42774277
JF-Expert Member
- Aug 24, 2018
- 6,833
- 8,853
Hebu share experience yako na Kampuni yao.Mkuu naona tangu niwaungishe kampuni na wewe mmenitambua kiaina...asante sana
Labda nitakuwa mteja wao baada ya Chinese new year.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hebu share experience yako na Kampuni yao.Mkuu naona tangu niwaungishe kampuni na wewe mmenitambua kiaina...asante sana
Aisee tunawapate ofisi zao wapi Hapa mjini maana tunataka tupate huduma zaoKwa ujumla wanajua sana kuwa attend wateja wao.
Huyu BM X6 ni bonge la mtu linalojali sana kazi yake na wateja.
Usisite kuwaungisha na hutojuta mkuu
Shukran sana [emoji120] tusamehe tunapokufokea unapochelewa ni utamu wenyewe unasababisha
Unajua nawaza kutaja Jina la Kampuni hapa pamoja na Address yake lakini nasita kwasababu story bado inaendelea, Yani hivi ninavyoandika hii comment Bado Kuna matukio yanaendeleaAisee tunawapate ofisi zao wapi Hapa mjini maana tunataka tupate huduma zao
Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Muone mkuu BM X6 hana noma mbona?Aisee tunawapate ofisi zao wapi Hapa mjini maana tunataka tupate huduma zao
Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Nitamuona ngoja Wakati ufike Kwa upande wangu ni kweli Hana noma BMX6Muone mkuu BM X6 hana noma mbona?
Umakini unahitajika hapo, asije taka kula tunda kimasihara mwisho wa siku akajikuta anaachishwa kazi kimasiharaTunda kimasihara Loading....
Mkuu malizia story kwanza usi disclose hizo info nadhani sio muda muafakaUnajua nawaza kutaja Jina la Kampuni hapa pamoja na Address yake lakini nasita kwasababu story bado inaendelea, Yani hivi ninavyoandika hii comment Bado Kuna matukio yanaendelea
Kama hii last Episode ni matukio ya mwezi wa kumi Mwaka jana (October 2022)
Antonniailipoishia
Sasa nimefika ofisini naingia room ambako kunafanyika meeting nimekuta staff wote akiwemo Accountant, Mama Accnt pamoja na Caryn
Accountant: "Ivi tukiongea tu ukweli mtu anawezaje kuchelewa siku kama leo? Uzembe mwingine umepitiliza"
Caryn: "Binti kaa kimya kuna Mahali nilimuambia apitie ndio maana amechelewa Mama unaweza kufungua kikao"
Tukaangaliana na Caryn, Accountant nae akanipiga jicho la wizi, nikaa kwenye kiti ila ukweli ni kwamba hakuna Mahali Caryn ameniagiza nimechelewa tu kwa uzembe wangu kama Accountant alivyosema
Muendelezo
SEASON 2 Episode 9
Mama Accnt: "Naomba tusikilizane kwa makini, nitaharakisha kidogo kwasababu muda sio rafiki....najua wengi wenu kama sio wote mnajua kikao kinahusu nini, kwa kifupi leo ndio Ile siku ya kuagana na ninyi rasmi, lakini sio kuwaaga tu na kuwatambulisha kiongozi wenu mpya mtakaye kuwa naye"
"Si mnajua safari lazima iendelee hata kama Dereva kachoka atatafutwa dereve mpya ambaye bado yupo fresh kuanzia kimwili hadi kiakili, Mama yenu mm nimeshachoka nahitaji kupumzika sasa, niseme tu kwamba nashukuru kwa ushirikiano wenu mzuri mliouonyesha kwangu"
"naomba pia ushirikiano huo huo mliouonyesha kwangu muoneshe pia kwa kiongozi wenu mpya, kama tulikwazana naomba tusameheane ni mambo ya kibinadamu hatujakamilika"
"Nitakaye waacha nae ni huyu Binti hapa pembeni yangu anaitwa (Caryn) Nadhani mlikuwa mkimuona akija hapa ofisini siku za hivi karibuni (kumbuka hapa hataji jina Caryn ila anataja Jina halisi la Caryn)
"Unajua Kampuni yeyote au hata nchi inapofanya mabadiliko ya kiuongozi lazima kuna tofauti na changamoto mpya zitajitokeza, mimi ni Mzee bahati nzuri wote hapa hakuna aliyenipita umri"
"Pengine hii ilikuwa advantage kwangu kwasababu inawezekana wengine mlikuwa mnaniheshi kama Mama yenu mzazi na sio kama Boss wenu, na mnajua Mama siku zote ana huruma kwa wanae, Wengi wenu hapa sijawafukuza kazi kwasababu nilivaa U-Mama wangu na kuweka U-Boss pembeni na maisha yakaendelea"
"Sasa huyu ninaye waacha nae ni kijana hata 30 hajafika na wala hana mtoto, hivyo nina uhakika yeye atatumia U-Boss kwasababu namjua pia ni mtu wa aina gani, na sio mbaya kutumia u-Boss kwasababu hapo ndipo Discipline inapopatikana, lakini sio kila mahali unatumia U-Boss, unanisikia Caryn"
"Na najua humu kuna wengine ni wakubwa kiumri kumshinda Boss wenu mpya, hiyo sio sababu ya kutomuheshimu kwasababu yeye ndie last say kwasasa akikufukuza kazi hakuna wa kupangua maamuzi yake"
"Naomba niongeee na wachelewaji pia, sitaki kuondoka hapa baada ya wiki nisikie flani amefukuzwa kazi na hata nikijua muda huo nitakuwa sina mamlaka ya kukurudisha kazini, nasisitiza hapa kwasababu najua kuna watu wanaweza kuharibu wakidhani mm naweza kuwasaidia"
"Kuna watu ni maarufu humu kwa kuchelewa kazini niwaambie tu kwamba kuanzia sasa kuchelewa kazini kunaweza kukufukuzisha kazi shauri yenu"
"Pia nadhani kuna mabadiliko yatafanyika kwa watu wanaoenda Zanzibar na watu wanaokaa store, Caryn mwenyewe ndio atajua jinsi atakavyo wapanga"
Kwa kufupisha tu maneno ni kwamba Mama Accnt aliongea sana siwezi kuandika maneno yote hapa sababu mengine pia nimeyasahau,
Mwisho wa siku Bi Mkubwa alimaliza kikao akatumbia Mimi, Secretary pamoja na Accountant turudi after break time tukatoka tukamuacha Mama Accnt na Caryn ofisini kwasababu kikao chenyewe kilikuwa kinafanyika ofisini kwake
Basi wa kwenda kunywa chai walienda, Sasa wakati nipo nje napiga chai Accountant nae akatokea alivyoniona nae akaja pale pale kwenye meza niliyokaa
Accountant: "Naona umerudi na nguvu mpya, una watu wa kukukingia kifua kabisa, ila BM nikuambie tu kwamba kama niliweza kummudu Mama ambaye ndiye mwenye Kampuni basi jua tu hicho kihawala chako hakinitishi, tutaona Mimi na yeye nani ni zaidi"
Kwani nilijibu basi nikanywa zangu chai nikasepa yeye hakunywea pale waliwaomba wale wahudumu wampandishie juu ofisini, Sasa na mm nikawa nimebaki katikati nikijiuliza 'kwani hii Kampuni ni ya nani haswa?' mbona kila mtu anavimba?
Ilivyofika majira ya 11:00hrs nikapanda juu kwaajili ya kikao cha pili, imefika saa tano kama Dakika tisa kikao kikaanza, nipo Mimi, Secretary, Accountant, Caryn pamoja na Bi Mkubwa, wote Wanawake wakiume nilikuwa mimi tu
Hiki kikao Cha pili kilikuwa hakina mambo mengi sana, Bi Mkubwa alituasa tufanye kazi kwa bidii na kwa kujituma, Pia akawaonya Secretary na Accountant kufanya kazi kwa mazoea
Mama Accnt: "Kitu kingine muhimu Caryn ambacho nilisahau kukuambia ni kuhusu TRA, ikitokea mzigo umekamatwa inabidi ujue namna ya kuongea na hawa watu (TRA), Uzuri BM yupo so atakusaidia zikitokea changamoto za namna hiyo kwasababu yeye anajuana na hao watu, kikubwa ni usikivu na kuwa mpole siku zote mazungumzo yanamaliza kila kitu sio kila mahali ni pa kutumia Pesa au unaweza kutumia pesa"
Labda nifafanue kidogo hapo kwenye kipengele Cha TRA, ipo hivi....napokea mzigo Airport ya Zanzibar nita clear, yani nitafanya clearance na kila kitu kinachotakiwa mzigo utavuka Maji Hadi Bandari ya Dar nitakutana na TRA
Pia napo nita clear kila Kitu pamoja na Kodi za Bandari na mawafeji then natoa mzigo napeleka ofisini, Mzigo ukifika ofisini utatunzwa store tukisubiri wenye mizigo yao kuja kuchukua,
Sasa mteja akija kuchukua mzigo wake siku hiyo ambayo mzigo ndio umetoka Bandarini hiyo inakuwa nzuri kwetu tunachokifanya akilipia gharama za kusafirisha tunampatia na Documents za TRA ambazo atatumia kuonesha TRA (Incase akikamatwa) kumbuka huyu haina haja ya kumpatia risiti
Kuna wale wateja wengine utakuta Mfano mzigo umefika Leo Jumanne basi atakuja Jumatatu ya wiki ijayo kufuata mzigo Sasa huyu mtu akichukua mzigo wake halafu bahati mbaya akakamatwa na TRA huwa ni changamoto sana, sitaki sana kuingia deep coz ni vitu sensitive sana
Basi kikao kikaisha tukaagana na Bi Mkubwa, na mimi ndio nilikuwa wa mwisho kuagana nae sababu nilimpeleka hadi Parking akanambia
Mama Accnt: "BM uwepo wako ndio unanifanya niamini kwamba Kampuni ipo katika mikono salama, nimeona unaukaribu kiasi na Caryn, Jitahidi mambo mengine uwe una mshauri, unajua yule Binti yupo smart lakini huwa simuamini sana, nilikubali tu kwa heshima ya Baba yake lakini nilitaka wewe ndio uwe pale"
BM: "Usijali Mama kila Kitu kitaenda sawa, hata hivyo Caryn mbona namuona yupo sawa tu"
Mama Accnt: "wewe si kwasababu umeshazoeana nae, mm namjua vizuri yule Binti atafanya panga pangua hapa ndani ya wiki tu hutaamini utakuja kuniambia"
Basi Bi Mkubwa akapanda kwenye ndinga lake akasepa, mm nikapanda juu nikapitiliza hadi store kwa wana tukapiga story mbili tatu
Mara Secretary akaja store "BM Boss anakuita" hii kauli nilishazoea kuwa nikiambiwa tu Boss anakuita basi ujue ni Bi Mkubwa, sasa Leo hii ka Binti tu rika langu eti ndiye Boss wangu
Basi mm huyo hadi kwa Boss lady nikamkuta yupo na Accountant, niliwakuta katikati ya maongezi
Caryn: "......sawa utafanyia kazi na hizo, utanipa hiyo report after meeting"
Alikuwa anaambiwa Accountant na sikujua walikuwa wanaongelea nn na baada ya maagizo hayo aliondoka nikabaki na Caryn
Caryn: "BM Vipi uko poa?"
BM: "Niko poa kabisa"
Caryn: "BM mm na wewe naweza kusema ni washkaji...je nipo sawa kusema hivyo?"
BM: "Yeah hujakosea"
Caryn: "Sasa ikitokea mshkaji wako kawa Boss wako, usimletee ushkaji kwenye kazi"
BM: "Sijakuelewa, wapi mm nimeleta ushkaji?"
Caryn: "Kilichotokea leo asubuhi hakikuwa sawa kabisa, Yani sijapenda, nilikuwa upande wako kwasababu tu ya yule Binti alinyanyua mdomo wake ila kama ni Mama ndio angekuwa anakusema mm nisingeongea chochote"
Duh! Yani pamoja na kunitetea kule kumbe mtu alimaidi nilivyochelewa, ilibidi tu nijishushe nikamwambia yaishe
Caryn: "Toka kaendelee na shughuli zako halafu naomba After Lunch niitie staff wote kwaajili ya kikao"
Nikarudi zangu store, nikaitisha chakula nikakilia kule kule store, muda wa kikao umekaribia nikawashtua wana, wengine walikuwa chini walienda kuitwa wote tukakutana Ofisini kwa Boss Caryn
Caryn: "Naomba watu wa sales wote mkae upande wa kushoto, baada ya hapo naomba tujitambulishe kwa majina"
Wote wakajitambulisha ila hapo kwenye majina sitaweza kutaja ila kwa kifupi ni kwamba watu wanaodili na store wapo 6 wakiwa na majukumu tofauti,
Wa kwanza ni Storekeeper mwenyewe, huyu ana deal na mizigo inayotoka na kuingia pamoja na kuandika Delivery note, mtu wa pili yeye anadili kupima mizigo tu na kuhakiki kilo, wanne waliobaki ni wa kubeba mizigo na kuipanga au mizigo inapofika pia huwa wanaichana ili kuigawanya (hapa nadhani mtakuwa hamjanielewa vizuri)
Iko hivi, watu huwa wanaagiza mizigo tofauti tofauti Kuna mikubwa na midogo, unaweza Kuta mtu anaagiza mzigo kilo zake haufiki hata kilo moja, na wateja wa design hii pia ni wengi unakuta mwingine mzigo wake ni kilo mbili tu au tatu,
Sasa kinachofanyika hivyo viboksi vidogo vyote vinakusanywa kwenye box moja kubwa, kwenye hilo Box linaandikwa jina la mteja mmoja tu ambaye nae humo ndani ana mzigo wake
Kwa mfano jina la mteja ni Glenn na kwenye Parking list mzigo utaonesha ni wa Glenn lakini ni wa kuchana, Sasa mzigo ukiwa ni wa wakuchana ina maanisha kwamba katika hilo Box kuna mizigo ya watu wengine kwahiyo inabidi itolewa na kila mzigo upimwe kivyake, sasa hiyo kazi yote ndio wanafanya hao vijana,
Watu wa sales hawa haina haja ya kuelezea sana, kama mnavyojua watu wa sales hulipwa kutokana na kazi uliyoifanya, labda niongelee kwa upande wa Kampuni yetu,
Sales hulipwa kwa wateja utakaowaleta na unalipwa kwa kilo utakazofikisha, kilo 1 ni Tsh 500, so ukiwa labda na wateja kumi katika hao wateja wako wote kilo zao zikajumlishwa labda zikafika kilo elfu moja (1,000),
So utapiga 500 × 1000 = 500,000 kwahiyo kwa hesabu ya kwa kila kilo moja 500 ukifikisha kilo elfu moja una laki tano yako, hao ni watu wa sales sasa nao wakajitambulisha kwa Majina mbele ya Boss Caryn
Caryn: "Mliobaki nawatambua haina haja ya kujitambulisha"
(akimaanisha Mimi, Secretary na Accountant)
Caryn: "My name is (****) I'm very excited to meet you guys and honored by this great opportunity to be Managing Director, I'm sure we'll be a great team in getting things done and accomplished around here, together we'll put (Jina la Kampuni) on the map and remember this guys there's no 'I' in team"
"As we all know Air Transport Companies are getting everywhere in this country now, ni lazima tujipange haswa tukiwa na Strategies mpya"
"As the Managing Director I will try as much as possible to create a very cardio relationship with my staff, Because I'm the new one here that enables me to understand you, know your weaknesses and your strengths"
"But, I repeat again 'But' I will no longer tolerate any form of laziness from anyone, so if you can't handle the work then quit"
"Nadhani nimemaliza Accountant Please after this meeting set up another meeting with Sales Team for me and I really need you to supervise them, Mnaweza kuendelea na shughuli zenu BM wewe baki sijamalizana na wewe bado"
Basi watu wote wakatoka nikabaki mimi na Caryn ofisini
Caryn: "BM nimetumiwa Parking list ya mizigo inayoingia kesho kwahiyo jiandae kwaajili ya safari
BM: "Sawa ila itabidi niende na mtu mmoja maana nikisema niende mwenyewe nitashindwa kujigawa mwisho wa siku mzigo utachelewa kufika Dar"
Caryn: "Okay lakini huyu mtu uliyekuwa unaenda nae hapo awali sitaki uende nae tena acha abaki store nikiendelea kukutafutia mtu wa kusaidiana nae"
BM: "Basi mteue mtu ambae nitaenda nae kwa muda"
Caryn: "Utaenda na Mimi"
Itaendelea
We siku ukiepa nae uko punguza njia za kurahisisha tofauti na wakati mwingine. Hii unaua kote kote kwa mara moja yaani TRA na wenzake pamoja na Hako kadada. So wote hawataelewa somo. Ila ujue kwa wakati hukunji kile kibunda ulichozoeaYani we acha tu huyu Demu ni mjanja sana, nilishamsoma, yani anataka ku master kila sector ili aweze ku control vizuri Office
Uko vaa uhusika tofauti na siku zote, negotiation iwe tofauti bila kumtonya TRA wala nani afu muda mwingine mtupie mpira yeye na kwakuwa hizo equation kutatua unajua wewe lazima atambwela na kuamua kukaa pembeni akijua ni knock out umempiga so ujiandae na njia nyingine atakazo kuja nazoUnaenda na Caryn kupigania TRA na ZAT maanina zile negociation za mapolo pale bandari asiwepo ataharibu.
Kwa ujumla wanajua sana kuwa attend wateja wao.
Huyu BM X6 ni bonge la mtu linalojali sana kazi yake na wateja.
Usisite kuwaungisha na hutojuta mkuu
Unajua nawaza kutaja Jina la Kampuni hapa pamoja na Address yake lakini nasita kwasababu story bado inaendelea, Yani hivi ninavyoandika hii comment Bado Kuna matukio yanaendelea
Kama hii last Episode ni matukio ya mwezi wa kumi Mwaka jana (October 2022)
Umakini unahitajika hapo, asije taka kula tunda kimasihara mwisho wa siku akajikuta anaachishwa kazi kimasihara
Story nzuri. HongeraEPISODE 01, SEASON 01
Wakuu nahitaji ushauri wenu ili niweze kufaulu katika huu mtihani, nimepewa kazi kubwa ambayo nikifaulu basi milango mingi itafunguka huko mbeleni.
Kuna Mzee flani huwa tunashirikiana kikazi na mara nyingi mizigo yake huwa anaiagiza kupitia Kampuni yetu, ni Mfanyabiashara na ameanza Biashara miaka ya 90s alivyomaliza tu O level, Sasa huyu Mzee kijana (1971) huwa tunaongeaga mambo mengi kuhusu Biashara huku nikitaka anipe miongozo ili na mimi nielekeze nguvu na akili huko
Huyu Mzee akijaga Ofisini ni lazima nionane nae japokuwa muda mwingi Mimi huwa nakuwa nje ya ofisi kutokana na majukumu yangu mengi si ya kufanyia Ofisini nimesema ni lazima nionane nae ni kwasababu zangu Binafsi na si za kiofisi, Huyu Mzee ndio ameni inspire mm kutaka kufanya Biashara si kimafanikio tu bali hata lifestyle yake, Yani kifupi ana enjoy mafanikio yake anafanya kazi huku amerelax nyakati za kujituma usiku na mchana kwake zilishapita, sio kama wazee wengine wenye Utajiri lakini Bado anajitesa siku nzima kama yeye ndio kaajiriwa jambo ambalo ni tofauti kwa huyu mzee, huwezi kujua ratiba yake muda wowote yupo Ofisini na muda wowote pia anaweza akawa nyumbani, Ni siku ya Ijumaa tu ndio Najua kwamba haendagi ofisini kwake labda kuwe na jambo muhimu sana ambalo linahitaji uwepo wake.
Sio mtu wa mitandao sana hasa kama hii Jf pengine hata haijui, Kuna siku nilimuuliza kuhusu mitandao akanambia anatumia Twitter na Whatsapp tu, so hii story Najua itakua ngumu kwake kuiona, maana hata kwa codes nitakazoweka kama akiiona atajua tu ni Mimi na ndio mchongo mzima utaishia hapo
Sasa nikibahatikaga kukaa na huyu Mzee mtu mbili huwa namuonesha shauku ya mimi kutaka kufanya biashara lakini kila nikimgusia swala hilo ni kama anaona sipo serious, anahisi nataka kufanya biashara kwa kufuata mkumbo tu, Kwasababu nakumbuka aliniuliza nataka kufanya Biashara gani mimi nikamwambia nataka kufanya Biashara kama ya kwake, aliishia kucheka tu
Nakumbuka siku moja nimetoka Zanzibar kupokea mizigo ya ofisi ya wateja, nimefika Dar Huyu Mzee akanipigia simu kuniomba kwamba mzigo wake nisiupeleke store Bali niende nao Ofisini kwetu ili nikitoka kazi nimpitishie kwake, na ndio ilikuwa mara ya kwanza kufika kwa huyu Mzee, Asee vile nilivyokuwa namdhania ni robo yake, Kuna watu wanaishi acheni nyie
Basi Mzee alinikaribisha vizuri sana mjengoni mjengo mjengo kweli! Wakati naingia kwenye Parking sijaona Gari yake niliozoea kumuona nayo siku zote (Land Cruiser ZX V8) nilimkabidhi vitu vyake Mzee akapanda juu Nadhani ni Bedroom kwake alivyorudi akanipeleka Backyard tukakaa, Sasa tulivyokuwa mule ndani sikuona mtu mwingine yeyote ikabidi nimuulize Mzee nyumba yote hii unaishi peke yako? akanambia "hapana mabinti zangu na Mama yao wameenda Kibaha watarudi Jumapili" (Siku hiyo ilikuwa Ijumaa)
Story zikaendelea pale Mzee akanambia "Kijana wangu nilikuambia uniletee mzigo kwa makusudi, mm kila Ijumaa huwa na utaratibu wa kupata chakula Cha jioni na familia yangu ya ndani na ya nje hivyo nilitaka na wewe uwepo" alivyosema familia ya nje niliwaza mbali, nikamuuliza kwani Mzee wewe una wake wa ngapi? kabla hajajibu alitabasamu "mmoja tu na Najua umeuliza hivyo kwasababu gani, nilivyosema familia ya nje nilimaanisha watoto wa mitaani ambao hawana makazi maalum, kwahiyo badae tutatoka kwenda kuwachukua" nikasema sawa ni jambo zuri Mzee
Wakati tumekaa na kuendelea na story Mzee akanambia kama nitataka kunywa chochote niende kwenye fridge nijihudumie, Nikamwambia haina shida, Mara ghafla Mzee akapokea simu Wakati anazidi kuongea akachange ni kama kapokea Taarifa mbaya, yule Mzee aliinuka pale alipokuwa amekaa akiwa bado anaongea na simu huku akiingia ndani, alivyotoka alikuwa kashika funguo mkononi akanambia "Kijana wangu nimepata dharula itabidi nikuache kidogo ila nitajitahidi niwahi kurudi ili tufanye lile jambo nililokuambia, in case of anything utanipigia simu" Nikamwambia sawa Mzee
Tukatoka kule backyard hadi Parking pale kulikuwa na Magari mawili ambayo sikuwahi kumuona nayo akaingia kwenye Jeep, Yale majeep yenye muundo kama wa Benz G Wagon, Mzee alifungua geti na Remote control akasepa, Mtu mzima nikachoma ndani, nikajiachia kwenye Sofa huku nikiperuzi, Giza likaanza kuingia na saa Ile Mzee anaondoka ilikuwa ni around saa kumi jioni.
Simu ikaita, kucheki ni Mzee, akanambia "Kijana wangu ni kama nitachelewa kurudi Sasa wewe Fanya hivi, umeiona hiyo gari hapo parking?" nikamjibu ndio "Sasa panda juu mkono wa kulia chumba Cha mwisho fungua mlango ingia ndani nenda hadi kwenye dressing table utakuta funguo ya Gari ichukue, si unajua kuendesha gari?" nikamwambia ndio lakini Sina leseni Mzee "Wachana na mambo ya leseni, kwani Driving licence ndio inaendesha gari? Sasa si umesema unajua ku drive, nenda jikoni kachukue hicho chakula pakia kwenye gari wapelekee wenye uhitaji sababu ninaweza nisirudi halafu hicho chakula kikaharibika" nikamjibu sawa Mzee akakata simu
Nikawa najiuliza pa kwenda kuwapata hao watoto, Basi bhana Mimi nikapanda juu kuchukua funguo ya Gari, nikazama hadi chumbani asee ni noma, Chumba kama sebule nikawa sielewi dressing table Iko wapi, kilichonisaidia ni kioo, nilivyoona kioo nikajua tu hii ndio yenyewe hadi kesho sijaelewa Ile dressing table imetengenezwaje, kweli nikakuta funguo pale juu Ile kupiga jicho pembeni nikakuta maburungutu ya pesa elfu tano tano, hata sijayagusa maana nilijua nyumba kama Ile haiwezi kukosa CCTV camera, me nikabeba funguo kikashuka chini hadi jikoni nikakuta mahotpot yana msosi wa kutosha (Wali njegere maini) nikayabeba hadi kwenye Gari (Alphard) nikarudi jikoni kucheck sahani zote za dongo nikaachana nazo nikarudi kwenye Gari nikafungua Geti nikasepa ila sasa nimetoka na sijui naelekea wapi nikicheki saa ni saa moja kasoro, nikaenda hadi Mwenge, nikapark kando ya Barabara nikawa nawaza hao watoto nitawapata wapi, mawazo yakaja niende kwa sister angu flani anakaa uswahilini huko ndiko nikagawe hiki chakula, nikapiga mahesabu ya masaa nitakayo tumia hadi kufika huko muda utakuwa umeenda hata hivyo nitakuta watoto wengi wapo majumbani mwao na watakuwa washakula nikaona nikifosi kufanya hivyo nitaendelea kuipa nguvu ile kauli ya "mwenye nacho huongezewa"
Nikatoka pale Mwenge nikaenda Buguruni, nimepitia Ile footbridge na Mataa nikaingia Barabara ya kama naelekea Ilala, sijafika hata mbali nikapark pembeni kusikilizia, sijakaa sana nikaona madogo wawili nikawasimamisha Nikawauliza wanapoishi hawakunijibu, nilivyoona hivyo sikutaka story nyingi tena niwaambia ninachakula nataka niwapatie lakini nyie wawili hamtakimaliza mnaweza kuwaita na wenzenu? mmoja akaniuliza "kiko wapi hiko chakula chenyewe?" nyie kawaiteni wenzenu mkija mtakiona chakula, nitawaambia hivyo wakaondoka nikakaa kama Dakika 8 nikaona wale madogo wanakuja na rundo la madogo wenzao nikajisemea Leo kazi ipo maana kwa Ile idadi niliyoiona ya wale watoto na nikipiga mahesabu ya kile chakula nilichobeba ni kama hakitatosha kabisa halafu saa hiyo hiyo nikakumbuka nilibeba tu chakula na sikubeba sahani nilipanga nipitie supermarket ninunue zile sahani za karatasi nikasahau
Madogo wakafika hadi kwenye gari, nikawauliza mgahawa wa karibu uko wapi?wakanionesha lengo nikwenda kununua chakula ili niongezee na hapo hapo nitapata sahani za kutumia kwasababu kwa kile chakula kilichopo kinatoshea kwa watu kama 9 ivi na kile kikosi Cha madogo 15 wamefika, nikalock gari nikawaacha madogo pale kwenye gari nikavuka Barabara hadi upande wa pili nikaulizia chakula nikaambiwa kipo, saa hyo ni saa 2 usiku na madakika yake, Nikwambia Mama ntilie nataka chakula Cha watu kama kumi, Yani sahani kumi za wali, akanipakulia akaniwekea kwenye ndoo, nikatumia ujanja wa kumwambia kila sahani ifunike ili chakula kisipoe ili nipate sahani excess, alivyomaliza nikampatia 20k Nikamwambia siendi mbali sana sahani nitakuletea mwenyewe, akakubali bila wasi na sijui kwanini aliniamini kiwepesi vile
Nikafika kwa madogo nikafungua gari nikatoa Yale mahotpot ujinga mwingine ambao niliufanya sikubeba vijiko vya kupakulia na kule kwa Mama ntilie sikuchukua Maji ya kunawa, Sasa ule msosi wa Kwenye hotspots nikaupakua kwa kutumia sahani nikakigawa kile chakula wengine ilibidi wale wali wa mama ntilie na baadhi yao wakala ule niliokuja nao ila ngegere na maini nilizigawanya katika Kila sahani, sasa nikawa nawauliza madogo mtanawa wapi mikono?, dogo mmoja akasema blaza haina haja mikono yetu misafi[emoji3] basi nikawaruhusu wafinye msosi na mm nikichukia sahani moja, walivyomaliza Nikaingiza mahotpot kwenye gari nikalock nikamchukua dogo mmoja Nikamwambia abebe ndoo yenye sahani anifuate wale wengine niliwaambia watusubiri, tukaenda hadi kwa mama ntilie nikampatia sahani zake akanirudishia balance yangu elfu 5, nikamuomba chenchi ya elfu 10 buku buku, akanipatia, tukarudi hadi kwenye gari na yule dogo, Nikawaambia Sasa Mimi na nyie tushamaliza nikampatia Kila mmoja buku buku angalau kesho Asubuhi wawe na uhakika nikaagana nao pale nikasepa, Wakati nipo Njiani nikampigia Mzee kumjulisha kwamba nishafanya kile alichoniagiza akanambia "sawa Sasa wewe unaweza kwenda na hilo gari kesho utalileta nyumbani, si ulifunga vizuri nyumba?" aliniuliza Nikamwambia ndio na funguo Niko nazo, "Haina shida ww unaweza kwenda kupumzika Sasa" okay Mzee, Sasa wakati huo naongea nae kwenye simu Mimi nilikuwa nishapita Ubungo Interchange naitafuta Mwenge, nikielenda nyumbani kwake, ilibidi nigeuze gari nilirudi nilikotoka sababu mm naishi Tabata, Yani kama ningewahi kumpigia simu basi nisingejisumbua kufika mbali kote huko
Kwa mara ya kwanza nafika mtaani kwangu na Gari, siku zote Mimi niwakufungua kale kageti kadogo Leo nafungua Geti lote kubwa ili kuingiza ndinga, maana nilipopanga tunakaa watu 3 nyumba zinajitegemea ila tunashea Compaund, nikapark gari nikaingia ndani kulala, kukakucha, Jumamosi mara nyingi huwa siendagi ofisini labda itokee naenda Zanzibar, so nikawa Sina ratiba ndefu nikafua nguo kadhaa nikaingia mtaani kupiga chai, nilivyomaliza nikarudi home direct nikakuta missed call ya Mzee maana nilivyotoka simu niliiacha, nikampigia akanipa maelekezo fulani pale ya kwamba atarudi Jumapili Pamoja na familia yake hivyo kama Nina muda nilipeleke Gari kule nyumbani au nibaki nalo hadi Jumatatu aje alichukulie Ofisini, nikamjibu sawa yote yanawezekana ila acha niangalie lipi litakuwa rahisi zaidi
Baada ya kukata simu nikapiga hesabu kurudisha hili Gari hadi kule mwisho wa mji, nikaona uvivu isitoshe gari lenyewe lilikuwa rafu mavombo machafu humo ndani, Yani ukifungua mlango wa gari Gari lote linanuka wali, nikatoa vyombo vyote, nikajikaza kuviosha hakuna Kitu kinanikera kama kuosha vyombo ndio maana huwa sipikagi mara kwa mara. nilivyomalizana na hiyo Kero nikalipeleka Gari Car Wash nikalirudisha kulipark home, hamuwezi amini nilishinda ndani hiyo weekend yote hadi inaisha na Gari limepark tu uwani
Jumatatu hii hapa, Asubuhi na mapema nikawa najianda kwenda kazini, Nikaingiza vile vyombo kwenye gari ila Sasa nikawa nawaza hao police huko Barabara kwasababu Sina Driving licence, nikasema potelea mbali nikatekenya mchuma hadi kazini nikalipark kimya kimya kama sio Mimi nikaingia Ofisini kwaajili ya kuchapa kazi
Imefika Lunch time najiandaa kwenda kupiga Menu yule Mzee nikamuona anaingia Ofisini halafu ana hasira amekunja sura, nikajisemea hapa kimeshanuka nikaanza ku recall matukio ili nijue ni wapi nimekosea hasa kule nyumbani kwake, kote nilicheza safe na mara ya mwisho kuongea na huyu Mzee ilikuwa ni Ile Jumamosi akinipa mabadiliko ya ratiba yake huku akinipatia option mbili za yeye kupata gari yake, na Mimi nilivyochagua kubaki na Gari hadi Jumatatu sikumpigia tena simu kumjulisha uamuzi niliouchukua....nikapata majibu kwamba inawezekana hapo ndipo nilipo haribu, alikuja kwenye desk langu na kuniambia "nipatie funguo ya Gari na ukimaliza kazi nitafute" hata hakunisalimia akatoka nje ya ofisi akaondoka....
Inaendelea badae acha nipate msosi.....story yangu ina episode 6 tu, episode ya kwanza na ya mwisho (1 & 6) ndio muhimu zaidi Sababu ushauri wako ndio unahitajika hapo
1. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
2. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
3. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
4. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
5. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
6. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni