Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Hiki ndicho nikionacho mimi.

Kajitahidi, ila bado hajaweza kufanya ikawa halisi, kwa Mtanzania akisoma tu anajua hii ni ya kutunga, ila ana kipaji kikubwa.
 
Dah, mi nikajua mtihani wenyewe ni Mzee anataka umuoe Caryn kumbe biashara???

Sasa mkuu, tuliza akili uuelewe vzr mtihani,...Lengo sio huyo kijana, lengo ni wewe haswaaa...

Ni rahisi mtu kusema anaanzisha biashara kutumia pesa isiyo yake ila ni ngumu pale hyo pesa inapokuwa yake, inahitaji Nia madhubuti kufanya hvo...Unachotakiwa Kwa maana nyingine ni kuprove you can't handle your own investments before people's investments.


Somo la pili, biashara huwez kuzisimamia mtu 1, so you need to have and groom your own team, proof ya pili anataka ni kuprove unaweza kumwezesha kijana nae akasimamia biashara na kujisimamia yeye na familia yake.

Haya yote ukifanikiwa hata kama hutopata mia toka upande wowote bado unaweza kujipanga na ukafika mbali...mtihani ni kwako uliposema unataka ufanye biashara bila shaka ulijipanga Kwa haya maana kama ndivyo basi Haina kufeli, ila kama ndo yalikuwa maneno hapo unalo...

And kukosea ila muhimu usikate tamaa...

NB: Namba za Caryn muhim mkuu, ndo taste yangu kabisaa
 
Hiki ndicho nikionacho mimi.

Kajitahidi, ila bado hajaweza kufanya ikawa halisi, kwa Mtanzania akisoma tu anajua hii ni ya kutunga, ila ana kipaji kikubwa.
Story telling na uandishi nampa A bila wasiwasi. Anaenda kuziba pengo la bold. Ila asije mbeleni akatwambia tuende sijui whatsapp au telegram tulipie..

Aendelee kutupa utamu hapahapa..
 
Story telling na uandishi nampa A bila wasiwasi. Anaenda kuziba pengo la bold. Ila asije mbeleni akatwambia tuende sijui whatsapp au telegram tulipie..

Aendelee kutupa utamu hapahapa..
Mkuu kwanini hutaki "kulipia" vitu vizuri ?
Hujui kwamba uandishi ni talanta ambayo inapaswa kumlipa yule aliyejaaliwa nayo...

Kama una kipaji, kwanini ufe na njaa
 
Caryn ana dharau sana sijaona sababu ya yeye kumdhihaki dada yake vile tena mbele za watu wasiowafahamu anamshusha na mzee pia hajamtendea haki michelle eti kisa kapenda kijana wanayemuona sio hadhi yao.

Mwisho wa siku wanakuandaa kuifahamu biashara uje umuoe caryn ambayae hatakuheshimu kamwe. Sijaona akili zake zaidi ya kebehi tupu.

Mwisho ukimuweka annie mbele utapoteza kazi maana mshadanganya kwa mama accountant pia utampoteza mzee maana anakuandaa kuwa kijakazi wake kupitia caryn
 
Ushauri:

1. Mapenzi
Wote wamekusaidia kwenye nyakati ngumu ila Annie unamuonea huruma zaidi, Accountant ana madhaifu ya kibinadamu ya kuropoka hii inatokana na familia na malezi, ila sioni sababu kubwa ya yeye kukosa point…..sometime inabidi udanganye ili mambo yaende sawa, Accountant anajua moyo wako uko wapi.

Anyway go for Annie naona ndio mnaelewana vile unataka.

Mfanye Annie ajue walau ndoto yako ya kutaka kiwa mfanyabiashara na fanya ajue uko na unalenga kuutengeneza mtaji kutoka kwenye hiyo kampuni, ila usikubali nafasi kwa masharti ya kuoa mtu usiyempenda.

2. Mzee na familia
Kuna muda unashuka sana mpaka inakuwa noma, hasa kwenye conversation na hako katoto, mpaka hapo nadhani huo mtihani wa mzee na huyo mtoto wa buguruni itakuwa umeshinda ila hako katoto Karen ki design ni type wale hawakupi ushindi kirahis rahisi.

Kukuza biashara ndani ya miezi sita kwa mtu ambaye hajawahi na imletee pesa zaidi ya 100,000 kwa mwezi plus majukum ya wadogo zake.Tengeneza link zaid na mzee huyo dogo anaweza kuja kuwa kirusi
 
Story telling na uandishi nampa A bila wasiwasi. Anaenda kuziba pengo la bold. Ila asije mbeleni akatwambia tuende sijui whatsapp au telegram tulipie..

Aendelee kutupa utamu hapahapa..
Akitaka watu walipie huko sawa tu, sababu anakaa chini, anapoteza muda, anaumiza kichwa plus bando.

Watakaoenda kulipia sintawacheka, wako sahihi kulipia kitu kizuri, japo mimi siwezi kulipia.
 
" Hahaaaa imeisha hiyo " in kidagaa voice
 
Ni true story mkuu, labda Mashaka yako yapo sehemu gani ya story?
Sioni mtihani mgumu kwa mzee, hapo anachotaka ni uaminifu na kama wengi wanavyofikiri kuwa unaandaliwa kumuoa Caryn but sioni hilo kwani ulishawahi kumwambia mzee kuwa una mtu wako, endapo utapiga u turn eti ujihusishe na binti yake, yatakukuta ya Michelle kuwa uko after money.

Endapo utaonyesha msimamo kubaki na Annie mzee atakuheshimu sana.

Kuhusu accountant;

Ukijichanganya umekwisha, hapo unaolewa mtu wangu.
Kupanga ni kuchagua, katika maisha usiingie kwenye mahusiano kwa kwasababu za kiuchumi utajuta.
 
Ni true story mkuu, labda Mashaka yako yapo sehemu gani ya story?
Usitarajie kuaminika na kila mtu.
Pili mtihani mdogo sana, zaidi unapaswa kuwa na msimamo.
Tatu...asikutoe mtu kwenye msimamo wa mapenzi.
Mke ni Annie
Annie
Annie
Ukikosea unachokitafuta hutakipata kamwe.
Note; japo stori ya kutunga lakini ina somo.
Kwanini ninasema ni ya kutunga?
Tittle/heading ya kijana wa Buguruni uliiweka mwanzo wa uzi lkn mtihani wenyewe umeweka juzi tu na Caryn alipomshauri babake awasaidie hao vijana.

Lakini wewe ulishamtaja kijana kwenye tittle/heading ya uzi
 
Nitaisoma baadae
 
Sawa mkuu, ndio nimeianza kusoma maoni yako, acha nisome na maoni ya wengine nione wanasemaje katika hili, Muda upo wa kutosha sina sehemu ya kwenda
 
Asante Mkuu kwa ushauri wako mzuri sana, kuhusu Biashara ya kuingiza laki 5 kwa mwezi ndio najiuliza ni nibiashara gani hiyo? Japokuwa wengine wameshauri Biashara ya mtumba...

Na hapo kwenye nyumba unakumbuka kauli ya Caryn "Don't cheat I know my Dady" hapo amemaanisha nikileta janja janja yoyote Mzee atajua kivyovyote vile hata ya kumfahamisha

Ila Caryn kuwa Mvumilivu kidogo nimzoee ili hata nikikupa namba yake nikupe na miongozo lasivyo utakula za mbavu namjua yule mtoto ana confidence imepitiliza....Mimi sijawahi kuchanwa na mtoto wa kike lakini Caryn Kawa wa kwanza, Ile siku nilivyotoka pale hotelini nilienda kuiandika kwenye Diary ibaki kama kumbukumbu
 
Story ina mafundisho ila imenifikirisha sana baadhi ya mambo, mfano unawezaje kukumbuka kila neno katika sentensi wakati wa mazungumzo yenu na mzee, caryn, annie, accountant, mama?

Inanifanya nihoji uhalisia (ukweli) wake.
Mengine nimeyasahau mkuu, hayo niliyoyaandika sio yote mkuu, Halafu haya matukio hayana muda mrefu, ni juzi juzi tu hapa
 
Labda Caryn ndio mjanja lakini hao wengine hamna kitu, na Caryn mwenyewe nakumbuka nilimuuliza kama anatumia Facebook Instagram na mitandao mingine nakumbuka alininijibu "I'm too old for that juvenile staff"

Halafu kwani Teenager ni kuanzia miaka mingapi hadi mingapi mkuu?
 
Hapo kwa Caryn kujenga hoja kama mtu mzima mi pia ilinifikirisha sana.

Anyway anajua kutunga na tumepata mawili matatu kama mafundisho katika maisha. Ngoja tuone huko mbeleni muendelezo wake utavyokua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…