Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Ilipoishia

BM: "Kwahiyo kama shida yangu ni Binafsi hunisikilizi sio?"

Caryn: "You should understand that I'm very busy na Mama leo hayupo, so if what you have come here to discuss has absolutely nothing to do with business, then I suggest you turn around and walk away or better still wait until office hours are over"

Muendelezo

SEASON 2 Episode 6

Hayo maneno Caryn ameongea huku ananiangalia usoni halafu hacheki wala hatabasamu, yani nimemuona Caryn mwingine kabisa tofauti na yule niliyemzoea, kumbe huyu mtu akiwa mazingira ya Kazi ndio anakuwa hivi?

Moyoni nikajisemea hapa haina hata haja ya kulazimisha, sababu naweza kumlazimisha kunisikiliza halafu msaada wenyewe akagoma kuutoa,

Basi nikamuaga nikamuambia acha Mimi nikusubiri nje hadi jioni ukishamaliza kazi zako tutaongea, Akanijibu kwa ishara ya dole gumba akimaanisha sawa

Nikatoka nje ilikuwa saa nne nikatafuta kwanza chai na bahasha yangu ya kaki mkononi, nilivyomaliza shida ya tumbo nikarudi yale maeneo ya ofisini kwa kina Caryn karibu na pale kuna shoe shine nikaenda kukaa hapo,

nilikuwa nausikiaga ule msemo wa 'kuchoma mahindi' hii siku sasa mimi nilijua kuchoma mahindi hadi wadau wa pale wakaanza kuniuliza "Ebhana vipi kuna mtu unamsubiri?" Shoeshiner ndio aliuliza, nikamjibu "ndio" nikamuelekeza Ofisi, viatu vyangu havikua vichafu kihivyo lakini ilibidi nimpe anisafishie ili kusupport ofisini

Kwenye hiki kijiwe kulikuwa na mastory ya town ambayo mengi ni Chai sijapata kuona jamani ila zilinisogezea masaa sikuboeka, Asubuhi nilipiga chai nzito kidogo hivyo mchana sikuona haja ya kwenda kula

Kwenye saa tisa kasoro Alasiri flani ivi naona Jeep lina reverse nikamuwahi kuniona eti akashangaa

Caryn: "BM! Usinambie tangu asubuhi ulikuwa hapa?"

BM: "Hii shida niliyokuwa nayo hata kama ungekuwa wewe, bado ungekuwa hapa"

Caryn: "Ni shida gani hiyo? Ebu ingia kwenye gari tuongee"

Nikaingia kwenye gari nikamuelezea shida yangu akakubali ila tatizo Passport size akawa hana

Caryn: "Nyumbani zitakuwepo kama hazitakuwa kesho nitapiga, but are you sure unataka kuwa taxi driver?"

BM: "Ndio, kwani kuna ubaya"

Caryn: "Hakuna ubaya ila kuna uzembe, kutoka kuwa logistics manager hadi tax driver! tena gari yenyewe sio ya kwako"

BM: "Sasa unataka nifanyaje? ebu nambie"

Caryn: "Do whatever it takes to survive"

Tulivyofika Fire nikashuka, akaelekea Sinza mm nikaenda Kariakoo kuwaongezea wale madogo nguo za kushindia maana niliwanunuliaga ila chache sana hazifiki hapa pairs 4,

Uliza hiyo Pesa ya kununua nguo nimeitoa wapi kipindi hiki ambacho pesa ya kula inataka kunipiga chenga

Saa zile namuelezea Caryn shida yangu ya kutaka awe mdhamini wangu kwenye mchongo wa Udereva Bolt,

Nikamuona kama kaingia huruma ivi akafungua ka storage ya gari akatoa noti za elfu tano tano zikiwa laki 5 akanipa akanambia "Achana na hiyo kazi unayotaka kufanya kama ni pesa ya kula nitakupa hadi pale utakapopata kazi ya maana"

Alivyosema hivyo cha kwanza pesa nilizipokea sijaziacha halafu nikamwambia nisaidie jambo langu nililokuomba halafu hayo mengine yabaki kama hiari tu,

Basi nikapita Kariakoo nikaenda hadi karume nikachukua mitumba kadhaa nikafanya na shopping ya vitu vya jikoni nikanyoosha goti hadi Yombo,

Madogo niliwakuta wanaendelea vizuri ila muda nilioenda Kaka yao alikuwa Bado hajarudi, stress iliyobaki nikuwapeleka hawa watoto wawili shule kitu ambacho naona kitachukua muda kukifanikisha, nikasubiri nile na msosi kabisa nikiondoka ni kwenda kulala tu

Jioni kwenye saa 1 kasoro nikarudi zangu home, nikamcheki Caryn kujua ratiba yake ya kesho yasijekutokea kama yaliyotokea leo,

Bahati nzuri passport picha alikuwa nazo so tukapanga Asubuhi mapema tuonane, kesho yake nikachukua picha nikaelekea kwa jamaa ilikuwa majira ya saa 5 asubuhi nimebeba nyaraka zote

Jamaa akafika na mkataba nikamtolea barua kutoka kwa mwenyekiti na mdhamini wangu, Sasa hapa kwa mdhamini kukawa na utata, kumbe huyu jamaa anamjua Caryn, kwasababu nilivyotoa passport photo ya Caryn jamaa akashtuka halafu akanipiga jicho la wizi akaniuliza

Jamaa: "Huyu mtu una mahusiano naye gani?"

BM: "Si nimeandika hapo My Sister"

Jamaa: "Mbona sijawahi kujua kama wana kaka ambaye ni wewe"

BM: "Kwani we unamjua Caryn?"

Jamaa: "Namfahamu kupitia Dada yake, Michelle alinitambulisha hata kabla sijamuona ila hajawahi kunambia kama ana Kaka"

BM: "Sio lazima kukutambulisha ndugu zake wote kwani wewe ni nani ake?"

Jamaa: "Ina maana Michelle hajakuambia Mimi ni nani kwake?"

BM: "Aliniambia tu ni rafiki yake"

Jamaa: "Tuachane na hayo, huyu anayekudhamini anajua kama anakudhamini kwangu?"

BM: "Ndio anajua, Sasa atatoaje picha na details pasipo kujua zinatumika wapi?"

Jamaa akawa kimya kwa sekunde kadhaa halafu akanambia "Basi sawa ila utasubiri kidogo gari lina marekebisho kidogo ya kuyaweka sawa, likikaa sawa nitakushtua"

Nikahisi kama jamaa ananikataa kimtindo ila hataki kunyoosha maelezo, nilijua kama kanikataa kwasababu kanirudishia Barua zile ikiwemo Ile ya utambulisho na passport picha ya Caryn

Na Mimi nikajikataa, nikamjulisha Michelle akanambia niende home, saa hiyo ishafika mchana nikafika kwa Mzee, nikamuelezea kwanza kila kitu Michelle halafu nikamuuliza

BM: "Kwani yule jamaa ni nani? mbona kama anakujua sana"

Michelle: "Ndiye Mr mwenyewe ila usijali amenielezea kila kitu, kuna kitu kidogo tu ndio kimekuharibia"

BM: "Kitu gani?"

Michelle: "Umepeleka picha ya Caryn mbaya zaidi ukasema ndiye mdhamini wako"

BM: "Sasa hapo shida ipo wapi?"

Michelle: "Caryn na yule mtu haziivi, si nilishawahi kupa story yake, kuna kitu amehisi labda, mbaya zaidi na wewe hukunambia kama unamuhusisha Caryn katika hili"

Sasa ndio nikapata picha kamili, kumbe yule jamaa kamuhofia Caryn ndio maana akawa ananihoji hoji.

BM: "Mimi sikujua, tatizo na wewe hukunambia ukweli toka mwanzo kama ndio Shemeji mwenyewe.

Mchongo ukayeyuka kama masihara vile kwaajili ya Caryn tu, basi nikarudi zangu mtaani,

Maisha yamechange ghafla yani sasa hivi sina ratiba, sina pa kwenda, sina Cha kufanya wakati juzi juzi tu hapa nilikuwa naona uvivu kwenda kazi Leo naitafuta kwa udi na uvumba

Wakati nimerudi nyumbani nakumbuka hii siku niliongea sana na Annie kupitia simu ambapo jana yake ndio alipokea mshahara wake wa kwanza,

Akataka kunitumia Pesa nikamkatalia sasa kwasababu yeye anajua nipo kazini hata hakunilazimisha sana akajua pesa ninayo ya kutosha kumbe mwenzie napumulia Mashine

Zikapita kama siku 2, Caryn akanicheki asubuhi nakumbuka hii siku niliamkia kwa sister

Caryn: [emoji338]"Mambo"

BM: "Safi, vipi"

Caryn: "Upo wewe, upo kimya sana"

BM: "Nipo tu"

Caryn: "Upo wapi?"

BM: "Nipo kwangu"

Caryn: "Sawa basi, nikitoka shop nitapitia"

Nikamuitikia lakini kama sijamuelewa, Yani anapitia nyumbani kwangu au anapitia tu Tabata ana mishe zake?

Basi nikapiga chai kabisa kwa sister then nikawaaga nikaenda Manzese kule anapoenda Dogo kujifunza maana Wakati anatoka nilikuwa bado nimelala so nimeenda kuhakikisha kama kweli kijana huwa anahudhuria class au ana mambo yake

Kijana nilimkuta pamoja na wenzake ila Boss wao sikumkuta, kijana maendeleo yake si mabaya nilivyojihakikishia hilo nikaondoka zangu nikaenda home

Mida ya jioni nilikuwa kijiwe flani cha Car Wash maeneo ya nyumbani Caryn akanicheki kunijulisha kwamba ndio ameingia njia ya Tabata,

Mimi Nikatoka pale kijiweni nikaenda mjengoni kuangalia kama mazingira yapo sawa, nikapaweka fresh kila kitu kikawa katika mazingira yake

Kwa upande wa jikoni kidogo kulikuwa kunasikitisha ukitoa Mchele hakuna kila Kitu, fridge ndio nimelizima kabisa, basi ukapita muda kidogo Caryn akanipigia simu kwamba amefika yupo nje,

Ivi mnajua kama Caryn nilishawahi kuja nae hapa ila hakuingia ndani aliishia nje (sijui nilikihadithia hiki kipande)

So alipakumbuka nilivyotoka nje nikamkuta but this time around kaja na li-Alphard hadi nikamaindi, nikamfungulia geti akalipark

BM: "Kwahiyo umeona Alphard ndio gari ya kuja nayo mtaani kwangu sio"

Caryn: "Kwanini unasema hivyo?"

BM: "Hii gari huwa hauiendeshagi ila kwasababu umejua unakuja Tabata ukasema uje nalo"

Caryn: "Jeep linatakiwa kwenda kufanyiwa Service nimeliacha nyumbani"

BM: "Haya Dada ingia na Noah yako iliyochangamka"

Caryn: "Acha kuongea sh*t kwa kitu ambacho huwezi kuki afford, ebu nikaribishe ndani mlango wako ni upi?"

BM: "Ni huku Madam"

Tukaingia ndani, kitendo Cha kuingia ndani Caryn Hata kabla hajakaa akaanza kuithaminisha nyumba

Caryn: "BM kumbe una kaa One bedroom House, sasa Leo nikisema nataka kulala huku itakuaje"

BM: "Si una lala tu, tatizo lipo wapi?"

Caryn: "Halafu na wewe utalala wapi?

BM: "Si hapa Sebuleni, wewe utalala chumbani"

Caryn: "Hapana, hauna hata kochi la three seater ukilala hapa kwa two seater si utajikunja sana, I was joking by the way mm siwezi kulala huku"

Nikajua amepadharau na mimi nikamwambia "Hata Mimi najua huwezi kulala nyumba za watu masikini"

Caryn: "Sijamaanisha hivyo unavyofikiria, muda mfupi nimeingia humu nimegundua hapa unaishi na Mwanamke, au kama huishi nae basi huwa anakuja mara kwa mara haya hebu nambie nikilala hapa halafu wifi yangu akaja kwa kushtukiza atakuelewa kweli?"

BM: "Mimi siishi na Mwanamke hapa, kitu gani kimekufanya uhisi hivyo"

Caryn: "Unajua kwasasa hutakiwi kunificha kitu, na ivi unajua kwanini nimekuja kwako"

BM: "Basi tufanye yameisha"

Ila Bado najiuliza huyu kajuaje kama nilikuwa naishi na Mwanamke, basi nikamkaribisha kwa mara nyingine

BM: "Vipi nikakuchukulie Maji au Soda?"

Caryn: "Achana na hivyo vitu, kaa hapo tuongee"

BM: "Sawa, nakusikiliza"

Caryn: "Unajua sikudhania kama utakuja kunikwaza kwa kiasi kikubwa namna hii umenikwaza mno, kitendo Ulichokifanya kimenikera kupitiliza ila huwezi jua kwasababu najitahidi kucontrol hisia zangu"

Kumekucha, sijui imekuaje tena, huyu mtu hadi kanifuata nilipo kweli nimeyatimba tena sio kidogo

Itaendelea
 
Tumeishia hapa
 
Back
Top Bottom