Hatma ya Raia kuzuia Polisi kuwakamata raia kuwapeleka vituo vya polisi wakihofia kutekwa

Jeshi la polisi nchini linaendelea kujipanga na kujizatiti zaidi kulinda usalama wa watu, mali na makazi yao, licha ya dosari, kasoro na changamoto kidogo zilizopo kwenye jamii kwa sasa..

tuvute subra na tuwe wastahimilivu kwa hali hiyo. Viongoz wanatafuta majawabu ya uhakika, na katika muda usiokua mrefu sintofahamu hiyo itakwisha, na kama Taifa tutasonga mbele pamoja na kwa kuaminiana zaidi 🐒

..polisi wameleta utamaduni mpya na mbaya wa kufanya ukamataji wakiwa hawajavaa sare.
 
kama hilo ni tatizo, jeshi la polisi nchini ni la waTanzania, ni wangwana sana, ni wasikivu sana ni wazi watabadilisha hali hiyo kwa haraka sana na tena kwa wakati muafaka...

ni muhimu sana wananchi pia kuepuka ukaidi, jeuri na kiburi dhidi ya wito na ilani za polisi ambazo ni kwa mujibu wa sheria na ni kwa manufaa ya usalama wao 🐒

nadhan tupo pamoja

..huo utaratibu alishika kasi wakati wa Magufuli.

..nilitegemea Mama 4R atakomesha utamaduni huo.

..wakati tunakua tulifundishwa kwamba mtu anayebeba silaha huku amevaa kiraia ni jambazi.
 
Jeshi la polisi nchini linaendelea kujipanga na kujizatiti zaidi kulinda usalama wa watu, mali na makazi yao, licha ya dosari, kasoro na changamoto kidogo zilizopo kwenye jamii kwa sasa..

tuvute subra na tuwe wastahimilivu kwa hali hiyo. Viongoz wanatafuta majawabu ya uhakika, na katika muda usiokua mrefu sintofahamu hiyo itakwisha, na kama Taifa tutasonga mbele pamoja na kwa kuaminiana zaidi 🐒
Linajipanga kwenye nchi yenye miaka 60 plus??
 
aah,
mie nimeshaeleza kwa kirefu zaidi, jambo hilo linashudhulikiwa na kutafutiwa majawabu na leo umeona mkuu wa nchi pamoja na IGP wakiwa na mazungumzo marefu sana...

kuna mabadiliko makubwa zaidi yanakuja na hali hiyo itabadilika kabisa 🐒
Hao ndio vinara wa kuteka wapinzani. Kwa hiyo huo mkutano wao ni mkutano wa nyonya damu. Bila machafuko hatuwezi kupata mabadiliko ya kweli.
 
Nadhani Chadema wakimaliza Uchaguzi wao wa ndani bilashaka patatulia tu, nadhani Tatizo lipo kwenye nafasi ya juu ya Uongozi wa Chama 🐒
 
Linajipanga kwenye nchi yenye miaka 60 plus??
lazima kujipanga kulingana na mbinu mpya ambazo wahalifu wanazitumia kufanya uhalifu ndani ya jamii,

Hilo ni jambo muhimu, la maana na endelevu katika kuimarisha utendaji, ulinzi na usalama wa watu, mali na makazi yao 🐒
 
Sidhani kama kuna raia anaweza kumzuia Polisi asimkamate mhalifu kama Polisi akifuata taratibu zilizopo.
Polisi wanatakiwa waelewe kwa sasa wananchi wengi ni waelewa wanajua haki na wajibu wao pindi Polisi anapotaka kumkamata.
Tatizo Polisi hawafati taratibu ambazo zipo za jinsi ya kumkamata mtuhumiwa ikiwamo kujitambulisha ,kuonyesha kitambulisho na kuwa na nyaraka kama search warrant ya mahakama.
Pili kuna ongezeko la watu kuchukuliwa kienyeji na Polisi na kisha kupotezwa au kwenda kuuwawa kisha Polisi kukataa kwamba sio wao .
Kwa muktadha huo lazima Raia wawe wakali kujilinda .
Kinachotakiwa ni Polisi kufata taratibu kama GPO inavyoelekeza
PGO
 
..huo utaratibu alishika kasi wakati wa Magufuli.

..nilitegemea Mama 4R atakomesha utamaduni huo.

..wakati tunakua tulifundishwa kwamba mtu anayebeba silaha huku amevaa kiraia ni jambazi.
mlifundishwa upotofu Lakini si mbaya,

hata hivyo jambo muhimu na la maana sana ni kwamba polisi Tanzania imedhamiria na kujizatiti kuhakikisha inatekeleza majukumu yake ya kulinda watu, mali na makazi yao kwa ufanisi zaidi licha ya changamoto zilizopo 🐒
 
Hali ya raia kuzuia polisi kukamata watu nchini Tanzania ni jambo linaloweza kuashiria mabadiliko makubwa katika mfumo wa utawala na usalama wa raia.

Katika kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na matukio kadhaa ambapo wananchi wamejitokeza kuzuia polisi wasiwakamate watu, ikiwemo waandamanaji, wapinzani wa kisiasa, na hata watu wengine wanaoshukiwa na makosa mbalimbali.

Hali hii inaonyesha mabadiliko ya mtazamo wa raia kuhusu haki zao na wajibu wa serikali.

Mwanzo wa hali hii unategemea hisia za kukosekana kwa haki na usawa katika jamii. Watu wengi wanahisi kuwa polisi wanafanya kazi kwa maslahi ya kisiasa badala ya kulinda raia. Hivyo, raia wanapojitokeza kuzuia kukamatwa, wanajitahidi kulinda haki zao na kutetea wenz wao dhidi ya unyanyasaji.

Hii inaashiria kuwa kuna ongezeko la uelewa wa raia kuhusu haki zao za kisheria na umuhimu wa ushirikiano katika kutetea haki hizo.

Hata hivyo, hali hii inaweza kuwa na athari kubwa kwa usalama wa raia na utulivu wa nchi. Kuzuia polisi kukamata watu kunaweza kuleta machafuko na kupelekea majibizano kati ya raia na vyombo vya usalama. Katika mazingira kama haya, kuna uwezekano wa kuongezeka kwa ghasia na uvunjifu wa amani, jambo ambalo linaweza kuathiri sio tu wale wanaohusika moja kwa moja, bali pia jamii nzima.

Kama hali hii itaendelea, inaweza kupelekea mabadiliko katika sera za usalama na utawala. Serikali inaweza kujikuta ikilazimika kuboresha mawasiliano yake na raia, pamoja na kubadilisha mbinu za kikazi za polisi ili kujenga uhusiano mzuri na wananchi. Aidha, kuna uwezekano wa kuanzishwa kwa mijadala ya kitaifa kuhusu haki za raia na wajibu wa vyombo vya usalama, ili kujenga mazingira ya kuaminiana na ushirikiano.

Soma Pia:

Kwa upande mwingine, ikiwa serikali haitachukua hatua za haraka kujibu malalamiko ya raia, inaweza kujikuta ikikabiliwa na maandamano zaidi na upinzani mkali. Hali hii inaweza kusababisha mgawanyiko katika jamii, ambapo kundi moja linaweza kujiona kama lina haki zaidi kuliko jingine, na hivyo kuathiri umoja wa kitaifa.

Kwa kumalizia, hali ya raia kuzuia polisi kukamata watu Tanzania ni ishara ya mabadiliko katika mtazamo wa raia kuhusu utawala wa sheria. Ingawa ni hatua inayoweza kuashiria uhamasishaji wa raia, ni muhimu kwa serikali na jamii kukabiliana na hali hii kwa njia ya amani na majadiliano ili kuhakikisha usalama na utulivu wa nchi unadumishwa.
Kwa upande wangu, vyombo na ama wadau wanaotoa elimu ya kisheria wangelifanyia kazi hilo kuwaelimisha raia kujua haki zao pindi wanapohitajika na polisi kituoni. Pili, raia waelimishwe pia polisi anapokuja kumkamata raia au kufanya upekuzi nyumbani ni mambo gani yanatakiwa yazingatiwe. Na je kama hayo mambo yasipozingatiwa wakati wa kumkamata raia au kufanya upekuzi nyumbani kwake, raia anatakiwa afanye nini au akalalamike wapi? Elimu kama hii ikifanyiwa kazi na pande zote mbili - upande wa polisi na upande wa raia - tatizo litaisha lenyewe. Lakini kama raia akitaka kujua kosa lake, then anajibiwa "usinifundishe kazi au kosa utalijua huko huko kituoni" (kama ambavyo baadhi ya watu huwa wana'share'), mvutano katika maeneo hayo mawili - ukamataji na upekuzi wa makazi - utaendelea kuwepo.
 
lazima kujipanga kulingana na mbinu mpya ambazo wahalifu wanazitumia kufanya uhalifu ndani ya jamii,

Hilo ni jambo muhimu, la maana na endelevu katika kuimarisha utendaji, ulinzi na usalama wa watu, mali na makazi yao 🐒
Kwahiyo hawakuweza kufikiria mbele patakuwaje?

Hawana intelijensia??

Kwahiyi wakati wanajipanga watu waendelee kufa na kupotezwa?
 
wakati unamendea mke wa watu kwa siri, unataka polisi wawepo, right? ili baadae mseme wanaingilia privacy za watu, si ndiyo?

ukifumaniwa na kufanyiwa utakachofanyiwa, mnaanza tena lawama na kuuliza intelijensia Ilikua wap?🤣

acha kumendea wake za watu,wacha kudhulumu haki za wengine...

ni muhimu sana kuishi kistaarabu na kuheshimiana ndani ya jamii.

na vyama vya siasa vinavyoendelea na uchaguzi wao wa ndani, Uongozi si Lazima ukatishe maisha wa mwingine ndrugo zango, inauma sana.

Malizeni uchaguzi kwa amani na bila kinyongo 🐒
 
Hali ya raia kuzuia polisi kukamata watu nchini Tanzania ni jambo linaloweza kuashiria mabadiliko makubwa katika mfumo wa utawala na usalama wa raia.

Katika kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na matukio kadhaa ambapo wananchi wamejitokeza kuzuia polisi wasiwakamate watu, ikiwemo waandamanaji, wapinzani wa kisiasa, na hata watu wengine wanaoshukiwa na makosa mbalimbali.

Hali hii inaonyesha mabadiliko ya mtazamo wa raia kuhusu haki zao na wajibu wa serikali.

Mwanzo wa hali hii unategemea hisia za kukosekana kwa haki na usawa katika jamii. Watu wengi wanahisi kuwa polisi wanafanya kazi kwa maslahi ya kisiasa badala ya kulinda raia. Hivyo, raia wanapojitokeza kuzuia kukamatwa, wanajitahidi kulinda haki zao na kutetea wenz wao dhidi ya unyanyasaji.

Hii inaashiria kuwa kuna ongezeko la uelewa wa raia kuhusu haki zao za kisheria na umuhimu wa ushirikiano katika kutetea haki hizo.

Hata hivyo, hali hii inaweza kuwa na athari kubwa kwa usalama wa raia na utulivu wa nchi. Kuzuia polisi kukamata watu kunaweza kuleta machafuko na kupelekea majibizano kati ya raia na vyombo vya usalama. Katika mazingira kama haya, kuna uwezekano wa kuongezeka kwa ghasia na uvunjifu wa amani, jambo ambalo linaweza kuathiri sio tu wale wanaohusika moja kwa moja, bali pia jamii nzima.

Kama hali hii itaendelea, inaweza kupelekea mabadiliko katika sera za usalama na utawala. Serikali inaweza kujikuta ikilazimika kuboresha mawasiliano yake na raia, pamoja na kubadilisha mbinu za kikazi za polisi ili kujenga uhusiano mzuri na wananchi. Aidha, kuna uwezekano wa kuanzishwa kwa mijadala ya kitaifa kuhusu haki za raia na wajibu wa vyombo vya usalama, ili kujenga mazingira ya kuaminiana na ushirikiano.

Soma Pia:

Kwa upande mwingine, ikiwa serikali haitachukua hatua za haraka kujibu malalamiko ya raia, inaweza kujikuta ikikabiliwa na maandamano zaidi na upinzani mkali. Hali hii inaweza kusababisha mgawanyiko katika jamii, ambapo kundi moja linaweza kujiona kama lina haki zaidi kuliko jingine, na hivyo kuathiri umoja wa kitaifa.

Kwa kumalizia, hali ya raia kuzuia polisi kukamata watu Tanzania ni ishara ya mabadiliko katika mtazamo wa raia kuhusu utawala wa sheria. Ingawa ni hatua inayoweza kuashiria uhamasishaji wa raia, ni muhimu kwa serikali na jamii kukabiliana na hali hii kwa njia ya amani na majadiliano ili kuhakikisha usalama na utulivu wa nchi unadumishwa.
 
Attachments

  • 354506.jpg
    354506.jpg
    14.5 KB · Views: 1
Back
Top Bottom