Ilipoishia
Ikabidi tu nimuelewa japokuwa anachokiongea kina make sense ila naona kama ana complicate sana mambo, tukaweka Kila kitu sawa Ilivyofika saa mbili kasoro tukarudi hotelini
Tukapiga msosi tukamaliza tukaelekea vyumbani, chumba changu hakipo mbali na chumba Cha Caryn, nilivyofika tu kwenye room yangu nikaingia bafuni kuoga, natoka bafuni namkuta amekaa kitandani nikajua tu huyu amekosa usingizi anataka tukeshe tukipiga story
BM: "Vip kwema?"
Caryn: "Itabidi tulale wote humu, mimi ugenini siwezagi kulala peke yangu"
MUENDELEZO
Episode 11 SEASON 2
Moyo uka vibrate kidogo ni kama nimesikia kitu ambacho sikutegemea kukisikia ila nikahisi kama nategwa kidizaini flani, mdomo ukawa mzito sijui nimruhusu au nimjibu kitu gani, alivyoona nimekuwa mzito kuongea akaendelea kuongea
Caryn: "Nipo Serious BM, mtu yeyote anayenijua vizuri analijua hili swala hata ukimuuliza Michelle"
BM: "Sawa hamna shida, mimi naweza kulala hata hapa chini kwenye Zuria"
Caryn: "Hapana, tunalala wote kitandani, ila nakuomba ukilala assume kama vile umelala na Mama yako mzazi sipo hapa kwaajili ya kukutega maana Akili za Wanaume nazijua"
BM: "Ivi upo serious kabisa kwamba huwezi kulala chumba Cha peke yako unataka tulale wote humu tena kitanda kimoja?"
Caryn: "Kwani kuna ubaya?...naomba nenda kule room kwangu kanichukulie Handbag yangu kuna sabuni nataka nikaoge"
Nikatoka kuelekea kwa room yake kumchukulia Handbag yake huku kichwani nikijiuliza maswali ya kutosha, kwamba huyu mtu kama ni kweli hawezagi kulala mwenyewe ugenini kwanini wakati tunalipia vyumba aliruhusu nilipie vyumba viwili badala ya kimoja?
Sikupata jibu la hilo swali nikahisi tu kuna kamchezo nachezewa, nilihisi Kimasihara imejileta yani stori ndani ya story kwamba hapa hapa ninaweza kupata Cha kuchangia kwenye Uzi wa Tunda na Masihara yake na Bado nikapata Content ya kunogesha Uzi huu wa kijana wa Buguruni
Kwa muda mfupi kichwa kiliwaza mambo mengi sana hicho ni kichwa Cha juu sasa, kichwa Cha chini nacho kilikuwa kimeshapata Notification kwamba muda wowote kuanzia sasa kunaweza kukanuka so be Attention
Lakini pia nikakumbuka wadau wa hapa hapa Jamii forum kwenye huu Uzi Season 1 kule episode ya mwisho kuna wadau walishauri kwamba nifanye yote lakini nisioneshe urijali kwa Caryn
Nikaona hapa nikiendelea kuwaza nini Cha kufanya sitopata jibu Cha msingi acha niache Universe iamue, nikachukua Handbag nikarudi kule room kwangu ambako nimemuacha Caryn
Caryn akatoa Sabuni akaingia bafuni kuoga, alivyomaliza akatoka akiwa ameshavaa Night dress akanikuta nimekaa kwenye kochi naangalia Tv
Caryn: "Hee! ndio kwanza unaangalia Tv? nikajua nitakukuta upo kitandani"
BM: "Kitandani? kwanini?"
Caryn: "Mizunguko yote Ile hujachoka tu? usie lala mapema, ivi kesho ndio imebaki Document moja eeh?"
BM: "Yeah, nataka ni-fight by saa 4 Asubuhi tuwe tumeondoka"
Caryn: "Kwahiyo kesho tunatoka hapa saa ngapi?"
BM: "Mapema tu kwenye saa 1 ivi, ili saa mbili itukutie maofisini....Sasa Cha kufanya wewe itabidi ukadili na mizigo tuliyoitoa Jana ipakiwe kwenye Boti huku mimi nikiendelea kutoa ambayo imebaki Airport"
Caryn: "Guinness Book itabidi waiandike hii, Mfanyakazi anampangia Boss Majukumu"
BM: "Madam, U Boss uliuacha pale Opposite na Rotana, umevuka Maji huu ni Utawala mwingine mbaya zaidi upo kwenye himaya yangu yani chumba changu"
Mazungumzo yalibase sasa katika mzaha japo nilikuwa namaanisha nilichokiongea, Caryn akavuta shuka mimi nikaganda kwenye Tv kama lisaa lizima
Ukiniuliza kwenye Tv nikikuwa naangalia Program gani najua basi nilikuwa nazuga kuusoma mchezo,
Kikubwa moyoni nilikuwa najiambia kwamba kama vitu vitatokea niache vitokee Automatically nisi force kwasababu huwezi jua inawezekana ni mtego sasa nikijimix nikaleta habari za kupapasana nitakuwa nimelichuma janga
Niseme usiku ulipita salama kabisa, huu usiku sitokuja kuusahau maana haijawahi kutokea katika maisha yangu, Asubuhi yake tuliamka fresh ila mimi ndio nilimuamsha Caryn, nilimuamsha mimi nikiwa nishapiga Maji na yeye akajiandaa tukatoka
Tukajigawa, Caryn alienda Bandarini kuweka kila kitu sawa mimi nikashughulika na Document chap then nikaenda Airport nikautoa mzigo chap kwa haraka sababu haukuwa mzigo mkubwa
Hatimaye tukavuka maji kurudi Dar es salaam, tukafika Bandari ya Dar tuka clear kila kitu tukaupeleka mzigo Ofisini, Kazi yangu ikawa imeishia hapo, nikampatia Storekeeper Parking list ya mizigo ya BATCH hii iliyoingia siku hiyo
Tulivyofikisha mzigo Caryn alienda Ofisini kwake moja kwa moja, muda huo ilikuwa kitu kama saa nane flani mchana nikawa najishauri kwenda kumuomba ruksa, Unajua kipindi kile Cha Utawala wa Bi Mkubwa nilikuwa nikifikisha mzigo tu nilikuwa nasepa zangu, Lakini si kwa huyu Binti ila nilijua kwa leo nitakubaliwa
Kweli nilivyoenda kumuomba akakubali ila yeye alisema atabaki hadi jioni japokuwa amechoka, Mimi nikajikataa nikaingia mtaani,
Siku zikapita wiki zikasonga nakumbuka ilikuwa November tarehe za katikati nikaja kupata nyumba maeneo flani kali sana zile nyumba ni vi Apartments flani hivi vipo sita zote zipo kwenye fence moja na kila nyumba ina vyumba viwili kimoja master halafu choo Cha ku share jiko na sitting room
Ile nyumba nilivyooneshwa tu nikalipia siku hiyo hiyo likabaki swala la kuhama tu, nilikaa kama wiki moja tangu nilipie rent ndio nikahamia kwenye makazi mapya
Kwenye makazi mapya nilihamia na kila Kitu changu kasoro Tv, Muziki na Makochi nilibadilisha, vitu vikakaa Mahali pake kasoro chumba Cha pili kilikosa kitanda maana mwanzo nilikokuwa nakaa ilikuwa One Bedroom nilikohamia ni Two Bedrooms so Budget haikuwa upande wangu kuniwezesha kununua kitanda kingine kwa muda huo
Nikajipa time ila Mpango ni kwamba nikishanunua kitanda nimchukue yule kijana wa mmoja wa Buguruni nikae nae maana nikisema nikae nao wote itakuwa uongo sababu wale wengine ni madogo sana kujihudumia vitu vingi hawawezi na mimi kazi yangu ni ya kusafiri safiri
Weekend ya kwanza nikiwa makao mapya nikapanga kwenda kwa Mzee maana nikitambo sijaenda na sijawahi kukaa muda mrefu kiasi hiki, Unajua tangu Ile safari ya Zanzibar niliyoenda na Caryn sijaenda kwao, ni karibia wiki 3 au mwezi + kama sikosei
Nakumbuka ilikuwa ni jumapili ya tarehe 13 November hii siku pia nakumbuka nilipost muendelezo wa story ambayo ilikuwa Episode ya pili SEASON 2
Basi mimi huyo mdogo mdogo hadi mjengoni kwa Mzee, Wakati naenda niliwasiliana na Mzee akaniambia anatoka mara moja na Bi Mkubwa so niende tu nitawakuta wakina Michelle
Basi nikafika Getini pale nikapita bila kupingwa mlinzi ni yule yule ananijua, Mlango wa nyumba akanifungulia Michelle
Michelle: "Wow! finally, it's been a while"
BM: "Sijakuzoea hivi sister Michelle"
Michelle: "Aje?"
BM: "Si hivyo vizungu mingi, Yai muachie Caryn mjukuu wa Malkia, kwanza yupo?"
Michelle: "Yeah, Boss wako yupo Upstairs "
BM: "U Boss kazini huko, yani Basi tu sina uwezo ila huyu ndugu yako huyu"
Michelle: "Kafanya nini tena jamani, mtu na rafiki yake mshatibuana"
BM: "Urafiki gani wa kukaziana kwenye kila kitu"
Michelle: "Kakufanyaje kwani?"
Nikaanza kumuelezea Michelle....turudi nyuma kidogo ili muelewe vizuri kitu alichonikwaza
Iko hivi mimi huwa naagiza mzigo China Accessories za magari na vitu vingine vya aina mbalimbali vikifika Bongo huwa nafanya Biashara
Baadhi ya vitu vyenyewe ni kama;
Electric toothbrush
Men USB chest bag
Tire Pressure Gauge
Body Renovate
Headlight repair
Car wheel hub reflecting
Crown Car driver license bag
Car air outlet perfume
Creative 3D glass craft metal keychain
Smart Car air compressor
Car Jump starter power bank
Air conditioner vent blinds
Phone holder wall Moun
Sasa mzigo ukatua Bongo, na mzigo wangu mimi ukifika huwa haupimwi kilo, utapimwa kilo ukiwa Bado upo china ndio unataka kupandishwa ndege, ila mizigo mingine inapimwa china na ikifika ofisini inapimwa tena ku confirm Kgs
Mzigo wangu huwa haupimwi mara mbili kwasababu siulipii, yani transport mimi ni Free of charge (hizo ni enzi za Mama Sasa)
Nikachukua mzigo wangu nikapita ofisini kwake ili nimuazime gari yake niukimbize mzigo maskani chapu
BM: "Boss lady nisaidie nafunguo nikimbie nyumbani mara moja, Leo sitakuchelewesha"
(Maana kuna siku nilichukua gari nikamchelewesha kama lisaa akanisusia gari nikaenda nalo nyumbani)
Caryn: "Yani uende nyumbani halafu urudi, sijakuelewa"
BM: "Yeah, naupeleka huu mzigo mara moja then narudi faster"
Caryn: "Aah! utanichelewesha BM, Leo request tu, huo mzigo ni wa nani kwani?"
BM: "Si wa kwangu naupeleka nyumbani, maana nikisema nisubiri jioni nipande nao. Daladala itakuwa uongo halafu mambo ya ku-request mimi sifagilii"
Caryn: "Ooh, so huo mzigo ni wa kwako...umelipiwa?"
BM: "Kulipia nini tena? Mzigo nimekuambia ni wangu"
Caryn: "Sawa sijakataa ni wa kwako, ndio nauliza umelipiwa?"
BM: "Okay haujalipiwa"
Caryn: "Sasa unaondokaje na mzigo wakati haujalipiwa, ebu nione Delivery note uliyoandikiwa"
BM: "Sina Delivery note"
Akanyanyua simu akampigia Storekeeper halafu akaitwa na Accountant, wakaja mule ofisini tukawa watu wa tatu yani mimi, Accountant, Storekeeper pamoja na Caryn akiwa wa nne
Caryn: "Accountant naomba nioneshe malipo ya ule mzigo pale mlangoni iwe ni Cash au Bank transfer, na Storekeeper nioneshe Delivery note ya huo mzigo"
Kwakifupi kwasababu mzigo sijulipia wote wawili Accountant na Storekeeper walikuwa hawana hivyo walivyoambiwa waoneshe
Delivery note ni karatasi ambayo inathibitisha kwamba mzigo ulikifa kwa mwenyewe huku ikionesha kiasi alicholipia pamoja na kilo za mzigo....Ila Accountant akajibu bila kupepesa macho
Accountant: "Ule mzigo haujalipiwa so sina pesa yake"
Caryn: "Kwanini haujalipiwa?
Accountant: "Mizigo ya BM huwa hailipiwi"
Caryn: "Kwanini isilipiwe, give me one and strong single reason kwanini mizigo yake hailipiwi"
Accountant: "Right question to the wrong person, Nadhani hili swali ungemuuliza aliyekuwa incharge wa hii Kampuni au muulize mwenyewe BM"
Caryn: "Okay, tufanye hailipii, wewe kijana naomba nioneshe Delivery note ya kuonesha kwamba BM amepokea mzigo wake"
Storekeeper: "Delivery note sijamuandikia kwasababu mzigo haujafanyiwa malipo"
Caryn: "Na mwenyewe unahisi upo sahihi kabisa kufanya hivyo, akikukana je kwamba hajachukua mzig"
Caryn: "Hawa wawili watakufanya uingie kwenye kosa, kama wanapeana mzigo bila ya kulipia wewe ulitakiwa kuuandikia Delivery note kuthibitisha kwamba mzigo umefika kwa muhusika"
Caryn: "Kaendeleeni na shughuli zenu, ila we naomba uniletee kitabu cha Delivery note"
Storekeeper akaambiwa alete kitabu cha Delivery note Accountant nae akaondoka nikabaki na Caryn, alivyoletewa kile kitabu cha Delivery note akamuambia Storekeeper akaupime ule mzigo wangu kwenye mzani
Kilo zikasoma 29 (29 KGs) Caryn akapiga hesabu ya dollar 12.5 kwa kila kilo, ikaja 833,730 kama hanijui Caryn akaniambia nitoe hiyo pesa ndio mzigo utoke
Nilimuangalia Caryn kama Dakika nzima hivi simmalizi, yeye ndio kwanza yupo busy na laptop
Caryn: "Aisee kama haulipii huu mzigo sema ili urudishwe stoo"
BM: "Urudishwe tu sina pesa sasa hivi ya kulipia mzigo"
Caryn: "Okay but huu mzigo usikae zaidi ya siku Saba huko stoo, ukipitisha ziku Saba za free utachajiwa gharama za stoo vile vile"
Turudi Leo sasa huku kwa Michelle
Michelle: "Unajua sio wewe tu, hata mimi mwenyewe niliagiza nywele akanilipisha, so ndivyo alivyo ni kumzoea tu"
BM: "Sawa sijakataa kulipia lakini usinicharge kama customers wengine, mimi natakiwa kufanyiwa favor, hata wewe pia"
Michelle: "Aahwe! Caryn anifanyie favor mimi? wewe ndio wa kufanyiwa favor, wewe ndiye bwana ake mshakuwa mwili mmoja sasa"
(Mapigo ya moyo yakajilesi nimesikia nilichosikia au ni masikio yangu tu)
BM: "Tushakuwa mwili mmoja? sijakuelewa una maanisha nini? au sijakusikia vizuri?"
Michelle: "Ebu niambie ukweli, wewe na Caryn ni wapenzi? isije ikawa umenihadithia hii story yako ya kulipishwa mzigo ili tu unipange ki saikolojia"
BM: "Aah jamani hatujafikia huko, Ukiachana na urafiki, mimi na Caryn ni mtu na Boss wake"
Michelle: "Ooh! Eti eeh, mtu na Boss wake wanawezaje kulala room moja"
Unajua nilipatwa na mshangao, hii Habari nyeti kama hii nani kavujisha? nilijiuliza lakini nikajua tu huyu atakuwa tu ni Caryn, sasa kama ni yeye kwanini amefanya hivyo akiwa na nia gani haswa?
Wakati naendelea kujiuliza Mzee pamoja na Mama wakawa wamerudi, Mzee akamuulizia Caryn akaambiwa yupo Chumbani kwake na muda wote huo tunapiga Story na Michelle Caryn hakutoka nje
Mzee: "Ebu kaniitie nina mazungumzo na nyie wote watatu"
Michelle akaenda kumuita Caryn, nikabaki na Mzee, nikicheki sura ya Mzee silioni tabasamu kabisa kitu kilichonishangaza zaidi nilimuona anatoa sigara kwenye mfuko wa koti halafu akatoka nje
Unajua tangu nimjue Mzee leo ndio namuona na sigara, nilikuwa sijui kama ni mvutaji, Michelle akarudi akiwa pamoja na Caryn
Michelle: "Huyu Mzee kaenda wapi tena?"
BM: "Kumbe Mzee huwa anavutaga sigara?"
Caryn na Michelle wakaangaliana kama vile kuna kitu wanahisi"
Caryn: "Something went wrong"
Michelle: "Yeah, ukimuona Mzee anaanza kupuliza hayo madude ujue kuna kitu"
Basi kila mtu akawa anahisi jambo lake lakini hakuna ambaye alikuwa anajua ni kitu gani hasa Mzee anataka kukiongea, Mzee akarudi kutoka Smoking zone
Na hii siku ndio nilijua kwamba hii nyumba huwa na smoking zone, Caryn anadai Mwaka unaweza kupita Mzee hajaenda smoking zone
Mzee akarudi akakaa kimya kama Dakika 2 hivi huku akiwa anachezea simu, ni kama alikuwa anajibu jumbe kwenye simu yake
Mzee: "Umefanya vizuri BM kuja leo, maana nilikuwa nafikiria kukutafuta, vipi maendeleo lakini?"
BM: "Mungu mkubwa maendeleo si mabaya"
Mzee: "Vizuri kusikia hivyo"
Mzee: "Unajua BM pamoja na Binti zangu hapa nyie Bado ni vijana wadogo, na katika umri wenu huo mdogo mmepata bahati ya kuongoza Kampuni kubwa mnazofanyia kazi"
Mzee; "Ni ngumu sana kukuta Kampuni ambayo inaendeshwa na kijana inapata maendeleo mazuri kwasababu vijana wana mambo mengi sana, vichwa vyenu vinakuwa havijatulia lakini nilichukua maamuzi magumu nikawapa hiyo dhamana"
Mzee; "Unajua hakuna kitu kibaya kama kuchanganya Mapenzi na kazi...."
Caryn akakohoa, Michelle akajinyoosha kama anataka kukaa vizuri, Mimi sikutikisa hata mguu, niseme tu kwamba KUMEKUCHA
Itaendelea