Mtanzania Mnyonge22
Senior Member
- Sep 2, 2022
- 125
- 455
MuendeleZo Lini?Dah! we acha tu, kama ulikuwepo vile
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MuendeleZo Lini?Dah! we acha tu, kama ulikuwepo vile
MwakaniMuendeleZo Lini?
Ilipoishia
Mama Accnt: "Tatizo ni kwamba mwenzako hajui kuongea na TRA kabisa, na hajui kubagain, kabla sijakuachia majukumu yangu itabidi uendelee kwenda nae trips kadhaa hadi atakapokuwa sawa"
BM: "Ni sawa, lakini Mama unajua Mimi nimekuja kukuaga, nimeona nikafanye majukumu mengine kwahiyo nilikuwa naomba ruksa yako"
Mama huwa anavaa miwani, kusikia hivyo akavua kwanza na mawani yenyewe, kuna vitu alikuwa anaandika akaacha akaweka peni chini yani ni kama vile hakutarajia kusikia nilichomuambia
Muendelezo
SEASON 2 Episode 5
Mama Accnt: "Mbona sikuelewi, kuna tatizo kwani?"
BM: "Hamna tatizo lolote Mama, ni kutafuta uelekeo mwingine wa maisha"
Mama Accnt: "Una uhakika kila kitu kipo sawa? maana hiki unachoniambia ulipaswa unipe taarifa Wakati ule unachukua likizo, Kwasasa mm nilikuwa najua umerudi kazini"
BM: "Kila Kitu kipo sawa Mama nilishindwa kuaga Wakati ule kwasababu sikuwa na uhakika na kitu ambacho naenda kukifanya"
Mama Accnt: "Mwanangu unajua tatizo sio wewe kuondoka, shida ni kupata mtu kama wewe, hebu naomba uende hata safari mbili na De*** umuoneshe namna kazi zinazofanywa"
BM: "Sawa, haina shida Mama"
Mama Accnt: "Na kuhusu mwenzako vipi? Mambo yenu yamefikia wapi?"
Hapa Mama ni kama alinote kitu maana baada ya kuuliza hilo swali nilijivuta kidogo kulijibu
BM: "Tushaongea na pia nitaongea nae kabla hata sijaondoka"
Mama Accnt: "Sawa, nakutakia Kila la kheri ila kama mambo hayataenda kama ulivyopanga nafasi yako bado ipo"
Basi nikamalizana na Mama yake Accountant nikashuka chini kuna restaurant nikaenda hapo kupata chai, Wakati naendelea kunywa chai nikamuona Accountant anashuka kwenye Bajaj ikabidi niachane na chai kwanza ili nimuwahi kabla hajaingia ofisini kwa mama yake, nikamuwahi 1st floor nikamsimamisha
BM: "Hizi mbio zote kwani unakimbizwa?"
Accountant: "Nawahi kuwatumia wateja invoice, Mambo lakini"
BM: "Safi, sasa skia...mimi sipandi huko juu tena maana nishamalizana na Mama, hapa nilikuwa nakungoja wewe tu"
Accountant: "Kwani hukua umekuja kazi leo"
BM: "Kama ningekuwa nimeajiriwa kwa kufuata taratibu zote basi ningesema Leo nilikuja kuandika barua ya kuacha Kazi, nimeshamuaga Mama sababu za kuacha Kazi nilizompa ni zakibinafsi sio shinikizo, sasa kwa upande wako kama akikuuliza utajua jinsi utakavyomjibu kama utamueleza ukweli au lah"
Accountant: "This was not the agreement we had why are you sounding so different"
BM: "Unajua nilifikiria mara tatu tatu uamuzi niliokuwa nataka kufanya nikahisi kama badae nitakuja kupata shida, so ni Bora hiyo shida niipate Sasa hivi lakini nikijua nipo katika maamuzi sahihi"
Accountant: "Mimi hata hunipi shida sababu nakujua, tatizo lako wewe huna misimamo, utanifuata tu"
Akapanda zake juu na mimi nikajikataa nikaenda Manzese, pale Manzese nilienda kwaajili ya Kijana wa Buguruni kuna sehemu niliona wanatengeneza Furniture so nikaenda pale kumuombea nafasi ili aongeze ujuzi maana Kijana anadai alishaanzaga kujifunza ila akaishia njani,
Bahati mbaya sikumkuta muhusika, zikapita kama siku mbili tatu nikaenda tena, nilienda majira ya Asubuhi nikakutana na muhusika nikamuelezea hitaji langu yule bro akanielewa, (Posho ilihusika) tena akaniambia ikiwezekana nimpeleke siku hiyo hiyo lakini sikuweza coz siku hii ndio nilikuwa naenda Zanzibar Ile safari Mama Accnt aliyoniomba niende
Tulirudi Jumatano na Sealink 2, tukafanikiwa kusafirisha mzigo nikamuelekeza mwana kila kitu, pia nikamuelekeza namna ya kula na TRA, Yani njia zote nilimfungulia jamaa ila sijaenda Deep sana maana Binadamu hawaeleweki kuku snitch ni Dakika 0 ili mradi tu yeye aonekane Mwema
Basi bana mzigo tukaufikisha Ofisini na mizigo mingine ikapelekwa Direct kwa wateja, Ile mizigo tulioifikisha ofisini ikaanza kupimwa kabla ya kuwekwa store ili kuhakiki Kgs,
Wakati mizigo inaendelea kupimwa Mimi na jamaa nilieenda nae Zanzibar tukaingia Ofisini kwa Mama yake Accountant kupiga mahesabu, tulivyomaliza Mama akanipa Milioni 5 hapo Wakati huo nilikuwa nimebaki Mimi na yeye tu yule jamaa mwingine ameshatoka
Mama baada ya kunipa zile pesa akaniambia "Mwanangu najua unastahili zaidi ya hii japo pia hii sio ndogo, lakini pia najua hapa utarudi tu"
Nikawaka sijamuelewa na hii kauli yake ya "hapa utarudi tu" kwamba huko ninakoenda nitafeli au? Nikaona Bi Mkubwa kama ananiletea pigo za mwanae. Nikamwambia "Mama hizi pesa naomba ukipata nafasi utaniwekea tu kwenye Account yangu
Mama Accnt: "Wala usijali kesho **** (Accountant) akienda bank nitampatia na zako akakuwekee"
Eeh Accountant tena ningejua ningezichukua tu, Nikamuitikia tu Bi Mkubwa maana ningebadili gia angani isingeleta picha nzuri
Nikaagana na Bi Mkubwa, bahati nzuri Wakati natoka pale ofisini Accountant Bado alikuwa store na Mimi nikatoka kama sikuwepo sikutaka mambo mengi, straight nikaenda nyumbani nilikuwa na usingizi debe maana huko kwenye meli hata sikulala vizuri
Zikapita kama siku mbili kwani Ile Pesa (Milioni 5) niliekewa sasa, nikampigia Mama kuulizia Bi Mkubwa akanambia kuwa alishampa Accountant toka jana labda alijisahau so atamkumbusha, Mimi nikajua tu hajasau Wala nini ila Accountant anataka tu kunikomesha
Sasa Dogo kule nilikompeleka Manzese kwenye mafunzo akawa anaendelea vizuri, na mimi wakati huo sina kazi nipo narandaranda tu mjini huku Pesa ikaanza kupiga Alarm kwamba mzigo muda si mrefu utakata so slow down kwa matumizi ambayo hayana ulazima
Zikapita kama wiki mbili kucheki Balance kitu kinasoma laki 2 na 40, hapo kumbuka natumia tu sina ninachoingiza, halafu Cha ajabu yule aliyenishauri niache kazi kwani ana Habari na mimi tena!? ndio kwanza ubusy kwake ndio umezidi kuongezeka hadi nikahisi kama ananikwepa
Jumamosi moja akanicheki mwenyewe sijambeep wala sijamtumia messages akanambia nimkute Mlimani City Samaki Samaki mida ya jioni, nikaapa huyu Leo nikionana nae lazima nimchomoe pesa maana hali inaenda kua tete
Kama kawaida mimi ndio nikawahi kufika, Alivyofika tu nikamuingia na gia ya Rent ya nyumba ya wale madogo
BM: "Caryn wiki hii inayoanza naweza kupata nyumba ya kukaa wale vijana, so nilikuwa naona Bora tungemalizana kabisa"
Nilivyomuambia hivyo akanikata jicho kwa sekunde kadhaa halafu akanambia
Caryn: "Listen to me, I know kwamba huna kazi lakini hii mbinu uliyokuja nayo si sahihi, kama una shida ni Bora ukasema tu nitakuelewa"
BM: "Okay, let me put this way, unakumbuka nilikuambia kwamba wale watoto wanakaa kwa sister na mimi ndio nilikuwa nawahudumia kwa kila kitu maana hali ya Dada angu naijua, so kwa vile Dada angu ndio anakaa nao nilikuwa naomba hiyo Pesa yao ya Kodi unipe ili nimpe sister kwaajili ya matumizi kwasababu naona mzigo unaenda kunishinda"
Caryn: "Sasa kulikuwa kuna haja gani ya kunidanganya?"
BM: "Nilidhani hutanielewa"
Caryn: "Unajua hadi sasa ni mwezi ushaisha unaenda wa pili huu na bado hujanipa feedback yeyote, unajua kama Mzee mwezi ujao tu anarudi tena tarehe za mwanzoni"
BM: "Kuhusu Dogo Biashara atakayokuja kuifanya ni ya Furniture, Uzuri ana idea na hayo mambo na nishamtafutia Mahali pakuongezea ujuzi na anaendelea vizuri tu"
Caryn: "Biashara ya furniture unaijua vizuri wewe? I don't think that Business will pull through in six months timer"
BM: "Caryn hapa sio swala la miezi 6, tunachoangalia ni Biashara kufanya vizuri tu haijalishi itachukua muda gani ila lengo ni kufanikiwa"
Caryn: "Pointless, Unajisikia kweli hicho unachokiongea, Unachokifanya kama hutozingatia muda ni kazi Bure, ni vizuri kujiwekea muda katika kutimiza lengo itakufanya uongeze bidii katika kufanikisha jambo lako"
BM: " Caryn leo I'm not in the mood for your motivational talks, we nambie tu kama pesa napata au sipati"
Caryn: "Nishtulie huyo Dada nyuma yako (muhudumu) tumuagize chakula tule kwanza maongezi badae
Nikamshtua muhudumu na Menyu ikaletwa, Caryn akachagua Kuku Nusu Makange sijui manaita na chips na Juice, muhudumu akahamia upande wangu kunisikiliza nakula nini, nikampiga jicho Caryn akagundua ninachohofia maana alishawahi kunifanyia umafia sehemu kama hii ya maankuli,
Caryn: "You're not the one paying so you don't have to bother"
Nikaagiza chakula kama kile alichoagiza yeye ila mimi nimeitisha kuku nusu ili hata akigoma kama siku zile niwe na uwezo wa kujinasua,
Tunamalizia kula nikampa proposal siunajua tena sasa hivi sina mchongo mjini hapa (Jobless)
Nikamuambia mpango wangu wa kufungua sehemu ya kutengeneza furniture na kuziuza ambapo yule kijana wa Buguruni ndio atakuwa fundi mkuu, Uzuri location nilishaipata shida ni kwamba ninaweza nikachelewa kuilipia halafu mtu akaichukua
Caryn: "So kununua vifaa, materials, na kulipia eneo inaweza gharimu kiasi gani Cha pesa?"
BM: "Milioni 10 tu, kwa hiyo Pesa nitapata vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi pamoja na materials mazuri, sababu nataka kutengeneza vitu unique"
Caryn: "Sasa 10 Millions wewe utaitoa wapi?"
BM: "Si ndio nilikuwa nasema kama inawezekana unikopeshe hiyo Pesa hata tukiandikishiana ni sawa tu"
Caryn: "Sijakuelewa! kwamba hiyo milioni 10 unaniomba Mimi au unamaanisha Mzee ndio unataka akupe hiyo Pesa"
BM: "Nakuomba wewe, Achana na Mzee"
Caryn: "I appreciate the fact that you think that i am rich, but I'm sorry to disappoint you"
BM: "Unamaanisha nini?"
Caryn: "Sijafikia hiyo level ya kuombwa milioni 10 ghafla na nikatoa"
BM: "Nilitegemea Support yako kipindi hiki kwasababu unajua wewe ndio. ulinishauri niache kazi"
Caryn: "Utakuja kunielewa badae kwann nilikushauri uache kazi, ila sasa isiwe ndio sababu ya kuniletea shida zako"
Dah! nilikuwa mnyonge asikuambie mtu, hadi nikamkumbuka Mshkaji wangu, unajua nilimsikiliza Caryn nikijua kwamba baada ya kuacha Kazi atanipa mchongo kumbe matarajio yangu yalizidi uhalisia
Niliacha na Caryn nikasema hapa itabidi nimcheki Accountant tu maana yeye ndio ana pesa yangu ya halali, alichonijibu sasa huyo Accountant nilichoka nikasema hapa acha nipige tu kimya nisimcheki Mama yake asije akaona nina dhiki sana ila kiuhalisia dhiki nilikuwa nayo
Nilikuja kupitia kipindi kigumu sana japo ni kwa muda mfupi lakini nilionja joto la jiwe, unajua pesa ilikuwa iliniishia haraka kwasababu nilikuwa nahudumia familia kubwa, Sister yangu ana watoto wawili plus wale madogo watatu Jumla wanakuwa 6, plus sister mwenyewe ni wa saba aisee acheni nyie
Hiki kipindi aliyenisaidia ni Mshkaji wangu wa Kinondoni japo alinisaidia huku ananisema, na kumbuka kipindi chote hicho nawasiliana na Annie Lakini hajui kinachoendekea sijamuambia kama niliacha kazi
Mwezi August kwenye tarehe 20+ kama Nakumbuka vizuri nilimfuata Michelle, nilijua Michelle hana Channel kama Caryn lakini nilimfuata hivyo hivyo kumuelezea shida sababu niliamini yeye nimuelewa
Nilivyoonana na Michelle nikamuelezea shida yangu, nilimuambia kwasasa sina mchongo mjini ila sijamuambia sababu halisi iliyonifanya niache kazi
Michelle: "Mzee anajua kama umeacha kazi?"
BM: "Hapana"
Michelle: "Kwanini hujamuambia?"
BM: "Sikuona ulazima huo labda akisharudi"
Michelle: "Umekosea sana, hata hivyo atakuwa ameshapewa taarifa"
BM: "Atakuwa kapewa taarifa na nani? na Caryn au?"
Michelle: "Kwani hadi Caryn pia anajua kama umeacha kazi?"
BM: "Ndio anafahamu muda tu"
Michelle: "Ooh, ila hata kama Caryn angekuwa hana taarifa ya wewe kuacha Kazi still Mzee taarifa yako ingemfikia
Nikawaza kwanini Michelle ananiambia kwamba Baba yake ni lazima anayo taarifa ya Mimi kuacha kazi ila nikaona ni kawaida sababu Mzee na Mama yake Accountant wana kaukaribu fulani ukizingatia Mimi nilikuwa mfanyakazi pendwa wa Mzee kwenye Ile Kampuni kitu ambacho kimenifanya niwe na ukaribu na familia yake
BM: "Sasa Michelle tunafanyaje Dada angu maana hali si hali"
Michelle: "Unajua BM mazingira yako ya kuacha Kazi bado sijayaelewa, Yani umeacha kazi mwenyewe bila kuachishwa then still unauhitaji wa kazi? I don't understand"
BM: "Kweli nina uhitaji na Kazi lakini mazingira ya pale ofisini yananibana nisingeweza kuendelea na Kazi"
Michelle: "Ni kama Kuna vitu unanificha, anyways kwani Caryn hajakuambia chochote kuhusu Ile Kampuni uliyokuwa unafanyia kazi"
BM: "Hapana hajaniambia chochote"
Michelle: "Okay, kwasababu wewe umenificha acha na mimi nipige kimya ila kama kweli unashida na Kazi kwenye Ile Kampuni nafasi yako bado ipo"
BM: "Dah! unajua kama ingekuwa sio wale madogo niliokuja nao hapa Mimi nilikuwa na uwezo wa ku survive muda mrefu bila kazi, kumbe ukiwa jobless halafu una watu wanaokutegemea kwa Kila Kitu stress yake ndio Ina taste namna hii?
Michelle: "Sijazoea kukuona ukiwa mnyonge BM, fanya hivi si ulishapata Driving license?"
BM: "Ndio ninayo"
Michelle: "Sasa Kuna namba nakupa utampigia huyu mtu utamuambia nimeagizwa na Michelle Nadhani anaweza kukusaidia ila kama utakubaliana na aina yenyewe ya Kazi"
BM: "Ni kazi Gani kwani?"
Michelle: "Ni ya Udereva, I mean kuendesha hizi Bolt"
Nilimkubalia ila kichwani nikipiga mahesabu nitakuwa naingiza kiasi gani Cha pesa kwa aina hii ya Kazi? Hizi kazi za vyombo vya moto kupeleka hesabu kwa Boss sijawahi kuzifanya ila kwa situation niliyokuwa nayo nikakomaa nayo tu kiaina
Basi Michelle akanipatia namba nikaisave nilivyorudi nyumbani nikaipiga nikamuelezea kama Michelle alivyoniagiza basi jamaa akaniambia tuonane kesho majira ya mchana
Kweli kesho yake nikaenda kuonana na mshkaji akaanza kunihoji maswali kibao mara Michelle ni nani ako? Huyu jamaa akaniitisha barua ya mwenyekiti yani jamaa akawa kama haniamini amini ivi, mara niwe na wadhamini wawili
Nikamwambia bro mimi mdhamini wangu si tayari unamjua
Bro: Michelle hawezi kuwa mdhamini wako, yeye amekuconnect na Kazi tu, ikitokea ukafanya uhuni wowote unajua Mimi siwezi kumshtaki Michelle
BM: "Yule ndio mdhamini wangu sasa, labda kama unataka niongeze mdhamini wa pili lakini hata hivyo mimi siwezi kufanya uhuni wa aina yeyote ule"
Bro: "Sawa, utaleta passport picha ya mdhamini wa pili namba zake za simu, Address pamoja na barua yako ya utambulisho"
Nikaondoka kumsaka mdhamini wa pili kichwani namuwaza mshkaji wangu wa Kinondoni ndio awe mdhamini wangu wa pili lakini navyomjua yule jamaa atanikatisha tamaa, nikamfikiria mtu mwingine wa karibu Sina zaidi ya Annie au Caryn
Nikamcheki Caryn ilikuwa jioni akanambia yupo na Bi mkubwa wake ndio wanatoka job, nikataka kuonana nae akaniambia kwa Leo haiwezekani sababu anaenda kumdrop Bi Mkubwa halafu anaendelea na safari zake, basi nikaomba appointment kwa kesho akakubali
Kesho yake mapema nikaamkia kwa mwenyekiti Nikapata Barua fresh, kipengele Cha kwanza kimeisha Sasa nikamcheki Caryn akanambia ndio anaelekea town, basi tukapata tukutane huko, Mimi nilivyotoka kwa mwenyekiti nikadaka kidala hadi town, nimefika town nikampigia simu
BM: [emoji338]"Hello"
Caryn: "Nambie"
BM: "Mimi nishafika"
Caryn: "BM nilidhani utaniwahi kabla sijaingia ofisini, sasa hivi nishaanza kazi kutoka itakuwa ngumu"
BM: "Haina haja ya kutoka, si unanielekeza tu mimi nakuja"
Caryn: "Labda nikuulize, shida yako ni ya kiofisi?"
BM: "Sasa ndio tuongelee kwenye simu, shida yangu wewe utaijulia huko tukionana"[emoji3513]
Akanielekeza huko ofisini kwao ambako ndio huwa anaenda na Mama yake, nikafika Nikamuulizia Caryn nikaoneshwa ofisini kwake eti kale kakaniuliza kama nina appointment, Yani Mimi niwe na appointment kuonana na Caryn? Nikamwambia sina ila ujio wangu anafahamu nikaambiwa nisubiri hadi apigiwe simu.
Nikarusiwa kuingia ila kwa muda mfupi niliokaa pale reception nikagundua kwamba baadhi ya staff wanamuogopa Caryn
BM: "Caryn wewe ni wa kunisubirisha Yani Hadi upigiwe simu ya kutoa ruhusa ndio nionane na wewe?"
Caryn: "Huo ndio utaratibu, don't take it personal....kwanza nimefanya heshima kukuruhusu kuingia kwasababu sijajua kama shida yako ni ya kiofisi au Binafsi?"
BM: "Kwahiyo kama shida yangu ni Binafsi hunisikilizi sio?"
Caryn: "You should understand that I'm very busy na Mama leo hayupo, so if what you have come here to discuss has absolutely nothing to do with business, then I suggest you turn around and walk away or better still wait until office hours are over"
Itaendelea
Dah haya maisha yani zinaagizwa European cars tatu kwa mpigo halafu anayeagiza zote anagawaIlipoishia
Nilivyofika ndani Ofisini kwa Mama yake Accountant Cha kwanza akanitolea bahasha yenye pesa
Mama Accnt: "Kwanza pole, najua mzigo wako haukukufikia"
BM: "Asante Mama"
Safari hii sikuleta maringo ya kutaka kuwekewa pesa kwenye account nikazibeba kama zilivyo,
Mama Accnt: "BM kwanini uliamua kuacha Kazi kwasababu za kipuuzi?"
Nikakumbuka muda mfupi Caryn ametoka humu ndani, atakuwa kamuambia nini huyu Mam
Muendelezo
SEASON 2 Episode 8
BM: "Sababu gani za kipuuzi Mama?"
Mama Accnt: "Unajua ulikosea sana ulitakiwa kunieleza ukweli, japo nilihisi kuna kitu hakipo sawa, nimekuja kujua ukweli too late, laiti ningejua huu ukweli kabla ya kile kikao Cha juzi ningefanya Mpango ukarudi lakini tatizo kule ushaongopa"
Kwani nilikuwa hata na Cha kujibu, nimebaki kimya tu nikimsikiliza Bi mkubwa
Kumbe Accountant aliamua kufunguka Kila Kitu kwa Mama yake, kwa mujibu wa mama yake Accountant baada ya kile kikao kule kwa Mzee alivyorudi nyumbani alimfahamisha Mwanaye mtu atakayekuja kumrithi,
Sasa Mama Accnt akawa anamuambia Mwanaye kwamba huyo mtu anayekuja kuchukua hiyo nafasi ni mkorofi hivyo ajue jinsi ya ku behave,
"Mimi mwanzo nilimpendekeza BM kwasababu najua yupo soft kidogo kama mimi so mngeenda sawa lakini huyu anayekuja itabidi mjipange" Mama Accnt alimuambia Mwanaye, ndio Accountant akaamua kufunguka
Tuliongea kwa muda mrefu kidogo hadi Caryn akatuma text ya kunijulisha kuwa ameondoka, basi nikamalizana na Bi Mkubwa tukaagana nikasepa, kidogo stress zikapungua sababu kibunda kipo Cha kutosha,
Nikampigia Caryn alichonijibu sasa, sijui anajikuta nani huyu mtoto We nitafute kesho kwa sasa schedule yangu Iko tight
Sikutia neno nikakata simu nikaenda Bank chap nika uhifadhi mzigo
Ikapita wiki ya kwanza Michelle akanicheki, kumbe nae kapewa kitengo bhana tena yeye alivyopewa tu immediately akaanza kazi
Sasa nilivyofika kwa Michelle baada ya story za hapa na pale akaanza kunipanga
Michelle: "Ila BM najua Ile siku umeongopa japo sijui ukweli ni upi ila umeongopa, and I'm sure Mzee anajua kabisa kama umemuongopea ila ameuchuna tu?"
BM: "Sasa Michelle unadhani mm ningefanyaje"
Michelle: "Inaonekana maelezo uliyoyatoa Caryn ndio amekupa, kuwa makini na yule mtoto Najua hana roho mbaya lakini sio Kila anachokushauri ukifuate"
BM: "Unamuonea Caryn wa watu bure"
Michelle: "Ila usijali kama mambo yataendelea kuwa magumu nipatie mwezi mmoja nitajua nitakuweka wapi hapa ofisini"
BM: "Katika yote tumeongea hili ndilo la msingi, lakini Baba yako ataona na Dankidanki tu kwenye makampuni yake"
Michelle: "Kuhusu Mzee we usijali, akinigomea mm nitamuambia Caryn aongee nae, mbele ya Caryn najua hawezi goma"
BM: "Basi sawa, Wacha tuone vile itakuwa ila hii office yako ina mambo mengi sana tofauti na ile "
Michelle: "Mambo gani tena?"
BM: "Si kama hivyo umeniambia badae unaenda kwenye kikao Cha Board sijui Kuna mambo ya representation, kule hakuna haya mambo labda hivi vikao vya kawaida tu tena ni mwezi hadi mwezi tena vikao vyenyewe vinawahusu sana watu wa sales"
Kwenye Conversation nimetumia neno "Kule" nikimaanisha nilipokuwa nafanya kazi, (kwa Mama Accnt)
Anyway Ila Ofisi anayosimamia Michelle kidogo ina watu wazima nahisi ndio maana Mzee kamuweka Michelle huku, maana unaweza ukawa smart katika kuongoza Kampuni lakini umri ukakuangusha na Nadhani ndicho kilichomfanya Caryn awe Disqualify
Siku zikaenda, Nakumbuka ilikuwa wiki moja kabla kufika October ili Caryn aanze kazi rasmi Mzee akanipigia simu na hapo sijawasiliana na Caryn karibia wiki mbili
Mzee: [emoji338]"Hujambo Kijana wangu"
BM: "Sijambo Mzee Shikamoo"
Mzee: "Marhaba, hatuonani siku hizi"
BM: "Nipo Mzee ni majukumu tu ya hapa na pale"
Mzee: "Naelewa, ivi ulichukuaga Driving lisence?
BM: "Ndio Mzee Niko nayo"
Mzee: "Sasa kesho mtawasiliana na yule Dereva wangu kuna magari mtaenda kuyachukua mtayaleta nyumbani"
BM: "Sawa Mzee haina shida" [emoji3513]
Ilivyofika kesho yake kweli jamaa akanicheki tukakutana Mnazi Mmoja jamaa alikuja na mshkaji mwingine hata sijawahi kumuona,
Basi tukaenda hadi sehemu husika tukakabidhiwa Gari, Wakati yule Dereva anakabidhiwa funguo (zilikuwa funguo za gari 3) ndio nikajua aina ya magari tuliokuja kuyachukua kasoro funguo moja tu ndio sijaona logo
Funguo moja logo yake ilikuwa VW, yani Volkswagen na nyingine ilikuwa ya BMW, funguo ya 3 kama nilivyosema sikuona logo yake, tukaenda zilipopaki vyuma, jamani vyuma vyuma kweli na zile funguo za gari mbili nilipatia, Alikuwepo BMW X3 na Ile Volkswagen ilikuwa ni Touareg
Gari ya tatu kumbe Ilikuwa ni Audi tena ni Audi Q3 mawazo yangu yalikuwa tofauti kabisa, niliwaza kwenye ma Prado TX, ma Land cruiser V8
Gari ziko 3 na madereva tuko watatu, kiukweli katika Gari zote nilitamani kuendesha Volkswagen kwasababu ndio ilikuwa gari ya maana kuliko zote halafu kingine ni kutaka kupata experience sababu sijawahi kuiendesha zaidi ya VW Tiguan japokuwa brand ya Audi sijawahi kuigusa gari yake hata moja, BMW nimegusa ila sio X3, kwa kifupi ni kwamba siku hiyo gari zote zilizokuwa mbele yangu sikuwahi kuziendesha so nikawa natamani kuziendesha zote ila priority ilikuwa ni VW Touareg
Jamaa alichokifanya akaanza kumpa yule mwenzake funguo ya BMW halafu mm akanipa ya Audi na yeye akabaki na ya Volkswagen ila kwangu ikawa sio mbaya kwasababu kama ningepewa nafasi ya kuchagua kati ya Audi na BMW Bado ningechagua Audi
Gari zilikuwa zishafanyiwa Service na Kila kitu na namba plate inasoma E, tukaanza safari VW ndio ilitangulia ikafuata BMW then wa Audi nikaunga tela, kwenye kisahani Cha speed wote tulikuwa sawa Audi inasoma 260 BMW nayo ina 260 ila Volkswagen ndiye ametuzidi kidogo yeye ana 280, lakini hilo halikumata kwasababu tulikuwa hatuendi mbali
Tukafika Salama nyumbani tukapaki vyuma ila Gari moja tu ikawa imeharibu ambayo ni Toyota Alphard Jeep Wrangler hatukuikuta, wale wenzangu wawili wakaondoka wakaniacha,
Mzee: "Katika maisha yangu yote ya kumiliki magari sijawahi kumiliki wala kuendesha Audi, umeionaje huko barabarani Iko vizuri?"
BM: "Mm mwenyewe Mzee ndio mara ya kwanza naendesha hii Gari, imetulia kiasi chake, ila siwezi kutoa majibu ya uhakika kwasababu Sina uzoefu wa kuendesha magari tofauti tofauti"
Mzee: "Okay, Iko na Body shape Nzuri hata hivyo"
BM: "Inaonesha hukuwahi kuipenda Audi, imekuaje umeiagiza sasa"
Mzee: "Hizi Gari zote sio za kwangu, hiyo Audi ni ya Michelle, BMW ni ya Caryn na Volkswagen ni ya Mama yako"
BM: "Ooh! sasa mbona ww hujajichukulia?"
Mzee: "Si Gari zingine zipo (Jeep & Alphard) nilitaka Kila mtu awe na Gari yake ili kuondoa kero hasa Caryn ni msumbufu sana linapokuja swala la magari"
Mzee: "Unajua Jeep nilijinunulia na Ile Land cruiser ilikuwa kwaajili ya Mama yao halafu wao nikawachukulia Alphard, Cha ajabu wote wakawa hawaitaki, wakiwa na safari zao Caryn atachukua Gari yangu Michelle naye atachukua Gari ya Mama yake"
Wakati huo tunaongea bado tulikuwa Parking, Mama nae akaja akatukuta tunazungumza na Mzee, halafu ni kama vile mama alikuwa anajua Gari zinazokuja ni mbili tu
Mama: "Gari ya Michelle ndio ipi hapa?"
Mzee akamuoneshea Audi Q3 ya Black Metallic
Mama: "Na ya Caryn?"
Mzee akamuoneshea BMW X3 nayo pia ni Black Metallic
Mama: "Ooh, Sasa hiyo gari nyingine ndio ya kwako?
Mzee: "Hapana, mimi ya kwangu si ni Jeep hiyo ni ya kwako"
Mama: "Jamani kulikuwa kuna haja gani ya kununua magari yote haya Wakati magari mengine Bado yapo"
Mzee: "Magari mengine hayo yapi unayoyazungumzia, wewe Gari lako limeharibika (Land Cruiser) ndio maana nimekuchukulia hilo, na hawa watoto nimewachukulia magari yao ili kila mtu ajipange na ratiba zake vizuri"
Mama: "Sawa, acha mimi nikimbie kule msibani japo nikaonekane"
Mzee akawa anampa Mama funguo ya Volkswagen, Mama akakataa
Mama: "Hapana, nitaenda na Toyota (Akimaanisha Alphard) hiyo Gari Bado ni mpya isije ikanisumbua Barabara"
Mzee hakupinga, Mama akatekenya li-Alphard akaondoka, nyumba nzima tukabaki mimi na Mzee pamoja na Mdada wa kazi
Tukahamia Backyard, Tangu Mzee arudi safari hii ndio mara ya kwanza kwenda kukaa Backyard, halafu nilichoki-note leo Mzee anaongea ki friendly zaidi tofauti na Ile siku ya Kikao
Tulivyofika Backyard mada tuliyoanza nayo Mzee aliniuliza kuhusu wale madogo, nikamuelezea ukweli kwamba Dogo hafanyi Biashara kwasasa ila kuna ujuzi anaupata ili kujiandaa kwaajili ya kuja kufanya Biashara hapo badae,
Akauliza wanapoishi nikamuambia wanaishi kwa sister ila nina mpango wa kuchukua nyumba kubwa ili niishi nao
Mzee: "Umenijibu sawa na kile Caryn alichonieleza"
BM; "Ooh kumbe amekuambia?"
Dah! ila huyu Demu miyeyusho kinoma sasa kama ningeongopa ingekuaje na hakunipanga kama amemuambia Mzee
Mzee: "Yeah na pia amesema anataka kukurudisha pale ofisini, sasa sijajua kama utakuwa na muda wa kujigawa"
BM: "Acha tuone kama itawezekana Mzee japo ratiba zangu sio tight sana kwa sasa"
Nikajifanya kuzuga kwamba nina shughuli za kufanya kumbe sina lolote, muda kidogo tukasikia Gate linafunguliwa, Alikuwa ni Caryn
Caryn: "Hi Dad....Mambo BM"
BM: "[emoji1531]"
Mzee: "Hellow, how was your day?"
Caryn: "Great"
Mzee: "Mwenzio yupo wapi"
Caryn: "Nimemuacha ofisini nimeona atanichelewesha, then Dad I saw BMW and others cars, I hope BMW is mine"
Mzee: "Ngoja kwanza....Caryn unajua ww safari zako ni za kibinafsi mwenzako safari zake ni za kiofisi yeye ndiye anapaswa kutumia Gari, kitendo Ulichokifanya sijakipenda hata kidogo"
Caryn: "Lakini Dad yeye mwenyewe kaniruhusu"
Mzee: "Michelle kakuruhusu tu kwasababu anajua hata angekuambia umuachie gari usingekubali"
Caryn: "I swear Dad nilitaka ku request Cab akanambia niondoke tu gari"
Mzee: "Sasa Gari yangu mtaachana nayo, kuanzia kesho Kila mtu atumie Gari yake"
Mzee akampatia Caryn Key ya BMW kisha Caryn akaelekea Parking sijui ndio kaenda kuitest, nikabaki na Mzee
Mzee: "Huyu mtoto anapenda sana Magari utadhani wa kiume, Michelle ndio hana hata time nayo"
BM: "Kweli, mm mwenyewe sijawahi kumuona Michelle akiendesha gari"
Baada ya muda kidogo Caryn akarudi akiwa na furaha akamuambia Baba yake kwamba ameipenda Gari
Mzee: "Sasa hivi wote mnafanya kazi, sitaki kusikia mtu ananiomba Pesa ya mafuta"
Caryn: "But Dad mm bado sijaanza kazi"
Mzee: "Si wiki ijayo tu unaanza kazi, halafu kuhusu kazi naomba usiende huko ukaanza kufukuza watu kazi hovyo"
Caryn: "Dad kama unaona sifai tafuta mtu mwingine wa kufanya hiyo kazi, kama umeamua mm ndio nifanye basi niache na maamuzi nitakayoyafanya"
Mtu mzima nipo pembeni nawasikiliza Baba na Mwana
Caryn: "Mfano kama yule mtu anaye clear mizigo sasa hivi bandari ni mzembe sijapata kuona, ndio maana nataka BM arudi"
Mzee: "Fanya utakavyofanya lakini usiharibu kazi"
BM: "Mzee mm naomba niwaache"
Mzee: "Sawa ww nadhani tutawasiliana sasa "
Nikatoka na Caryn akinisindikiza hadi nje kabisa ya Geti, mm huwaga sina hizi apps za ku request sababu sio mtu wa ku request, usafiri wangu mkubwa ni Boda, Bajaj na daladala, Caryn akani requestia Bolt Wakati tunasubiria Bolt ikabidi nimuulize
BM: "Caryn mbona hukunipanga issue ya kazi hadi Mzee ndio ameniambia"
Caryn: "Kwani sikukuambia?"
BM: "Hujaniambia chochote mimi, Yani Leo ndio Mzee ameniambia na wewe nimekusikia Sasa hivi"
Caryn: "Dah mambo ni mengi kichwani nisamehe Bure"
BM: "Kwahiyo ulivyomwambia Mzee akasemaje"
Caryn: "Dad hawezi nikatalia kitu, na nishaongea Boss wako (Mama Accnt) we jiandae Jumatatu tukutane Kazini"
Dah! ukisikia Second chance ndio hii, kama namuona Accountant na huko ofisini sijui itakuaje yani Caryn na Accountant uwaweke pamoja show yake sijui itakuaje
Bolt ikafika mm nikaondoka, katika zile pesa Milioni 5 nilizopewa na Mama Accnt ilibaki kama 4.5 plus na Ile milioni ya Caryn Jumla inakuwa 5.5 milion sasa kesho ni mwendo wa kucheki na madalali wanitafutie nyumba maana nishapata uhakika wa maisha
Wiki ikaisha sijapata nyumba niliyoipenda halafu nilitaka nihamie kwenye makao mapya kabla sijaanza kazi,
Siku ya kuripoti kazini ikafika hii siku niliambiwa niwahi sana sababu ya vikao ndio siku ambayo Caryn anaenda kuachiwa Ofisi rasmi, ratiba niliyopewa inasoma vikao ni vitatu,
Kikao Cha kwanza kinaanza 08:30hrs ambacho kitaongozwa na Mama Accnt, hiki kikao kinawahusu staff wote kwasababu anaenda kutambulishwa MD mpya,
Kikao Cha pili ni After Break time 11:05hrs nacho kitaongozwa na Mama Accnt, hiki kitawahusu vichwa vya Kampuni tu, Yani Mama Accnt mwenyewe Secretary, Caryn, Accountant pamona na Mimi
Kikao Cha tatu na Cha mwisho kitafanyika majira ya mchana after Lunch time 14:00hrs ambacho kitaongozwa na Caryn, hiki pia kitahusisha staff wote wa Kampuni kasoro Mama yake Accnt tu
Aisee hii siku nikachelewa Nakumbuka mvua ilinyesha hii siku jam huko barabarani si ya kitoto, hadi nafika ofisini ilikuwa ni saa 08:49hrs, hadi muda huu kikao kilitakiwa kiwe kimeenza Wakati nipo njiani Mama Accnt alinipigia simu akanambia "Unajua wewe ndio unasubiriwa" nikashuka kwenye kidala nikadaka Boda
Sasa nimefika ofisini naingia room ambako kunafanyika meeting nimekuta staff wote akiwemo Accountant, Mama Accnt pamoja na Caryn
Accountant: "Ivi tukiongea tu ukweli mtu anawezaje kuchelewa siku kama leo? Uzembe mwingine umepitiliza viwango"
Caryn: "Binti kaa kimya kuna Mahali nilimuambia apitie ndio maana amechelewa Mama unaweza kufungua kikao"
Nikamuangalia Caryn nikakuta yupo serious yani anachokiongea anakimaanisha, Accountant nae akanipiga jicho la wizi, nikaa kwenye kiti ila ukweli ni kwamba hakuna sehemu Caryn ameniagiza nimechelewa tu kwa uzembe wangu kama Accountant alivyosema
Itaendelea
Umughaka 2Asante mkuu kwa kutii kiu ya wengi..
Tunasubiri umalizie
Fanya kwa vitendo ww kwanza halafu sisi tutafuatatunaomba tulipie hata 1000 buku labda jamaa hana bundle
tupewe lipa nambaFanya kwa vitendo ww kwanza halafu sisi tutafuata
Duh! Lipa namba tena? Atakuwa nayo kweli?tupewe lipa namba
Laiti kama Members wote wangekuwa kama wewe hii story ingekuwa nzuri sana zaidi ya hapa watu wanavyoiona kwasababu nikiandika huwa nakimbizana na muda ili nisiwacheleweshe sana so kuna matukio mengine nayasahau.we kaa tulia tunga taratibu usiwe na haraka mzee
ili ukija hapa utupe kilicho bora
okayLaiti kama Members wote wangekuwa kama wewe hii story ingekuwa nzuri sana zaidi ya hapa watu wanavyoiona kwasababu nikiandika huwa nakimbizana na muda ili nisiwacheleweshe sana so kuna matukio mengine nayasahau.
Ila kama ningekuwa napost at least kila baada ya wiki mbili ningekuwa napata muda mzuri wa kukumbuka matukio na kukumbuka maongezi jinsi yalivyokuwa
Kama Episode iliyopita kile kipande nipo na Mzee Ile Conversation ilitakiwa iwe ndefu na maongezi yalikuwa muhimu sana lakini Nimekuja kukumbuka baadhi ya sehemu nikiwa tayari nishapost