Hatma ya Muungano ipo mikononi mwa Maalim Seif, ili kuulinda basi tumtendee haki huyu mzee angali hai

Hatma ya Muungano ipo mikononi mwa Maalim Seif, ili kuulinda basi tumtendee haki huyu mzee angali hai

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Maalim Seif ni Mtanzania, tena ni Mtanzania mzalendo kwelikweli!

Ni miongoni mwa watu ambao mwalimu Nyerere aliwaheshimu sana kutokana na misimamo thabiti na kipawa chake kikubwa sana cha akili.

Lakini ukiacha kuipenda Tanzania, Maalim anaipenda sana Zanzibar, nchi aliyozaliwa. Wazanzibar wanamheshimu pia.

Sisi huku Tanganyika tuliamua kuendelea kumuita Nyerere "mwalimu", Siyo kwamba hakuna viongozi wengine walikuwa walimu huko zamani, bali ni kutokana na ukweli kuwa Nyerere alikuwa mtawala lakini pia aliendelea kuwa mwalimu wa falsafa za maendeleo na haki.

Na huko Zanzibar mzee wao wampendaye wakaamua kumuita "Maalim", hii ni lahaja tu za Kiswahili lakini mwalimu na maalim ni maneno yenye maana ileile kumaanisha "yule afundishaye"

Maalim Seif amekuwa mvumilivu mno katika masuala ya siasa, kafanyiwa faulo na madhambi chungu nzima katika njia yake ya kisiasa, lakini hajawahi kuhamasisha vurugu, uvunjifu wa amani, umwagaji damu au kuumiza Wazanzibar kwa sababu za kisiasa. Na kitendo hiki cha kuweka mbele maslahi ya wazanzibar ndicho kilichompa heshima sana mbele ya wazanzibar wenyewe.

Tanzania ya Leo ina bahati moja. Ina mtu ambaye ni kipenzi cha Wazanzibar, na pia ni muumini wa Muungano. Natoa rai kwa serikali ya Nchi hii, MTUMIENI HUYU MZEE VIZURI KULINDA MUUNGANO KABLA HAJATANGULIA MBELE YA HAKI!

Hatari ninayoiona ya kudhani kuwa Kuwalazimishia Wazanzibar kiongozi ndiyo njia sahihi ya kulinda muungano, hii ni njia yenye upeo mfupi sana, itafika mahali Wazanzibar watapata Kiongozi mwingine ambaye ni Radical, na huyu anaweza kuwamobilize Wazanzibar waukatae muungano.

Ikifikia hapo, ama itabidi mtumie nguvu kuulinda, mtapelekea umwagaji damu wa kutisha na Dunia itawagomea na itawalazimisha muwaache Wazanzibar wenyewe na nchi yao huku wahusika wa vitendo hivyo wakichukuliwa hatua na mahakama za kimataifa Au itabidi muwaachie tu nchi yao wajitawale!

Sasa sisi tukitumia busara hatupaswi kufika huko, Tumsaidie Maalim na Wazanzibar kwa kuwapa haki yao ya uchaguzi bila kuleta mambo ya Jecha, Kisha maalim atasaidia kuutetea muungano na wazanzibar watamsikiliza.

Uzuri wa mtu kama Maalim ni kuwa hawa ni aina ya viongozi ambao hata wakiwa wameshatangulia mbele ya haki basi vizazi na vizazi huendelea kuwafanya rejea ya utatuzi wa. mambo mbalimbali maana wanakuwa wameacha alama.

Kama Maalimu akiwa raisi wa Zanzibar na akafanikiwa kuweka precedence ya kuuheshimu muungano, basi amini usiamini huu Muungano utakuwa legitimized zaidi vizazi na vizazi vijavyo. Lakini mkimnyima maalim ushindi wake, kisha wazanzibar wakaweka dukuduku moyoni, basi dukuduku hilo litaendelea vizazi na vizazi vya wazanzibar na kuuona muungano kama project ya Ukoloni mamboleo na hivyo kuudharau, kutoupenda na kufanya kila wawezao kuondokana nao na bahati mbaya watakuwa hawana mtu katika historia wa kumfanya rejea ya namna alivyodeal na muungano na akatunza maslahi yao kama nchi!

Hayati Benjamin Mkapa hadi mwishoni mwa uhai wake alijuta sana yaliyotokea pemba kipindi cha utawala wake, na alitamani kuona Muungano wetu unaimarika na pia manung'uniko ya Wazanzibar yanaisha. Na alitamini kuona Wazanzibar wenyewe wanachagua kiongozi wao wenyewe kwa haki bila kuingiliwa.

Tumtumie Maalim kutuwekea precedence nzuri ya kuulinda muungano wetu, nje ya hapo tutegemee radicals wenye ushawishi wasioutaka huo muungano waungwe mkono na Wazanzibar kisha muuone kama huo muungano wenyewe mtafanikiwa kuulinda!

Hatuwezi kuulinda Muungano kwa "kuwateulia" Wazanzibari rais Dodoma kama tulivyofanya kwa huyu mnayemuita "rais mteule"

Maalim Shikamoo!
 
"Zanzibar ilikua nchi huru kabla hata ya Tanganyika. Kipindi Tanganyika ikiwa imetawaliwa bado na mjerumani ikiitwa GERMAN EAST AFRICAN COLONY, Zanzibar ilikua inatambulika kama nchi."

"Kisa Karume na Nyerere walikaa pamoja basi Zanzibar itawaliwe na Tanganyika?". Zanzibar irudi kwenye ukoloni wa kutawaliwa. Kwamba Waziri wa Kilimo wa Tanganyika akitaka kwenda nje anakwenda kama Waziri wa Tanzania, ila Waziri Wa Kilimo wa Zanzibar akitaka kwenda nje mpaka aombe ruhusa."

- Dk Azaveli Lwaikama
 
Uchaguzi bado, unapenda Seif aaipshwe tu kwa kile unachokiita kwamba yeye ndiyo Mzanzibar na kwamba Dr Hussein ni mbara na kwamba Wazanzibar wamepangiwa mbara? Ni aina gani ya mawazo haya? Kwanini tusiwe waungwana tukawaachia wananchi wakaamua badala ya kuanza kuwa na ile dhana ya kuonewa?
 
Huyu mzee naye TISS tu.

Kama angekuwa TISS wasingempora ushindi wake mara kwa mara.

Yeye mara kibao amelalamikia System kuingilia chama chake cha zamani cha CUF na kukivuruga ili akose platform ya kufanyia siasa.
Sasa sijui TISS gani wanamharibia TISS mwenzao!

Mimi ninachojua, vyama vyote na taasisi zote nchini TISS wapo.

Na mtu kuwa TISS haimaanishi huruhusiwi kushindana kihalali na kutwaa dola, maana TISS ni rafiki wa Taifa si adui ya Taifa. Na Taasisi ya TISS haipaswi kuwa biased in favor ya CCM labda kama wanajipa majukumu yasiyowahusu. TISS huwa ni kwa ajili ya wananchi!

Kwao hawajali kama mtu wa TISS aliyeko upinzani atapambana na mtu wa TISS aliyemo CCM kwenye kinyang'anyiro fulani cha kisiasa ili kutwaa uongozi wa nchi. Eventually wote ni watu wa Taifa moja
 
Kwao hawajali kama mtu wa TISS aliyeko upinzani atapambana na mtu w TISS aliyemo CCM kwenye kinyang'anyiro fulani cha kisiasa. Evuntually wote ni watu wa Taifa moja
Umeandika vizuri mkuu, TISS nikwamaslahi ya taifa na si ccm.
 
Kama angekuwa TISS wasingempora ushindi wake mara kwa mara.
Yeye mara kibao amelalamikia System kuingilia chama chake cha zamani cha CUF na kukivuruga ili akose platform ya kufanyia siasa.
Sasa sijui TISS gani wanamharibia TISS mwenzao!
Mimi ninachojua, vyama vyote na taasisi zote nchini TISS wapo.
Na mtu kuwa TISS haimaanishi huruhusiwi kushindana kihalali na kutwaa dola, maana TISS ni rafiki wa Taifa si adui ya Taifa. Na Taasisi ya TISS haipaswi kuwa biased in favor ya CCM labda kama wanajipa majukumu yasiyowahusu. TISS huwa ni kwa ajili ya wananchi!
Kwao hawajali kama mtu wa TISS aliyeko upinzani atapambana na mtu wa TISS aliyemo CCM kwenye kinyang'anyiro fulani cha kisiasa ili kutwaa uongozi wa nchi. Eventually wote ni watu wa Taifa moja
Ila Sio kwa TISS ya Tanzania ni kama polisi tu
 
Back
Top Bottom