo una maanisha hata hapa kwako nisiwe nakuja mara kwa mara ili niweze ku maintain hadhi yangu?"
(niliongea kwa njia utani lakini nikiwa namaanisha nilichokuwa naongea)
Mzee: "Hapana, namaanisha kwamba kitu chochote ambacho kinapatikana kwa nadra kina hadhi"
Mazungumzo yanaendelea huku Mzee anakagua gari, akamuita na mlinzi kuna maagizo akampa then akamuaga, tuliondoka nyumbani saa moja usiku tukaenda kukaa mahali Mzee alikuwa anapata kahawa, Mimi nikapiga msosi kabisa baada ya kumaliza tukakaa kaa pale hadi mida ya saa nne kama sio saa tano, Mzee akaenda washingroom alivyotoka safari ikaanza
Mzee: "Yule kijana alikuwa na shida gani?"
BM: "Ah, ni vijana wetu hawa wa mtaani alikuwa anaomba pesa akale"
Mzee: "Vijana wa siku hizi sijui wana shida gani, hawawezi kufikiria vitu vya kufanya na ni wazima wa afya, option yao iliyobaki ni kuomba, baadhi ya walemavu wanafikiria vitu vya kufanya pamoja na ulemavu wao kwasababu wauelewa"
BM: "Wana uelewa? uelewa gani?"
Mzee: "Wanaelewa kwamba mwisho wa uwezo wa kufikiria ndio mwanzo wa matatizo, yani Binadamu akiacha kufikiria ndio matatizo yanaanza
BM; "Hiyo Ina maana kwamba hawaichukulii hali yao ya ulemavu kama tatizo"
Mzee: "Wanaochukulia hali hiyo kama tatizo ndio matatizo yao yanaanzia hapo, ukisema Mimi siwezi kufanya kitu flani kwasababu sina connection (vijana wa siku hizi mnadai Kila Kitu ni Connection) tayari unakuwa ushai-limit akili yako kufikiria zaidi, mwisho wa siku mambo hayawezekani kweli"
Story ziliendelea huku Mzee akipiga gia, hapo katikati mimi nikalala tulivyofika Singidani asubuhi nikamsaidia kuendesha hadi tunafika Mwanza, siku zote nilizokaa Mwanza hadi naondoka sikuonana na Annie na nilifanya hivyo kwa makusudi kabisa,
Tulivyorudi Dar Mzee ndio akanipanga kuhusu safari ya China, kama mnakumbuka Episode ya 18 ndio iliishia hapa, tukarudi kwenye matukio ya Mwaka jana ambayo niliyaruka, huu sasa ni muendelezo wa matukio ya Mwaka huu kuanzia mwezi wa 3
So nikamkatalia lakini sikumkatalia kuonesha ya kwamba nimeridhika na maisha (hapana) nilimtolea sababu za uongo na kweli za kifamilia lakini hakunielewa, akaniambia niende nikampumzike halafu siku inayofuata tuongee vizuri
Nilivyofika nyumbani nikakuta mazingira kama vile kuna mtu alikuwa anaishi, maana nilikuta kusafi kila kitu kipo mahala pake, kumbe ni Caryn ndio alikuja kufanya usafi na kuondoka
Kesho yake nikaenda kwa Mzee majira ya jioni, nilimkuta Mzee anapiga story na mlinzi wake wa getini, nilijua wanapiga story kwasababu mlinzi alivyonifungulia Geti alirudi pale alipokaa Mzee ndio nikajua kama kulikuwa kuna mazungumzo yanaendelea, baada ya muda kidogo mlinzi akatuacha na Mzee
Mzee: "Unakokaa na huku kwangu ni mbali eeh?
BM: "Kiasi sio sana"
Mzee: "Nikipata nafasi wiki ijayo nitakuja kutembea"
BM: "Karibu sana"
Mzee: "Ukiondoka unikumbushe nikupatie funguo ya Gari uende nayo Caryn atairudisha"
Wakati naingia pale Parking nilikuta Gari mbili tu, Lexus ambayo tumetoka nayo Mwanza na Jeep Wrangler pamoja na Gari ya Bi Mkubwa Volkswagen Touareg, (I mean nilikuta Gari 3)
Sasa Mzee alivyosema atanipa gari moja ili nisipate shida ya usafiri kichwani kwangu nikawa napiga mahesabu, kwamba ni gari gani kati ya zile 2 Mzee atanipa maana najua Ile ya Bi Mkubwa sio ya kushea japo haipo kwenye matamanio yangu
Nimesema sio ya kushea kwasababu kuna siku Caryn alitaka kuchukua gari ya Mama yake Mzee akamuambia, "Chukua gari yeyote hata yangu, lakini sio ya Mama yako"
Muda ule Wakati naendelea na maongezi na Mzee, Caryn akanicheki alitaka kujua naondoka muda gani
Sasa kuhusu safari ya China nikamuelekeza Mzee mwisho wa siku akanielewa ila akanipa kazi
Mzee: "Nimekuelewa, ila kwasababu hii nafasi nilikuwa nishakujaza wewe, itabidi unitafutie kijana smart atakaeenda kuifanya hii kazi badala yako"
Nikamuitikia na kumuahidi kufanya hivyo japo kwangu nimeona ni kama mzigo wa lawama lakini sina budi kulifanikisha hili kwasababu kwangu nimeshamuangusha tayari kwa mm kukataa kwenda, Jamaa aliyekuwepo kule China kwa sasa ana handover office mwezi wa sita, So Mzee akanipa mwezi mmoja tu wa kukamilisha kazi yake, kama nikifanya chini ya hapo itakuwa better zaidi
Tukamaliza mazungumzo, Mzee akanipa funguo ya Gari, otea ni gari gani? ni Jeep buana[emoji1544] akanipa na 200k ya ku refill mafuta maana mshale ulikuwa unaelekea chini
Nikateleza na Jeep hadi mjengoni, nilidhani nitamkuta Caryn kashafika ila haikuwa hivyo, usiku ule ule nikaanza kufikiria ni mtu gani sahihi wa kumpatia Mzee, Kila Niki review phone contact sioni, washkaji ninao lakini nina mashaka nao, kama yule wa kinondoni ndio wa kwanza kumfikiria lakini siwezi kum connect kwenye hii issue
Aysee acha niwaambieni kitu, msiwalalamikie marafiki zenu walipo vitengo kwamba hawawapi michongo, kabla ya kulalamika jitasmini kwanza wewe mwenyewe upo Connectable? Anyways Wakati naendelea kuwaza nini Cha kufanya huku nikipitia majina ya namba za simu nilizozisave, meseji kutoka kwa Caryn ikaingia kwenye simu yangu "Hey, umekuja na Mzee" sikumjibu kwa message nikamvutia waya
BM: [emoji338]"Vipi ww uko wapi kwani?"
Caryn: "Nipo getini hapa naona gari ya Mzee, ndio upo nae?"
BM: "Hapana, Gari nimekuja nayo mimi"[emoji3513]
Baada ya kumwambia nipo pekee angu ndio nikasikia Geti kubwa linafunguliwa, Caryn alivyofika nikaacha kuwaza vitu nilivyokuwa naviwaza
Caryn: "Kijana siku hizi unatembelea Jeep, ungekuja na new toy"
BM: "New Toy?"
Caryn: "Si Lexus Ile, Believe me Ile Gari sijaindesha hadi hivi tunavyoongea"
BM: "Hujaamua tu, ukitaka hata kesho unaweza kulichukua"
Caryn: "Dad siku hizi amechange, kabla muende Mwanza nilimuomba Ile gari akanibania"
BM: "Sasa kama amekubania wewe, Mimi ni nani hadi anikubalie kunipa gari yake pendwa kwa Sasa"
Caryn: "Tuachane na hayo, kwenye simu umeniambia amekupa kazi, ni kazi gani?"
BM: "Baada ya kufanya kama vile ulivyoniambia Mzee hajapinga ila kanipa jukumu la kumtafutia kijana wa kwenda kuifanya hiyo kazi"
Caryn: "Sasa hapo kuna ugumu gani?"
BM: "We unadhani ni simple kumpata mtu aina ya Mzee anayemtaka?"
Caryn: "Kwani huna marafiki?"
BM: "Naogopa kumconnect rafiki zangu na Mzee, coz nawajua vizuri"
Caryn: "So unamaanisha wewe na rafiki zako hamfanani kitabia! how? I mean how do you guys become friends kama hamfanani tabia & what kind of friends do you have?"
BM: "Too much Questions Caryn....nimetoka Mwanza na Baba yako, wale. marafiki zake niliowaona hakuna hata mmoja anaeendana na Mzee kitabia"
Caryn: "Nadhani utakuwa hujui utofauti wa friends na Business Partners, wale ni Business Partners"
BM: "Sasa mkishakuwa Business Partners si mshakuwa marafiki tayari"
Caryn: "Mnaweza mkawa marafiki na mkawa Business Partners, lakini si kila Business Partners ni marafiki"
BM: "Na si kila marafiki ni Business Partners"
Caryn: "Dah! siamini kama ni BM anaongea hivi...By the way Dad alishawahi kuniambia Watu wengi tunawadhania wana akili kwasababu wamefunga vinywa vyao, ukitaka kujua akili ya mtu ni wakati anaongea"
BM: "That's the most sarcastic insult of the year....."
Caryn: "Okay, what I meant ni kwamba ni rahisi kwa marafiki kuwa Business Partners lakini ni ngumu kwa Business Partners kuwa marafiki"
Nikaona nikiendeleza majadiliano tutavurugana, nikaenda zangu room kulala.
Zilipita siku kadhaa, mwezi march (mwezi wa 3) kuelekea tarehe za mwishoni kazi yangu ya kumtafuta mtu wa kwenda kufanya kazi china ikawa imekamilika,
Nilipokuwa nakaa zamani nilifahamiana na bro flani hivi, tulikuwa majirani wa karibu tukazoeana sana kiasi Cha kuwa washkaji, jamaa ni mtu safi wala hana mambo mengi, ila tangu nilivyoondoka kule nilipokuwa nakaa ushkaji Mimi na yeye ukapungua so Wakati naangaika kumtafutia Mzee kijana, mshkaji hata hakuwa katika mawazo yangu, kuna siku tu alinipigia simu Ile design ya kunipa 'Hi' tulivyomaliza kuongea ndio nikaanza kum-consider
Nikaenda kumu-approach jamaa akakubali ila kwa bahati mbaya jamaa hakuwa na Passport, nikamkutanisha na Mzee, Mzee nae akajiridhisha, jamaa akaambiwa atafute Passport halafu maswala mengine amuachie Mzee
Kuna watu wako serious na maisha nyie, Jamaa alipata Passport ndani ya siku mbili, Wakati ya kwangu niliisotea mwezi mzima, jamaa alivyoniambia kwamba kashaipata Passport sikuamini nikamuambia hadi niione, akaipiga picha akanitumia WhatsApp nilivyoiona nikamvutia Mzee waya kumjulisha
Kumbe kitendo Cha Mzee kumuambia jamaa atafute Passport ulikuwa ni mtihani kwa jamaa, kwasababu Mzee anadai yeye angeweza kum connect na watu na ndani ya masaa 24 mshkaji angepata passport, hivyo alitaka kupima 'Nia' ya jamaa na ushapu wake.
Nilivyomaliza kuongea na Mzee ilibidi nimrudie Jamaa, (huyu jamaa tumpe jina gani? mbatizeni jina lolote maana nishachoka kutunga majina) Nikamuambia ni jinsi gani alivyoukwepa mtego maana Mzee aliniambia kama ingepita wiki jamaa angekuwa hajapata passport basi angekuwa unqualified
Jamaa nae akaanza kunipa behind the scenes Hadi alivyopata passport, mchizi wakati anaambiwa atafute Passport pesa aliyokuwa nayo kwa Wakati ule ni elfu 69 tu, alichokifanya akaenda kuweka Bondi Tv, Television aliyonunua Milioni moja na laki 2, kaenda kukiweka Bondi kwa laki 3, nilisikitika sana alivyonipa hiyo taarifa, maana hiyo laki 3 mm ningempa tu halafu mbele ya safari tungejua tunamalizanaje, ila jamaa anakuambia kwa mchongo niliompa hakutaka kunikopa hata buku
Zilipita kama siku 2 hivi nikakutana na Mzee mjini, tukatafuta sehemu tulivu tukakaa, mwezi wa tatu tarehe za mwishoni (Date 20+)
Tukazungumza tuliyozungumza mwisho wa siku Mzee akaniambia
Mzee: "Mtu uliyeniletea sina mashaka nae hata kidogo, lakini itabidi Caryn ampitishe maana yeye ndiye atakaye fanya nae kazi, na si unamjua yule Binti alivyo, tunaweza kupoteza muda kumsafirisha mtu halafu akakataa kufanya nae kazi"
BM: "Okay, kwahiyo sasa tunafanyaje?"
Mzee: "Itabidi huyu rafiki yako aanze kuja pale ofisini ku volunteer ili aweze kuzoeana na Caryn, halafu Mimi nitasikiliza majibu ya Caryn atakayonipa"
BM: "Na kama Caryn akimkataa?"
Mzee: "Akimkataa mtu tuliyemtafuta sisi atatafuta yeye mtu mwingine, sababu unajua maamuzi ninayoyafanya kuhusu Kampuni ni lazima yeye ayapitishe hata kwa Mitchell ni hivyo hivyo, wao kwasasa ndio wanaongoza Kampuni Kuna vitu wanajua ambavyo mimi sivijui"
Changamoto ndio inaanzia hapa, Mwamba anatakiwa auface ukuta wa Berlin (Càryn) Jamaa yupo smart lakini kutokana na aina ya mtu anayeenda ku-Deal naye naweza kusema ni 50/50, Yani kufaulu inawezekana na kufeli inawezekana vile vile, najaribu kuvuta picha mtu aliweka Tv yake bondi yenye thamani ya Milioni moja plus kwaajili ya mchongo halafu aje aambiwe mchongo hakuna, (I can feel the pain)
Pia katika maongezi Mzee akaniambia kuwa kwa vile ahadi za kuja kupaona kwangu zimekuwa nyingi bila mafanikio akaniahidi na kunihakikishia atakuja siku ya Pasaka kula sikukuu kwasababu siku hiyo Bi Mkubwa Yani mke wake atakuwa yupo mkoani
Hivyo Ukiachana na Annie, Mzee pia ameingia kwenye list yangu ya wageni nitakao wapokea siku ya Pasaka japokuwa Annie alisema atakuja before Pasaka
Itaendelea
[emoji837]Episode ijayo itamaliza matukio yote, Mzee uso kwa uso na Annie? na Mzee akifika kwangu ndio amefika kwa Mwanae Caryn kwasababu anajua ni sisi ni majirani (Neighbors)
[emoji837]Pia itajulikana kama jamaa anayetakiwa kwenda China alifaulu mbele ya Caryn au ndio hivyo tena, (Huyu jamaa tumpe jina gani asee?)
[emoji837]Episode ijayo pia ndio itatufikisha kwenye ANOTHER DAY TO REMEMBER itajulikana ni nini kiltokea siku hiyo hadi nikaandika hayo maneno Another day to remember
All in All hii ndio Episode pekee niliyoiandika katika kipindi kigumu, Episode zote zilizopita nimeziandika huku Niki enjoy lakini hii nimeandika utadhani nimelazimishwa hii yote ni kwaajili ya Promise ya Mei mosi
Cheers guys till next time