Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Saivi kasema iko Mikononi mwake, yule dogo wa Buguruni alisingiziwa tu.Hatima ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni.
Kamanda tupe muda kamili lini utaanza na saa ngapiSo niendelee humu humu sio
Sawa mkuu, vyovyote iwavyo maisha lazima yaendelee. Hongera kwa mapambano.Nilitaka kuanzisha Uzi mwingine ambao nilitaka kuupa jina la "FROM HERO TO ZERO, Hatma ya maisha yangu ilikuwa mikononi mwangu HUMBLE BEGINNINGS"
Muendelezo wa visa vya hii story SEASON 1 & 2 nimeona heading itakinzana na visa vya SEASON 3 ndio maana nilitaka kuja na Uzi mwingine wenye title nyingine lakini ni muendelezo wa story hii hii tulioanza nayo mwanzo.
Ukizingatia pia yule kijana ambaye ndiye aliyebeba jina la Uzi alifariki mwaka jana nadhani nilikuja kuleta update humu kwenye huu Uzi, Mungu amlaze mahala anapostahili🙏🏾
Kwa uchache tu, wahusika ni wale wale ila kuna walioongezeka. SEASON 3 mapenzi kama kawaida yapo ila Kwa sehemu kubwa ni harakati za kimaisha, humu ndani Kuna sarakasi nyingi za kuhuzunika na kutia huruma "FROM HERO TO ZERO", Mimi kama BM maisha yalinichezesha hapa katikati, kutoka kuingiza milioni 2 to 3 Kwa wiki hadi 90,000 Kwa wiki (elfu tisini sio poa)
Niliachana na harakati za Bandarini nikahamia kwenye mishe zingine kabisa (HUMBLE BEGINNINGS) Ila haya Maisha haya nyie acheni tu, usipozichanga karata vizuri kurudi mavumbini ni kugusa tu, halafu pia haya mapenzi yanalostisha sana
Kuna sehemu nilikosea kufanya maamuzi ambapo ndipo anguko langu lilipotokea mbaya zaidi niliyesimama nae hakusimama na mimi, Si mnakumbuka zile kura nilizowapigisha humu? Candidates wakiwa ni Caryn na Annie picha ndio linaanzia hapa, waliosema LOVE IS NOT ENOUGH hawakukosea hata kidogo.
Kuna baadhi ya mambo ukitaka kuwa sahihi katika kuyafanyia maamuzi ni lazima uwe selfish kidogo lasivyo mbeleni kuna majuto makubwa sana na hapo ndio nilipokuja kugundua ya kwamba "Hatma ya maisha yangu ilikuwa mikononi mwangu" na sio kwa kijana wa Buguruni
All in All Maisha yaliendelea na bado yanaendelea, SEASON 3 Episode 1+ soon humu humu kama baadhi ya wadau waliopendekeza kwamba nisianzishe Uzi mwingine
Naomba unitag kwenye uzi utakapoihamishia hii storyAase humu ndani mpo?
Leo nimeamka siku nzima nilikuwa naiwaza hii story, nadhani ni muda sahihi Sasa wa kuleta muendelezo wake, lakini sitoileta kupitia Uzi huu nitafungua Uzi mwingine.
Poa Mwamba maisha yana challenge nyingi sana Hongera kwa kutoa muda wako kutupatia hamasa vijana wenzako.Aase humu ndani mpo?
Leo nimeamka siku nzima nilikuwa naiwaza hii story, nadhani ni muda sahihi Sasa wa kuleta muendelezo wake, lakini sitoileta kupitia Uzi huu nitafungua Uzi mwingine.
Siwezi kuweka ahadi ya muda ila niseme tu nimeanza kuiandika Leo, so muda wowote kuanzia wiki ijayo inaweza kushuka, kwasababu issues sio kuiandika tu, inabidi pia nitulie niweze kukumbuka matukio ambayo ni muhimuKamanda tupe muda kamili lini utaanza na saa ngapi
Shukrani mkuu, tuko pamoja...nahisi tutakutana tu humu humu, kama kutakuwa na mabadiliko tutajulishanaSawa mkuu, vyovyote iwavyo maisha lazima yaendelee. Hongera kwa mapambano.
Kwa niaba yangu, na kwa niaba ya wengine nipende kukujulisha kuwa tupo tayari kwa muendelezo. Iwe ni humu, ama pengine utakapoona yafaa kuanzisha uzi.