Hatma ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iamuliwe na wananchi

HOJA NI KWAMBA, kwanini tusifute tu hivi vinnchi viwili, tuwe na moja tu na zanzibar iwe MKoa? tuwe na rais mmoja.
Nyerere alitaka ku preserve history ya Zanzibar. Popote pale duniani nchi ndogo kwa ardhi na idadi ya watu inapoungana na nchi kubwa kijiografia na idadi ya watu nchi ndogo huwa na hofu ya kumezwa. Wakati tunaungana Zanzibar ilikuwa na watu 360,000 huku Tanganyika ikiwa na watu 12milioni. Lkn Zanzibar ilikuwa ni nchi kamili. Kutaka Serikali moja na Rais mmoja ni kuidogosha Zanzibar na kuifanya kuwa Mkoa sawa na Mwanza. Tunaweza kuondosha kero za Muungano bila kuidogosha Zanzibar. Kutoka kero 22 Hadi kubakia 4 ni mafanikio makubwa mno
 
Kwanini usipigiwe kura na wananchi?
 
Tulishatoa maoni yetu Kwa Tume ya Jaji Warioba tuna taka serikali tatu full stop kukusanya maoni tena ni upigaji wa fedha za umma kama upigaji mwingine
 
Hizo kero mbona huwa hamzitaji mnaishia tu kusema idadi?
 
Kwanini usipigiwe kura na wananchi?
Mwishoni mwa 1700 huko USA kulikuwa civil wars. Hizo civil wars zilikuwa ndiyo zinaunganisha states mbalimbali. Kumbuka kuwa USA ilitawaliwa na mataifa 4 kila mmoja na kipande chake; Netherlands, United Kingdom, Spain na France. Kuwa nchi moja kulipiganwa vita na kupata USA yenye 51 states.

Hakuna mwanachi yeyote alipiga kura.

Kwa karne hii muungano ni bora kuliko utengano. Kero ziendelee kutatuliwa
 
Mimi sikatai, juzi tumeona wananchi kule Uingereza walipiga kura na PM akajihuzulu, why not us? mtu kutoka bara anafaidika na nini na huu muungano fake? ukinunua gari Zanzibar huna tofauti na kununua gari Ujerumani
 
Utaambiwa Muungano upigiwe kura na tume ya uchaguzi ndio itazihesabu
 
Embu niambie huu muungano wetu ni wa aina Gani nipe japo mfano mmoja wa muungano wa aina yetu
Kero kubwa kwenye huu muungano ni serikali mbili kutatua hii ni serikali tatu tusidanganyane hata kidogo
 
Nani atasimamia hizo kura za maoni?
 
Kila nchi Ina historian yake. Hata mkoa wa Iringa una historian tofauti na Kilimanjaro. Cha muhimu historian ziwekwe pembeni tuwe na Muungano kama wa marekani. Nchi owe Moja yenye utawala wa majimbo.
 
Mimi sikatai, juzi tumeona wananchi kule Uingereza walipiga kura na PM akajihuzulu, why not us? mtu kutoka bara anafaidika na nini na huu muungano fake? ukinunua gari Zanzibar huna tofauti na kununua gari Ujerumani
Unataka kuvunja muungano kwa ajili ya gari tu uliyonunua ZNZ?

Si uende tu Mnazi Mmoja, Ilala na Kinondoni show rooms za magari kibao
 
Unataka kuvunja muungano kwa ajili ya gari tu uliyonunua ZNZ?

Si uende tu Mnazi Mmoja, Ilala na Kinondoni show rooms za magari kibao
Mbona wao wananunua kutoka kwetu? nimekupa tu mfano wewe mpuuzi, niambie mtu wa bara ananufaika kwa kipi na huu muungano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…