Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Annie hawezi kunisahau yule, Atakayemuoa atapata shida sana
Akija fahamu umemwacha kwa sababu hizo, amini kaka Hatoyama kukusikia na usije Shanghai hata kama kwa bahati mbaya alipata mimba yako, akaichomoa kabisa au mtoto akizaliwa amwambie baba yako alishafariki siku nyingi sana,
Yaani usinidanganye kwa hilo kaka, maana kila mtu anahitaji kuheshimiwa hisia zake, ila hapo kwa Annie mkuu umezingua pakubwa sana, ni kama ulishamchoka muda sana ila unaogopa kumwambia nimekuchoka, kwa yale ambayo amekutendea, ila kama umeamua kumkatili mkatili sasa kuliko kuendelea kucheza na hisia na muda wake, mkuu,
 
Hapa umemaliza kila kitu...mwenye masikio na asikie....
 
Mie navyojua Mapenzi huchaguliwi huamuliwi na mtu unaamua mwenyewe kutokana na vigezo vyako na moyo wako unasemaje,wengi wamemchagua huyo Caryn sababu ya Ukwasi wa pesa za Baba yake😁muda utaongea.
 
Ebu tusubiri kwanza Annie mwenyewe afike Dar, mambo mengine mbona yanazungumzika tu
kaka hadi hapa tulipofikia iko wazi kabisa moyo wako umemdondokea carrien,nimemuonea tu huruma Annie kwa muda wake aliopoteza kwako
 
Nimeishia hapa
Kuna nyingine??



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hizi kura zitakupoteza
Hapo mwanamke wa kuwa naye ni Annie.


Mtu aliyekufaa katika dhiki,, unconditional love ipo hapo.


Huyu Muhasibu ukiwa naye atatumia Kampuni km fimbo ya kukutishia.


carren hapana kwa kweli,
Yupo kimaslahi.

Usiache mbachao kwa msala upitao.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madam Shunie naona nafsi yako haijakubali kabisa, ila ndio hivyo tutafanyaje tena
Toka mwanzo BM ulionekana tu upande ambao upo naomba tu usimuumize Annie na hata kama mtaachana iwe sababu ya kweli isiwe tu sababu ya mapenzi yako yapo kwa Carryn
 
BM X6 yaani habari za Annie umetulambisha mwiko tu, then story za Caryn umetujazia upawa halafu kwenye kura unawaweka kwenye uzani mmoja!

Ama kweli Annie ameanza kutafutiwa sababu. Ngoja tusubiri.
 
Sikujua Kama wazo la kupiga kura umelifanyia kazi, since then ndo naufungua huu uzi leo, thank you mr.

But sijaelewa kwann wakulungwa wamemuona Caryn na sio Annie, kwasababu ya pesa au huo ukaribu mlio nao sasa. okey pamoja na yote bado nakutakia mema ndugu yangu, kila la kheri
 
BM X6 yaani habari za Annie umetulambisha mwiko tu, then story za Caryn umetujazia upawa halafu kwenye kura unawaweka kwenye uzani mmoja!

Ama kweli Annie ameanza kutafutiwa sababu. Ngoja tusubiri.
Uko sahihi mkuu.. story yote imejaa content ya caryn (ambaye ni co-starring) afu at final anakuja pambanisha na special Appearance (Annie)....

Kwa akili ya kawaida tu BM X6 tayari kichwani analo chaguo lake (ambay ni caryn 99%), izi hapa ni mbwembwe tuu
 
Hapana umeninukuu vibaya boss wangu me sijapenda tu tabia yako ya kuwapambanisha hao wadada wote hawana hatia ni kama unataka kuchezea hisia zao tu
Hii tabia ya kuwaweka watu wawili mezani haiko poa.
Mimi nikimpenda mtu ninanyooka sihitaji ushauri wa mtu
 
Hatma ya maisha ya mtu haiwezi kuamuliwa na mtu mwingine kamwe. Suala la kijana wa Buguruni au kuwapambanisha Annie & Caryn kwa kura za mchongo ni madoido ya kunogesha stori .. Najua unajua hilo.
 
Ni kweli Mkuu lakini Annie hata kama nikimuacha, nitahakikisha anabaki kuwa kama Rafiki kwangu, siunajua Love can be really without being forever

Ila bado nazichanga karata akifika ndio nitajua zaidi
Hili jambo lifute kabisa, huyo cary anakupenda kimaslahi she is using you to her goals, yale maneno ya mzee alikuwa sahihi unaweza kupoteza hapo katika upande mmoja au moja kwa moja... Sasa nikushauri baki na Annie mkuu baadae usijute bahati za kupendwa uja mara moja tu.. utakuja kujuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…