A man with no name
JF-Expert Member
- May 7, 2017
- 1,135
- 1,574
Pole mkuuMzee wangu visanga vilitokea hapa katikati ni noma
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pole mkuuMzee wangu visanga vilitokea hapa katikati ni noma
Oya kuna siku nilitaka kuji mix....kama ni mitego nimeikwepa mingi sana hata siku nikija kunasa huko mbeleni itakuwa sio kwa uzembe tenaSema huyu dogo caryn aisee, usije kujiroga ukawaza kumla, iwe kimasihara au kwa kudhamilia. She's a headache.
huyu michelle atakuwa analiwa tigo na lijamaa sio kwa kupenda huko dah
Kwa akili za Caryn akitimuliwa home anaweza sema anataka ahamie kwako maana hawezi kulala peke yake
[emoji134] Dah acha nisiseme kitu, we jamaa unanijua nini nje ya Jamii forum? Haiwezekani code unazifungua halafu unapita mule mule
Her problem ni kwamba, hana adabu hata kwa mtu anayempenda. Watu wa jinsi sii hupenda kunyenyekewa.Oya kuna siku nilitaka kuji mix....kama ni mitego nimeikwepa mingi sana hata siku nikija kunasa huko mbeleni itakuwa sio kwa uzembe tena
Oya kuna siku nilitaka kuji mix....kama ni mitego nimeikwepa mingi sana hata siku nikija kunasa huko mbeleni itakuwa sio kwa uzembe tena
Hongera sana. Ni wachache sana wenye misimamo kama yako. Hata mimi ningeshindwa. Ningeishia kuharibu. Maana ningepita nao wote watatu kitamboOya kuna siku nilitaka kuji mix....kama ni mitego nimeikwepa mingi sana hata siku nikija kunasa huko mbeleni itakuwa sio kwa uzembe tena
Anie na Accoutant walishaliwa kitambo sana, pengine na Mdhungu MD wa logistics company ameshaliwa ila bado hatujafika uko, tuliza mtori nyama zipo chini mkuu.Duuuh...! Kweli kuna jamaa elimu imewasaidia sana sana. Kwanza unajua nini maana maisha. Unajua kujiheshimu (kama ni kweli kote ulikotupitisha). Pili unajua kupangilia maneno,habari na kikubwa husahau ulichokihadithia. Tatu unajua Kiswahili fasaha sana sio wale wa "mpaka" anaweka "mbaka". "Hapa" anaweka "apa".
Mwisho hongera sana kwa msimamo wako mkuu. Kama alivyoongea mzee uko smart. Mimi najijua ni smart lakini kwako nimekwama saanaaaa. Maana mpaka sasa ningekuwa nimetafuna Anie. Nmetafuna kitambo akauntant. Ningekuwa nimemtafuna Caren. Saa hizi ningekuwa mbioni kumla Mishele.
Hongera sana.
Unatufundisha mengi.Hizi ndio zinafundisha uhalisia wa maisha. Mwisho nayaona mafanikio ya maisha yako.
Kuna kitu kimenigusa sana hapo. Wale vijana na watatu. Natamani nikawasake na mimi hata watatu wa mitaani niwe nawapa chochote nitakabarikiwa.
Asante sana kwa story yako mdogoangu na hongera
Dah! Shukrani mkuu umeenda deep sana, I appreciate [emoji1545]Duuuh...! Kweli kuna jamaa elimu imewasaidia sana sana. Kwanza unajua nini maana maisha. Unajua kujiheshimu (kama ni kweli kote ulikotupitisha). Pili unajua kupangilia maneno,habari na kikubwa husahau ulichokihadithia. Tatu unajua Kiswahili fasaha sana sio wale wa "mpaka" anaweka "mbaka". "Hapa" anaweka "apa".
Mwisho hongera sana kwa msimamo wako mkuu. Kama alivyoongea mzee uko smart. Mimi najijua ni smart lakini kwako nimekwama saanaaaa. Maana mpaka sasa ningekuwa nimetafuna Anie. Nmetafuna kitambo akauntant. Ningekuwa nimemtafuna Caren. Saa hizi ningekuwa mbioni kumla Mishele.
Hongera sana.
Unatufundisha mengi.Hizi ndio zinafundisha uhalisia wa maisha. Mwisho nayaona mafanikio ya maisha yako.
Kuna kitu kimenigusa sana hapo. Wale vijana na watatu. Natamani nikawasake na mimi hata watatu wa mitaani niwe nawapa chochote nitakabarikiwa.
Asante sana kwa story yako mdogoangu na hongera
Usituangushe vijana wenzio ww mtokee tu carn Kama kazi basi mwanaume rijali unakosea sana carnDah! Shukrani mkuu umeenda deep sana, I appreciate [emoji1545]
Nilikuwa na Mpango wa kuleta muendelezo tarehe 5 mwezi wa 3 yani jumapili ya wiki ijayo lakini kwa comment yako nitajitahidi kuleta muendelezo jumamosi ya kesho kutwa, nikichelewa sana jumapili
Haina haja ya kumtokea yeye mwenyewe kwani hahitaji mme ,atamtokea akimuona ndiye amfaaye maishani mwake. What it means to be to you it means or come easily and effortless and when it's time to leave you let it leave your effortless with no personal fragile ego in stakeUsituangushe vijana wenzio ww mtokee tu carn Kama kazi basi mwanaume rijali unakosea sana carn
Hahaaa eti mafta taaDah ila Michelle amekuwa mafta yataa
Kumbe ulihamia sehemu mpya?Ilipoishia
Tukafikà kwenye gari Caryn akaona jinsi gari ilivyo haribika, nikamuona tu anatoa simu halafu akanipa funguo
BM: "Mimi funguo ya nini sasa?"
Caryn: "Unauliza funguo ya nini? we huoni Ulichokifanya?"
BM: "Naona, ila sasa una maana gani mm kunipa funguo?"
Caryn: "Maana yangu ni kwamba unirudishie hio funguo gari likiwa kama nilivyokukabidhi....
BM: "Sasa wewe unarudije nyumbani?"
Caryn: "Mimi nitajua narudi vipi, hata ku request nita-request"
BM: "Ebu acha utoto bhana, uta-request vipi Wakati Gari hili linaendesheka kabisa"
(Nikamshikisha funguo yake mkononi)
Caryn: "BM tunapimana akili sio? for your own good chukua hii funguo na kesho muda kama huu naitaka hii gari iwe imeshakamilika"
Muendelezo
(Episode 15 SEASON 2)
Nikachukua funguo nikajua huyu tayari kashamaindi nikaenda kukaa kwenye gari ndani kusikilizia labda anaweza badilisha mawazo, hakupita muda mrefu kupitia side mirror nikaona IST imekuja ikamchukua, Eeh ndio nikajua kumbe yupo serious na alichokuwa akikiongea
Ikabidi na mimi niwashe mzigo wangu niondoke maana sio gari tena naona kama ni mzigo, nikafika nayo hadi mtaani mida ya saa mbili kasoro usiku nikamcheki mshkaji wangu kumjulisha kwamba nimesusiwa gari, sikutegemea jibu alilonipa mshkaji
Eti "Kama vipi ibuka nalo mtaani twende tukale nalo bata viwanja" nilimjibu tu "kutoka tena itakuwa ngumu nina uchovu wa kutosha'
Ila mshkaji niliona kama ananiletea miyeyusho, Yani gari lina majanga anataka tukale nalo bata kwa mfano likitokea janga lingine? si ndio nitaambiwa nilinunue kabisa gari lenyewe
Kesho yake mida ya saa tatu asubuhi nikamcheki mshkaji akanambia nimuibukie mtaani, nikamuibukia mshkaji sijapita hata ofisini, Nilivyofika mtaani kwa jamaa gari lenyewe nikalipaki nje sikutaka mambo mengi
Mshkaji: "Ivi sijakuambia...yule jamaa wa kuirekebisha taa Jana alinicheki alienda Morogoro msibani ila anageuza leo masaa ya mchana mchana atakuwa kashafika town"
BM: "Dah! Oya kama vipi tukaanze na rangi tuokoe muda, kitambo hadi huyo jamaa ako afie tutakuwa tushamalizana na kipengele kimoja"
Mshkaji: "Lakini kwa ushauri wangu tungeanza na taa ila kwasababu ww ndio unaamua fresh"
MB: "Hizi heka heka za magari kwa huku bongo sijawahi kudili nazo, ni wapi wanafanya panel beating na kupiga rangi vizuri"
Mshkaji: "Sehemu ziko nyingi ila kidogo mfuko wako inabidi uwe umechangamka"
BM: "We twende bhana ila usinipeleke sehemu expensive sana"
Mshkaji akanipeleka Garage flani maeneo ya Mikocheni tumefika garage picha linaanza tukaambiwa tukabidhi gari halafu sisi tuende ofisini kuna viti vya wageni full kipupwe kama tupo njombe, sasa ili kubalance kipupwe na joto la mwili tukaletewa Kahawa ya motooo
Masaa kadhaa kupita tukapewa taarifa kwamba chuma ipo tayari, nikapewa invoice nikalipia, huduma ilikuwa nzuri lakini kibunda nacho kilinitoka
Tukakabidhiwa Gari kwenye majira ya saa nane mchana, Kilibaki kipengele Cha Headlight na uzuri jamaa nae alikuwa kashafika town tukampelekea gari, akacheza nayo chuma ikarudi kwenye ubora wake....siku hadi inaenda kuisha sikuwasiliana na Caryn
Nikamcheki kwenye simu wakati naelekea ofisini ilikuwa saa kumi na moja jioni na dakika zake, simu haikupokelewa kufika ofisini nikakuta wamefunga
Nikasema ngoja nimpigie Michelle pengine yupo nae, Michelle akanijibu kwamba alikuwa nae muda sio mrefu ila ametangulia nyumbani walikuwa waondoke wote ila ni kama Michelle Bado ana viporo vya kazi ofisini
Halmashauri ya kichwa ikanambia hili gari kama lipo sawa halina tatizo nisilale nalo tena, nilirudishe kwa mwenyewe hata kama nimemcheleweshea, wanasema heri nusu shari kuliko shari kamili
Nikatia Gear kuelekea kwa Mzee, nimefika kwa kina Caryn na Caryn mwenyewe hayupo nimemkuta Mzee na Bi Mkubwa, nikasalimiana nao
Mzee: "Gari imeshafaa?"
Ka moyo kakafanya Pah! nikashtuka, (nikajua hapa Caryn kashamchana Mzee)
BM: "Yeah, ilikuwa ni sehemu ndogo tu"
Mzee: "Sasa na yeye amegonga gongaje! mbona ameanza kuwa mzembe, Gari mpya ameanza kuitia viraka"
(Nikagundua hapa kuna venye Caryn kachanganya ukweli na uongo, hiki anachokiongea Mzee ni kama vile amemuambia Gari ameligonga yeye)
Ikabidi na mimi nitambae na beat, alipoishia na mimi niendeleze
BM: "Ilikuwa bahati mbaya tu Mzee haikupata damage kubwa hivyo"
Mzee: "Nilishangaa Jana mtu anarudi bila gari namuuliza akasema kakuachia ili umpelekee garage"
BM: "Yeah, ni kweli na hata hivyo garage kwenyewe nimechelewa kutoka nilivyopita ofisini sikumkuta nikaona nimletee tu huku nyumbani"
Mzee: "Umefanya vizuri"
Sikukaa sana, muda ule ule ikabidi nimuage Mzee maana ningeendelea kukaa pengine ningejichanganya kwenye maelezo na sijui Caryn kamuambia vitu gani Baba ake
Nikarudi zangu kwangu, kesho yake Asubuhi nikatimba ofisini, nikakuta Storekeeper pamoja na Secretary wameshafika Caryn alikuwa bado hajafika na Accountant, nikashuka chini kushtua utumbo na chai ya moto
Kabla hata sijaletewa chai maana ilikuwa Bado ipo jikoni nikaona Bimmer ya Caryn inaingia, akashuka akaelekea ofisini, nilivyoshtua utumbo nikarudi ofisini nikaingia kwa Caryn
BM: "Madam, vipi uko poa?"
Caryn: "Yeah, I'm good"
BM: "Gari umeionaje? Iko sawa?"
Caryn: "Nilikuachia gari ofisini kwanini uliamua kuileta nyumbani? why?"
BM: "Sasa nakupigia simu hupokei na wewe ulisema gari yako unaitaka jana, unadhani mimi ningefanyaje? maana nilikuja ofisini nikakuta mshafunga"
Caryn: "Lakini sikukuambia ulipeleke nyumbani ww ungebaki nalo tu, haya ulivyofika nyumbani Mzee akasemaje?"
BM: "Mimi hata sikukaa nilimkabidhi funguo nikaondoka"
Caryn: "Hajakuuliza chochote?"
BM: "Hapana, aliniuliza tu kwamba gari lipo sawa? nikamjibu lipo sawa"
Caryn: "Sasa nikuulize na wewe ilikuwa ukagonga gari?"
BM: "Ooh, kwasababu gari limeshatengenezwa ndio unataka kujua ilikuaje ila Jana hukutaka kujua hayo mambo"
Caryn: "Ningekupa hiyo nafasi jana ningekuonea huruma though nilikuonea huruma hata hivyo, maana najua umetoboka hapo ulipo, ivi Headlight umenunua bei gani?"
BM: "Na nimetoboka kweli, taa Ile nimenunua milioni moja na laki nne"(Uongo)
Caryn: "Duh! pole mwaya, ndio ukome hata hivyo"
BM: "Gari yako siendeshi tena"
Caryn: "Wewe kwa unavyopenda magari, utaendesha tu na ukiharibu unalipa"
Muda wa kazi ukaisha, jioni Wakati nipo nyumbani napunga punga upepo kwenye balcony uzaramoni wanaita kibaraza Michelle akanipigia simu
Michelle: [emoji338] "Hello"
BM: "Yes"
Michelle: "Vipi uko poa?"
BM: "Yeah niko poa"
Michelle:. "Upo na Caryn?"
BM: "Hapana, niliachana nae ofisini"
Michelle: "Ooh, nikajua upo nae, vipi kazi yangu imefikia wapi?"
BM: "Kazi yako bhana nisha-play part yangu, so wewe msikilizie Caryn mwenyewe"
Michelle: "Majibu ya hivi ndio siyataki, wewe yule unammudu unajua, sema hujajua tu"
BM: "Sasa yeye ndio mwenye maamuzi unataka Mimi nifanyaje?"
Michelle: "Hujam convince vya kutosha, wewe kama mtu kosa lako analifanya lake atasokaje kukusikiliza"
BM: "Una maanisha nini unaposema kosa langu akalifanya lake"
Michelle: "Ooh unadhani mimi sijui kama mmemuongopea Mzee kuhusu gari, Mimi najua wewe ndio umegonga gari lakini Caryn kamuambia Baba ni yeye ndio amegonga"
BM: "Sasa kwani kuna shida gani? si ilitokea tu bahati mbaya kama ni gari nishalitengeneza"
Michelle: "Hapa shida sio gari tena, shida ni uongo mlioutengeneza ukijakugundulika ni uongo, kama ulikuwa hujui uongo ni adui namba moja wa Mzee na Mzee akija kugundua wewe na uongo ni marafiki automatically na wewe unakua Àdui kwa Mzee...Mimi nimemaliza
Akakata simu....hii sasa sio kawaida hawa mabinti wa Mzee ni kama kuna mchezo wananichezea, inawezekanaje Michelle kupata taarifa ninazojadili Mimi na Caryn tu kama sio Caryn mwenyewe anayemwambia hizi habari
Kupoteza mawazo nikampigia Annie nikaongea nae kama nusu saa ivi, eti ananiambia "Sasa hivi najua huyo Accountant atakuwa kashamia kwako kabisa" angejua tu huyo mtu haniambii kitu sasa hivi, basi tutaagana na kutakiana usiku mwema
Kesho yake jioni tumeshafunga ofisi wafanyakazi wote wameshaondoka nipo mimi na Caryn tu tumebaki ofisini, nikamuuliza Caryn issue ya gari
BM: "Caryn ivi Michelle anajua kama gari lako liliharibika?"
Caryn: "Yeah anajua"
BM: "Amejuaje?"
Caryn: "Si nilimuambia"
BM: "Lini?"
Caryn: "Bro! too much questions! what's wrong?"
BM: "Nataka tu kujua"
Caryn: "Aah achana na hizo mambo tuondoke"
BM: "Hapana Caryn Nipo Serious nataka kujua"
Caryn: "Kujua nini sasa"
BM: "Ulimuambia lini?"
Caryn: "Anyway, nilimuambia juzi siku ambayo ulitakiwa uniletee gari hapa ukachelewa nilipita ofisini kwake aliniona sina gari alivyoniuliza nikamuambia tena nikamdanganya sasa"
BM: "Aje?"
Caryn: "Nilimuambia nimechubua rangi so gari nimeiacha garage"
BM: "Sasa mbona yeye anajua mimi ndio nimeigonga"
Caryn: "Mmh! kajuaje? kwasababu unajua Hadi Mzee nimemdanganya anajua ni mimi ndio nimegonga that's why nilikuwa na wasiwasi juzi ulivyoenda isije ikawa umeropoka mambo tofauti na niliyoongea"
BM: "Mm nilivyosikia maelezo ya Mzee nilijua kabisa umemdanganya so na mimi nilipita mule mule ulipopita japokuwa sikujua kwanini ulimdanganya"
Caryn: "Aah achana nao bhana issues ndogo tu hiyo isikuwazishe"
BM: "Caryn ivi ulisema unatumiaga pombe eeh?"
Caryn: "Yeah, but only wines na sinywi kulewa vipi unataka kunitoa out?"
BM: "Now I got you, kuna venye unakunywa ukiwa Michelle hadi unaongea ambayo hukupaswa kuongea"
Caryn: "Yani wewe bado uko na hizo mada! nikajua tushafunga chapter, ebu twende watu wasije wakatufikiria vibaya"
Tukafunga ofisini kigiza kilikuwa kishaanza kuingia kila mtu akashika njia yake, jumamosi yake huwa ni nusu siku wakati tunakaribia kufunga Ofisi Caryn akanambia hana pa kwenda so anataka akapaone kwangu
Kweli tulivyofunga ofisi tukasepa wote, mara nyingi kwenye safari ambazo nipo na Caryn huwa ana prefer mimi niendeshe lakini kwa mara ya kwanza hiyo siku nilimkatalia, akakaa kwenye Steering mwenyewe kazi yangu ilikuwa tu kuelekeza njia hadi tukafika
Kitu kimoja kuhusu Caryn huwa hapitishi vitu kirahisi, Yani Mfano umenunua saa atakuponda atakuambia "saa gani sasa hiyo" nakumbuka trip niliyoenda nae Zanzibar ile siku nilitinga shati langu flani ivi mwenyewe naliaminia akanambia "huongozani na mimi ukiwa umevaa hilo shati" hamuezi amini nilibadilisha pesa alitoa yeye lakini ya kununua shati jingine
Hata kule nilipokuwa nakaa zamani alikuwa hapakubali lakini nilivyofika nae makazi mapya mwenyewe alipakubali hadi nikashangaa....tulivyofika tu
Caryn: "Sasa hapa nakupa nyota zako bro, pazuri sana"
BM: "Aah basi kweli hapa pazuri hadi wewe umepakubali!"
Caryn: "Halafu sio kuzuri tu, kumetulia pia....hizi nyumba zote zina watu?"
BM: "Yeah zote zina watu"
Caryn: "Lazima watu wapakimbilie, nyumba moja ingekuwa vacant ningechukua"
BM: "Usiongee sana ebu twende ndani"
Tukaingia ndani bhana Disappointment zikaanza kama kawaida yake
Caryn: "Dah! nyumba nzuri unaweka mapazia ya kichaga"
BM: "Ushaanza, ebu sema unakunywa nini nikuhudumie mgeni"
Akanambia anachokunywa nikamletea story zikaanza, katikati ya story akauliza
Caryn: "BM unajua wewe ni Gentleman and you're handsome, nahisi una Mwanamke lakini hujawahi kunitambulisha, labda nikuulize una Mwanamke? I mean fiance or something"
Dah! Hili swali limekuwa la ghafla mno halafu anauliza huku ananiangalia machoni, hiyo ni kumaanisha nini...kwamba mdomo unaweza kuongopa lakini macho hayaongopi...
Itaendelea
Hii story imekua ni nzur sana BM X6. Inatoa experience za maisha at sometimes na kama alivyosema ndugu hapo haichoshi kwa sababu uandishi wako ni mzur mno.. nami niungane nae nikupe Hongera kwa hili.. tuko pamoja mkuu.. My appreciation piaDah! Shukrani mkuu umeenda deep sana, I appreciate [emoji1545]
Nilikuwa na Mpango wa kuleta muendelezo tarehe 5 mwezi wa 3 yani jumapili ya wiki ijayo lakini kwa comment yako nitajitahidi kuleta muendelezo jumamosi ya kesho kutwa, nikichelewa sana jumapili
Asante sana karibu. Tunajifunza mengi mkuuDah! Shukrani mkuu umeenda deep sana, I appreciate [emoji1545]
Nilikuwa na Mpango wa kuleta muendelezo tarehe 5 mwezi wa 3 yani jumapili ya wiki ijayo lakini kwa comment yako nitajitahidi kuleta muendelezo jumamosi ya kesho kutwa, nikichelewa sana jumapili
🤣🤣🤣😜😜....! Sawa mkuuAnie na Accoutant walishaliwa kitambo sana, pengine na Mdhungu MD wa logistics company ameshaliwa ila bado hatujafika uko, tuliza mtori nyama zipo chini mkuu.
Yaah! Mimi muumini wa lugha fasaha, iwe Kiswahili au Kingereza. Unazitendea Haki sana lugha zote.Dah! Shukrani mkuu umeenda deep sana, I appreciate [emoji1545]
Nilikuwa na Mpango wa kuleta muendelezo tarehe 5 mwezi wa 3 yani jumapili ya wiki ijayo lakini kwa comment yako nitajitahidi kuleta muendelezo jumamosi ya kesho kutwa, nikichelewa sana jumapili