Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Umemchana vizuri kabisa japo hatujui nini kimemsibu unaweza kuta kaugua labda. Pamoja na kia story yake nzuri sema ikikaa sana ina bore coz inapoteza hata kumbukumbu za matukio ya mwisho ili kuunga story inayoendelea. Kama ana busara akusikilize na abadirike.
 
Mimi napongeza watoa story wengine kama Kigakoyo.....Jbourne96.....SinganoJr....pamoja na umughaka....wanajitahidi sana sana sana.
Kunae na huyu mwamba mwingine wakuitwa mireille aisee jamaa ni shenz kabisa,mwamba anazitiririsha kama hana akili vizuri,ukisoma hiyo utampa salute,post alitupia kwa siku 1 tu wewe unasoma wiki nzima na ni tamu blaa😂,
I salute you mwamba
 
Wewe ni popoma

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Yote umeyataka mwenyewe kukaziwA. Saa hizi ungekuwa boss mwenyewe. Kila kitu kingekuwa kwenye maamuzi yako
 
BM hii story yako ni nzuri sana tafadhali rudi ushushe episodes umetupa addiction alafu unatutelekeza
 
Hiyo Penzi la Amida itupie hapa tuone mkuu
 
Hii Penzi la Amida sijawahi ipitia. Itupie kichwa hapa tuone ili iwe rahisi kuifuata mkuu
 
Asante mkuu. Tupia na hiyo How I met my Wife mkuu
 
"Najua watakusaidia kunipopoa"[emoji23].

Story imejaa events ambazo sio za lazima.

Tunaweza kuelewa stori yako hata pasipo kutuelezea namna gani unafanya shipping ya mizigo na delivering.
 
Labda nianze kwa kuwatoa wasiwasi wale wanaodhani nitasusa Uzi, Hilo haliwezi kutokea, na sikatazi mtu kutoa maoni yake hata mkinitukana mimi nitayasoma tu na uzuri ni kwamba mimi nikiwa free kama hivi huwa nasoma kila comment, hata aliyecomment nukta huwa napitia comment yake

Iko hivi, nilishindwa kutoa muendelezo jumapili Ile iliyopita kama nilivyoahidi kwasababu jumamosi yake nilisafiri na Mzee nimekuja nae Mwanza, na hadi leo hii tupo huku ila tunategemea kurudi week hii hii kama mambo yataenda sawa kama alivyopanga

Na muda mwingi nipo pamoja na Mzee, muda ambao naacha na Mzee ni ule muda wa kwenda kulala tu, sasa siwezi kuwa na Mzee tumekaa Mahali halafu mimi nipo Busy na simu naandika story, (labda mtasema kwanini nisiandike usiku muda ambao nakuwa peke angu) Huo usiku nao nakuwa nimechoka kwanza natakiwa kuwaza ratiba za siku ya kesho yake, so muda kama huo nautumia kupumzika

Yani ni vile tu hamjui na ndio maana nikiona mtu anatoa maoni yake kwa makasiriko mimi huwa hata sikasiriki wala kumshangaa, kwahiyo nikisema niwaendekeze ili kuwafurahisha naweza kujikuta naharibu sehemu nayopatia ugali kwasababu upande mmoja nita loose focus

Kuandika story (labda kichwa changu ni kizito) huwa inanichukua hata siku nzima, nimemshangaa yule jamaa aliyesema Dakika 20 tu inatosha kuandika episode 1, blaza shida sio kuandika tu kwasababu hii sio story ya kutunga, shida ni kukumbuka matukio, mf mdogo ni zile sehemu Caryn anazotema Yai,

Ivi mnajua kwamba asilimia 90 ya conversations anazofanya Caryn ni za Kingereza, na ili story ivutie inanibidi nipite mule mule lakini ninachokifanya kwa baadhi ya sehemu mimi huwa natafsiri maongezi yake kwasababu nikisema niandike Convo zake kama zilivyo kuna baadhi ya watu hawataelewa, kwanza mm mwenyewe kuna misamiati mingine anayoongea siielewi maana yake, so natumia ujanja wangu kuunganisha maneno

SO nimesema huwa inanichukua siku nzima kwasababu ya kukumbuka matukio na kuyapangilia, na siku zote nikimalizaga kuandika episode huwa naipitia kuisoma zaidi ya mara tano, sometimes naweza nisipost siku hiyo niliyomaliza kuandika nikaja kuipost siku inayofuatia, yote hiyo ni ku make sure hakuna tukio muhimu nililolisahau kwasababu ilishanitokea nimepost episode nikaja kukumbuka Kuna Mahali niliruka

Halafu katika maisha usijilinganishe na mtu mwingine, Mimi kunifananisha na watu wengine wanaoleta story humu ni kunikosea, kwasababu I'm sure tumetofautiana katika kila kitu hadi katika ku priorities mambo

Mimi mwenzenu focus yangu ipo kwenye kazi ambayo inaniweka mjini huku Jamii forum huwa nakuja kuchungulia tu nikiwa free kama hivi, na naamini pia nyie mna kazi zenu zinazowaweka mjini mkishapiga pesa huko mtaani ndio mnakuja kuchungulia humu kama BM kaleta muendelezo

Sasa kama Mimi mwenyewe hii story siipi umuhimu wa hivyo kwanini wewe ujichoshe kwa kuipa kipaumbele namna hiyo, kama ni muhimu sana basi wekeni Dau nikirudi Dar nishushe Episodes back to back kwasababu Mzee kaniambia tukirudi nipumzike siku Saba lakini siwezi kufanya hivyo mimi nina maisha gani ya kupumzika bhana, japokuwa nikipumzika mshahara wangu upo pale pale lakini nikienda job ndio napiga hela zaidi

Narudia tena fanyeni kazi hapa tunakuja kubadilishana mawazo na kuburudishana tu....au inawezekana wenzangu mnapiga pesa huku mmekaa!? kama ndio hivyo wekeni Dau mezani na mimi nipige pesa huku nimekaa kwa kuandika story. Mkifanya hivyo mm nitapumzika hiyo week moja ya Mzee aliyonambia na focus yangu yote nitaihamishia hapa......Deal???

Kwaherini bhana Mzee ni kama anakaribia kutoka lunch time hii
 
Umeeleweka mkuu, we piga kazi.

Hata hivyo wanalalamika ni wachache, watu wengi wanapita kimya kimya.
 

Kazi kwanza burudani baada ya kz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…