Hatma ya Shilole mikononi mwa BASATA

mtz daima

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2015
Posts
1,561
Reaction score
579
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini limeona picha chafu na zisizo na maadili za Msanii Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole alipokuwa akifanya onesho lake nchini Ubelgiji hivi karibuni.

Katika picha hizo ambazo zimelaaniwa na watanzania wengi nchini kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, Shilole anaonekana akiwa Jukwaani huku viungo vyake vya sehemu za siri vikiwa hadharani na zaidi akionesha tabia ambazo kwa kiasi kikubwa zimefedhehesha na kuidhalilisha sekta ya Sanaa na Taifa kwa ujumla.

Aidha, BASATA limepokea malalamiko kwa njia ya simu na mawasiliano ya internet kutoka kwa watanzania waishio ughaibuni wakilaani tukio la Msanii huyo. Katika mawasiliano yao wameeleza kwamba wamefedheheshwa na kudhalilika na tabia hiyo chafu iliyooneshwa na msanii huyu.

Ikumbukwe kwamba, Shilole ni msanii aliyesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa, hivyo anapokwenda nje ya nchi kabla hajapata visa anapewa barua ya utambulisho kama msanii wa Tanzania, hivyo anapokuwa nje ya nchi anatambuliwa kama msanii Mtanzania, anapofanya kinyume na misingi ya kazi ya Sanaa, anajifedhehesha yeye mwenyewe, kazi ya Sanaa na nchi yetu pia.

Aidha, ikumbukwe kwamba BASATA limeshapata kumwita na kumuonya msanii huyu kutokana na tabia yake ya kutokujiheshimu pale awapo jukwaani na yeye aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo chafu. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio hayo na kwa sasa katika ardhi ya nchi nyingine ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu Sanaa kama kazi nyingine.

BASATA linapenda kueleza kwamba;
1.Litamuita kwa mara nyingine tena kumtaka ajieleze kwa nini alifanya onesho hilo la kujidhalilisha na kudhalilisha hadhi ya mwanamke, msanii na Sanaa kwa ujumla
2.Kama maelezo yake hayataridhisha hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake maana tayari ameshadhihirisha kwamba akifanyacho si Sanaa na hakina uhusiano na kazi ya Sanaa ambayo ina heshima yake na inahitaji ubunifu, weledi na kujitambua.

BASATA linawakumbusha wasanii wote nchini kuwa Sanaa ni kazi kama kazi zingine lakini siku za hivi karibuni wasanii wengi wamekuwa wakikiuka suala zima la maadili kwa kutengeneza kazi chafu zisizofaa mbele ya jamii ya watanzania wanaoipenda na kuiheshimu kazi ya Sanaa yenye staha. Tuungane kwa pamoja kukemea kazi chafu zinazozalishwa na wasanii wasiojitambua kwani suala la maadili ni suala mtambuka na linaanzia katika ngazi ya familia.

Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapopata mialiko ya kikazi kwenda nje ya nchi. Linawakumbusha kwamba haiwezekani msanii kutumia picha chafu na mavazi dhalili na kuonyesha utupu katika kuvuta mashabiki.

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini.

My take: Wasanii wengine wenye malengo makubwa kama Vmoney, Dmondi nk. wajitathmini

Chanzo: Michuzi
 
Huyu Shilole wamfungie kwanza miezi ka sita hivi ili atie akili kazidi kujizalilisha na kuonyesha nyeti zake wakati ni fedheha kwa wanawake wote kuonyesha kiungo sensitive .
 
Jamani Basata hilo ni uonevu huo ni mwili wake ana haki ya kuutumia anavyotaka mmemuona Shilole tu, kigodolo hamjakiona mpaka mnamuadhibu shilole!
 
Kosa amelifanyia nje ya nchi, acha sheria za huko zifanye kazi. Huku atafundwa tu aache upuuzi wake.
 
Jamani Basata hilo ni uonevu huo ni mwili wake ana haki ya kuutumia anavyotaka mmemuona Shilole tu, kigodolo hamjakiona mpaka mnamuadhibu shilole!

Kweli kabsa basata waachee njaa mbona kina rihana atujawahi kusikia hii mizengwee
 
Kabla ya kuhukumiwa, watutumie video ya tukio ili tujilidhishe kama nyonyo zilitoka zenyewe , au alikuwa anaigiza utamaduni wa south africa, au mehemuko. Inawezeka sana zile sindilia za kukaba matiti yaonekane saa sita ziliiachia ghafla baada ya kuruka juu huku akiserebuka, unajua wakina dada wanayakaba sana maziwa kiasi kwamba akijisahau likakimbia kwenye ling inakuwa shidahh.
 
Kosa amelifanyia nje ya nchi, acha sheria za huko zifanye kazi. Huku atafundwa tu aache upuuzi wake.

Huko nje hata utembee uchi hakuna mwenye mpango na wewe. Mfano Australia kuna siku maalum watu kubaki uchi kabisa
 
jamani basata mwenzenu bra ilishuka bahati mbaya...kaaaaah!!! kwanza biashara matangazo...

Unamaanisha biashara ipi mkuu yeye alipewa leseni ya muziki hivyo kutangaza viungo vyake ni kwenda kinyume na masharti ya leseni yake. Ova
 
Huyu Shilole wamfungie kwanza miezi ka sita hivi ili atie akili kazidi kujizalilisha na kuonyesha nyeti zake wakati ni fedheha kwa wanawake wote kuonyesha kiungo sensitive .

Ni dalili ya kuishiwa ubunifu ila pesa mbaya sana jamani hivi mpenzi wake nu.hu si alikuwa nae? Kwanini hakumshauri kama kweli anampenda
 
Jamani Basata hilo ni uonevu huo ni mwili wake ana haki ya kuutumia anavyotaka mmemuona Shilole tu, kigodolo hamjakiona mpaka mnamuadhibu shilole!

Haonewi ndugu yeye alipewa barua yenye nembo ya bibi na bwana ikimtambulisha kuwa msanii toka Tanzania siyo mwonesha nyeti hahaaa.
 
Ni dalili ya kuishiwa ubunifu ila pesa mbaya sana jamani hivi mpenzi wake nu.hu si alikuwa nae? Kwanini hakumshauri kama kweli anampenda

Shilole hana aimbalo na hajui mziki sasa ili kupata kiki anaona afanye vituko vya kujiacha wazi ili azungumzwe kumbe ndo anazidi kujizalilisha. Sio Mara moja kuna siku alipost kashikwa nyonyo hadharani bila hata braa na nuhu nyingine makalio. Nahisi watakua wanavuta bangi si bure hata kama ni Uhuru wa kufanya mambo hawa wamezidi wehu kabisa.
 
Kweli kabsa basata waachee njaa mbona kina rihana atujawahi kusikia hii mizengwee

Basata hawana lolote mbona hata huku Tanzania alikuwa anacheza hivyo, hiyo ni chuki ya watanzania wanaoishi ughaibuni kujidai wanajua kulinda mila na desturi za kitanzania wakati wao ndio wanaiga mambo ya ughaibuni, huo wote ni wivu, wamuache ajitafutie pesa hiyo ni biashara hakuna mtu atakayemsaidia shida zake, mimi nasema aendelee aonyeshe mpaka papuchi ni mali yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…