tatzoKIBUNDA
Member
- Mar 10, 2021
- 5
- 7
Kuna mtu mtaani aliniambia marehemu akifa akaacha deni Bank basi Deni hilo linasamehewa na kwamba Bank inalazimika kutoa pia mkono wa pole kwa wafiwa. Hii ni kweli ?Deni litalipwa kutokana na mali ulizoacha, bank watasaidiana na msimamizi wa mirathi kabla hajaanza zoezi la kugawa mali ulizoacha
Tukuulize ulikua na mpango waa kufa kabla haujamaliza mkopo au ulikua na mpango baada ya kukopa tu ufe? Yaan mpango wako ni upi kati ya hio? Unataka ukope million 500 mpaka 800 halafu unakufa bank inapata faida kutokana na kifo chako si ndio?Je, Mkopo huo bado utatakiwa kulipwa ?
Kama ni mtumishi wa serikali, wewe kufa tu. Bima italipa. Ila kama ni mfanyabiashara, na uliwekea dhamana nyumba! Aisee nyumba itapigwa mnada kama uliowaachia urithi watashindwa kulipa hilo deni. Kwa hiyo usijiue kwa makusudi halafu ukafikiri benki itakuchekea tu.Je, nikiwa nimekopa Mkopo katika Benki yoyote nchini Tanzania (NMB as case study) alafu kabla sijamaliza kulipa Mkopo huo, Nikafariki. Je, Mkopo huo bado utatakiwa kulipwa ? Kama ni ndio, je ni nani atawajibika kulipa ?
Naomba Ufafanuzi pamoja na msimamo wa Sheria katika jambo hilo
Benki watauza dhamana uliyowekaJe, nikiwa nimekopa Mkopo katika Benki yoyote nchini Tanzania (NMB as case study) alafu kabla sijamaliza kulipa Mkopo huo, Nikafariki. Je, Mkopo huo bado utatakiwa kulipwa ? Kama ni ndio, je ni nani atawajibika kulipa ?
Naomba Ufafanuzi pamoja na msimamo wa Sheria katika jambo hilo
Ikitokea mtu ameacha kazi na bado ana rejesho kama milioni 20 ivi. Sheria inasemaje hapo?Deni litalipwa kutokana na mali ulizoacha, bank watasaidiana na msimamizi wa mirathi kabla hajaanza zoezi la kugawa mali ulizoacha
Mkopo haujui una kazi au hauna, inachojua ni deni kulipwa basi.Ikitokea mtu ameacha kazi na bado ana rejesho kama milioni 20 ivi. Sheria inasemaje hapo?
Nafikiri hua kuna terms and conditions za kila mkopo na aina ya dhamana.Ikitokea mtu ameacha kazi na bado ana rejesho kama milioni 20 ivi. Sheria inasemaje hapo?
Kama dhamana ya mkopo ilikua ni ajira basi Bima italipa, lakini kama dhamana ya mkopo ilikua nyumba ama kiwanja ama gari, basi dhamana itauzwa ili kumalizia deni la marehemJe, nikiwa nimekopa Mkopo katika Benki yoyote nchini Tanzania (NMB as case study) alafu kabla sijamaliza kulipa Mkopo huo, Nikafariki. Je, Mkopo huo bado utatakiwa kulipwa ? Kama ni ndio, je ni nani atawajibika kulipa ?
Naomba Ufafanuzi pamoja na msimamo wa Sheria katika jambo hilo
Asante mkuuNafikiri hua kuna terms and conditions za kila mkopo na aina ya dhamana.
Lakini kwa ufupi ni kwamba ikitokea umeamua kuacha kazi kwa hiyari ama umesitishwa kazi, na wakati huo ulikua na mkopo dhamana ikiwa ni hiyo ajira... basi hapo utaenda kufanya mazungumzo na bank husika ili uone namna ya kulipa kwa rejesho la nafuu.