Kushushia mzigo Airport ya Dar ni Gharama kubwa sana, na Ukiachana na Gharama kwa upande wa Zanzibar kukagulia haichukui muda sana kama Dar, Mzigo ukishukia Dar unaweza kuchukua hata siku 2, ukaguzi wao wana complicatisha sana, Yani kitu kimoja kimoja wanakinyambua ili kupiga Ushuru vizuri na wakikuambia Ushuru ni milioni 15 basi Jua ni milioni 15 net, hakuna ku bargain. Lakini Zanzibar unaweza ku bargain,
Lakini kumbuka ukishushia Mzigo Zanzibar basi jua uta deal na TRA mara 2, Yani Zanzibar mzigo ukishuka kwenye Ndege na Dar Mzigo ukifika Bandarini, lakini pamoja na mzunguko wote huo Bado ni cheap mzigo kushukia Airport ya Zanzibar kuliko ya JKIA, kwanza Zanzibar ni mara chache sana kukagua mizigo yote ndio maana inakuwa cheap kupitisha mizigo kule na haichukui time mingi