Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani CAG ni mpemba?CAG anafiti hapa
I see.Tanzania ni nchi isiyo na dini rasmi, na mtu anatakiwa kupata urais kwa uwezo, si kwa dini.
Nyerere katika hotuba yake moja alisema hata mtu asiye na dini anaweza kuwa rais.
Kuhesabu miaka ya kupata rais m Protestanti ni kuchochea udini.
Kosa kubwa la watanzania ni kufanya mabadiliko kupitia CCM matokeo yake ni watu wale wale wanaoharibu na kutengeneza.Kumbuka upatikanaji wa nyerere ulitokana na shirika LA Roma hata kumwandaa na mprostanti aliandaliwa na mariale mangi ila ikashindikana na kwa kupokezana mfumo wenyewe umeandaa watu kwa miaka kumi kumi,ccm wamegawa miaka hiyo kwa mifumo ya kiutawala wariberali miaka kumi then wajamaa miaka kumi
Kwa mfano mzuri wa hilo dude ccm tazama taifa LA marekani utaelewa vizuri
Siri gani? Kivipi?I see.
Kuna siri kubwa sana nyuma ya pazia sio kama unavyoona na kusikia.
Katiba inafuatwa ?Siri gani? Kivipi?
Mimi naandika kuhusu sheria na katiba ya nchi, si kuhusu innuendo.
Kwa hiyo kuongea udini ni kitu kizuri?Katiba inafuatwa ?
Je, inavunjwa kwa manufaa ya nani?
Je,katiba inasemaje juu ya mgawanyo sawa wa madaraka?
Hivi Leo akiingia Mkuu mdini au mkabila utamjuaje kwa kuangalia katiba?
Akija Mkubwa akaamua kuibadili hii nchi iwe ya dini yake na iongozwe kwa misingi ya dini yake nani atamzuia?
Kuna mtu anayeweza kujadili uteuzi wa mkubwa?
Ataanza tu kwa kumtafuta mkubwa wa wajeda wa dini yake ,mkubwa wa wandava wa dini yake, mkubwa wa wavaa suti nyeusi wa dini yake , mkubwa wa pesa wa dini yake , mshitaki mkuu wa dini yake, mkubwa wa modi wa dini yake, wakubwa wa kila idara wa dini yake ,vyombo vya habari vinakua na wapambe wa propaganda wa dini yake n.k.
Watu wakinungunika wataambiwa kwani hawa sio watanzania wenye sifa stahiki?
Wakitokea watu wa kupinga hadharani basi pyuu pyuu inawahusu na magereza na mabomu ili kuhakikisha hakuna anayefurukuta.
Nani asiyeogopa risasi.?
Katiba inayompa mtu mmoja maamuzi ya kuamua chochote bila kuhojiwa wala kuulizwa ni hatari sana.
Ndio maana wanaamua kuficha siri zao wanazojua zitawasaidia kulinda yale wanayoyafanya ambayo kiujumla ni kwa manufaa yao kwanza.
Anaweza akahamishia hata ikulu Pemba na hakuna a wa kuuliza.
Akiondoka anakua ameshajipanga ndani ya mfumo kuweka maslahi yake.
Katiba inapaswa iweke mipaka kabisa ili watu wahoji na ikigundulika kuwa kuna upendeleo au ubaguzi basi mahakama inatengua na mkubwa anaheshimu.
Vinginevyo kwa sasa tunaenda tu kwa kudra za mwenyezi Mungu lakini iko siku kwa katiba hii hii yatafanyika mambo ya ajabu sana na watu watakua wamechelewa.
Hukusikia RPC Kule Arusha akiwa muhamasishaji mkubwa wa CCM wakati katiba inamkataza.
Nani anapaswa amwajibishe bila shaka ni yule yule anayepigania chama chake kishinde ndio maana walimshangilia mtu anayevunja katiba.
Sio kitu kizuri kabisa ndio maana tunaonyedha kuwa Katiba ina Loophole la kuweze mtu mmoja kuweza kujenga himaya ya kiduni na akafanikiwa.Kwa hiyo kuongea udini ni kitu kizuri?
Unaelewa kwamba unaunganisha hoja mbili ambazo hazina muunganiko?Sio kitu kizuri kabisa ndio maana tunaonyedha kuwa Katiba ina Loophole la kuweze mtu mmoja kuweza kujenga himaya ya kiduni na akafanikiwa.
Uganda kama sio majeshi ya Tanzania kuivamia na kumtoa Amin ilikua inaelekea kubaya.
Mtu mmoja kupewe mamlaka makubwa kuliko Mungu nu hatari zana endapo ataamua kufuata itikadi anayoona ni nzuri.
Anaweze pia akafuta dini zote na kuamuru vitabu vyote vya dini vitiwe moto.
Ukipinga dawa yake ni kukutanguliza mbele tu.
Haya Leo hayapo hapa kwetu lakini tumeona jinsi waafrika walivyo Urahisi kutawaliwa kwa fikra za mtu mmoja na kuvunja katiba anavyotaka kupitia wateule wake wasiohojiwa.
Yani mtu mmoja anaweza kuteua watu katili sana na wanye hulka kama yake na wakatuka kufanya anachotaka na nchi nzima ikaufyata.
Hivi ukanipa Ukubwa wenye kuteua nafasi zote za kutafuna Keki ya nchi halafu nikaamua watu wote nitakao wateua lazima wawe na imani kama yangu au watakaounfa mkono imani yangu nani atanizuia kama katiba haisemi kuwa anaweza kuuzwa na hata uteuzi wangu kupingwa kwa data za upendeleo?
Nikiulizwa nitasema nchi haina dini na nimeangalia vigezo sio imani.
Na nitasema anayehoji hoji akamatwe mana ni mchochezi anayetumiwa na mabeberu.
Ukiandamana unakula chuma.
Watu wanaufyata na katiba haisemi chochote kuhusu teuzi.
Tusiipuuze Demokrasia na katiba inayowapa wananchi mamlaka yao ya kuwahiji viongozi wao.
IPO siku Afrika tutaelewa japo kwa kuchelewa
Udini unaweza ukajengwa ndani ya Mwaka mmoja tu na nchi ikawa ya dini anayomusudia mtu mmoja kama katiba inampa mamlaka makubwa ya kimungu.Unaelewa kwamba unaunganisha hoja mbili ambazo hazina muunganiko?
Udini na loopholes za kikatiba hakuna uhusiano.
Katiba ingesema rais wa Tanzania ni lazima awe Mkristo Mkatoliki, hapo ungekuwa na justification ya kuhusisha mapungufu ya katiba na udini.
Katiba haijali dini ya mtu.
Utaingizaje mambo ya udini kwenye mapungufu ya kikatiba?
Unaelewa kwamba kama katiba inampa rais nguvu sana, hapo kuna tatizo la katiba kumpa nguvu sana rais, hakuna katiba kuwa na udini?
Kwa hiyo unakubali matatizo ya katiba kuvunjwa/ kuwa dhaifu yako immediate zaidi ya matatizo convoluted ya udini?Udini unaweza ukajengwa ndani ya Mwaka mmoja tu na nchi ikawa ya dini anayomusudia mtu mmoja kama katiba inampa mamlaka makubwa ya kimungu.
Kuendelea kutegemea busara ya mtu mmoja ni hatari sana.
Ni lazima kila mtu awekewe mipaka na breki .
Ili isitokee mtu akaamua kuendesha nchi kama serikali iliyotokana na mapinduzi.
Nakupa mfano tu:
Hivi unafikiri kama awamu ile Chama kikubwa waliyoweka mahakama ya dini kwenye Ilani yao wangekutana na Rais Mdini na Mkatili,asiyetoa nafasi kukosolewa wala kupangiwa ingekuaje ?
Yani Maaskofu waliokua wanakaa vikao na kumpinga kwa nyaraka Mbalimbali na midahalo na maandamano na vitisho kuwa akiileta ile mahakama watamtoa madarakani angeamua tu kutumia Uamiri Jeshi wake mkuu na kuwasukuma ndani wote na kuzitumia ipasavyo bunduki nani angehimili risasi kutetea katiba ?
Kwanza angemchagua waziri wa Katiba na sheria mwenye mrengo huo.
Mkuu wa wambongo wa mrengo huo.
Mkuu wa wajeda wa mrengo huo .
Mvaa suti mrengo huo.
Spika mrengo huo.
Wabunge wanye midomodomo timua.
Zima TV zote na mitandao.
Hakuna wa kuhoji ,ukihoji wanajitokeza washabiki wake wanakuteka fasta.
Sheria za dharura na kuongeza kipengele cha mahakama ya dini kwenye Katiba na kisha kutangaza nchi ya dini.
Na hofu kuu kutanda
Nani angehoji ?
Kama sio ustarabu tu na kuheshimu katiba lakini ipo wazi kabisa kuwa bila kuwa na katiba mpya hii kusema nchi haina dini na ukabila tunajidanganya sana mana hata akiwa mkabila sio lazima atangaze kuwa nchi sasa ni ya kikabila au kidini . Yananafasi kubwa kufanyika kimya kimya watu wakayaona kwa vitendo na wakijaribu kusema watazuiwa na kipengele cha kumpa mkubwa mamlaka ya kufanya anachotaka bila kuhojiwa .
Ukiendelea kuhoji utaitwa mchochezi.
Kusema kuwa katiba haina dini bila kuweka namna ya kudhibiti mtu yeyote asije akajaribu kuliingiza taifa kwenye udini ,ni kujidanganya.
2005 Chama kikubwa kwenye ilani yake kiliingiza udini mwenye kampeni bahati nzuri mgombea wake alikua hana hulka ya udini lakini walifanya walifanya hivyo mana Hakuna kipengele kwenye katiba chenye uwezo wa kumbana Mwenyekiti wa Chama ambaye alikua ni mkuu wa nchi aliyeruhusu hayo kufanyika wakati wa kuandaa ilani hiyo.
Na ni wazi kabisa bila katiba mpya watu wameshaona kuwa kumbe inawezekana kabisa ukishika kiti kikubwa na chama basi unaweza kufanya chochote na hakuna wa kukugusa wala kukuhoji.
Ni sawa katiba kusema hii nchi ni ya kijamaa wakati viongozi wote ni mabepari.
Ni maneno tu lakini hakuna uhalisia kivitendo.
Nadhani hujanielewa na hutaki kunielewa.Kwa hiyo unakubali matatizo ya katiba kuvunjwa/ kuwa dhaifu yako immediate zaidi ya matatizo convoluted ya udini?
Tuna katiba dhaifu inyomruhusu rais kuwa na nguvu za kifalme.Nadhani hujanielewa na hutaki kunielewa.
Udini upo chini chini kwa sababu malalamiko yapo chini chini.
Tofautisha Udini kwenye utawala na utawala wa kidini.
Ukabila kwenye utawala na Utawala wa kikabila. Ni vitu viwili tofauti.
Utawala wa kidini unazaliwa na Udini kwenye utawala.
Utawala wa Kikabila unazaliwa na ukabila kwenye utawala.
Kuzuia Utawala wa Kidini au Kikabila ni lazima nchi iwe na katiba inayozuia mianya ya kuunda ukabila au udini kwenye utawala.
Kwa Katiba tuliyonayo inayosema tu hii nchi haina dini bila kuweka mipaka ya kidhibiti watawala wasiwe na dalili yoyote ya upendeleo katika suala LA Dini na kabila na hata ukanda ipo Siku atatokea mdini kweli kweli na atatumia mamlaka yake kikatiba kuifanya nchi yetu iwe ya kidini na hakuna atakayeweza kumzuia.
Tumeona Mara nyingi hakuna anayeweza kumzuia mkubwa wa nchi za Afrika mana Mara nyingi ndiye pia mkubwa wa Chama chake.
Mbele ya Pyupyuu hakuna atakayesimama na kutetea katiba mana imekataza lakini haijaweka breki kwa anayeweza kuidumbukiza nchi kwenye Utawala wa kikabila,kidini na kikanda naupendeleo mwingine.
Hivi unajua ni kwa nini miaka ya nyuma kuna vyama viliwahi kuitwa vya kidini wakati wa Uchaguzi?
Vingine vikaitwa ni vya kikabila?
Waliojawa na hofu walikua ni wale waliokua madarakani . Kwa nini walijawa na hofu wakati katiba hairuhusu kutawala kidini wa kikabila ?
Bila shaka walijua kuwa kwa mwaka mmoja nchi ingeweza kugeuzwa kwa kutumia katiba hiyo hiyo isiyo na mpaka kwa mkubwa.
Lakini Udini au ukabila au Udini unakoma hata kama nchi itatawaliwa na Askofu au shekhe endapo kuna katiba inayombana Mkuu wa nchi.
Mfano pawe na Kamati maalumu inayoundwa na Bunge kwa ajili ya kujadili Uteuzi wa Rais na baada ya kuuchambua unapelekwa bungeni kujadiliwa kama kuna pingamizi dhidi ya mteule au kama kuna mwananchi au taasisi ya dini yenye malalamiko iwasilishe kwenye kamati.
Mfano; inatokea Mtu mmoja anateua 98% ya wakuu wote wa idara wa dini yake wakati nchi ina dini kwa asilimia zinazolingana au kukaribiana. Nani atazuia hilo mana halipo nje ya uteuzi wa kikatiba.
Nadhani atakayehoji ndio ataitwa mdini na mchochezi .
Je, dini nyingine haitakua na haki ya kunungunika kwa sababu tu katiba inasema nchi haina dini? Je, nini kitafuata endapo mtu atateua 98% ya watu wa dini au kabila lake kama sio baada ya muda kuanza kubadili baadhi ya sheria ?
Ukirudi kwenye Chama anakata kila asiye wa dini yake au kabila lake na kupitisha wa kabila lake au dini yake.
Ukihamia upinzani unakutana na Mkurugenzi mwenye maelekezo anakunyima form ya uchaguzi.
Ukilalamika unakutana na Msajili na Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi wa dini Yake au kabila lake anatupilia mbali malalamiko yako.
Nchi haijaenda kama anavyotaka mtu mmoja iwe ni kidini au kikabila?
Katiba isitoe mamlaka makubwa sana kwa MTU mmoja mana ndipo wanaotamani Udini na ukabila wanapopapenda .
Tuna katiba dhaifu inyomruhusu rais kuwa na nguvu za kifalme.
Kwa nini udini uwe na sehemu muhimu ya kusemwa kuliko kitu kama, matumizi mabaya ya fedha za umma yasiyofuata mpango?
Ukisema udini Magufuli anaweza kukuambia makamu wake na waziri mkuu ni waislamu, na yeye hajawahi kuwa na shida kuteua waislamu.
Ukimbana kwenye matumizi mabaya ya fedha za umma bila kufuata bajeti wala tenda unaweza kuwa na case strong zaidi.
Utasemaje mtu akikuambia hivyo?