Hatma ya Ukraine itakuwa mikononi mwa Urusi

Hatma ya Ukraine itakuwa mikononi mwa Urusi

Subiri ngoma bado mbichi July hii Putin ataanza kupata majibu yake

Maandalizi ya kivita ya uhakika huchukua muda mrefu .Kuanzia julyl hii Putin lazima ataita maji mma
Hizi kauli kila mwisho wa mwezi mnaziongea "vita Bado mbichi", "ngoja mwezi unaokuja putin atakiona".....blah blah
Hadi mlisema putin amekufa ,hatoboi huu mwezi
kitu unachotakiwa kukumbuka muda wote Russia ni super power country na kuingia nae vita is too much risk ndio maana NATO Bado wanazikoki bunduki zao tu hadi leo
 
Hatujasahau mauaji ya waislam maelfu huko Serbia yaliongozwa na Ukraine walibaka wanawake na kuua watu, waislam bado wanahasira na hiyo nchi ya kishoga ndio maana chenchnia wamejitoa mhanga kuwa upande wa mrusi kulipa kisasi dhidhi ya ufedhuli uliofanywa na hao mashoga
Akili sawa? Mauaji ya Waislamu Serbia, Kosovo na Bosnia yalitekelezwa na Waserbia, hasa wale ambao leo wanamwunga mkono Putin na kupokea ahadi zake za urafiki.
Ukraine ilikuwa na nini katika sehemu za Yugoslavia? Wapi? tarehe gani?

Ukitaka kona Putin aliua Waislamu wapi - angalia Chechniya. Alitumia uwongo kuhusu "ugaidi" wa Chechniya kujenga mamlaka yake katika Urusi. Bwana Litvinenko (aliyesumishwa baadaye na Putin) alieleza jinsi gani polisi ya siri ya Putin ililipusha mabomu katika miji ya Urusi ili kumpatia waziri mkuu Putin nafasi kuanzishavita dhidi ya Chechniya na kwa njia hiyo kuonekana kama shujaa ili ashinde uchaguzi wa Urai mwaka 2000. Wachechniya 50,000 waliuawa kwa mafinikio ya Putin.
 
Subiri ngoma bado mbichi July hii Putin ataanza kupata majibu yake

Maandalizi ya kivita ya uhakika huchukua muda mrefu .Kuanzia julyl hii Putin lazima ataita maji mma
Ni kweli. Kwa sasa Ukraine imetumia asilimia kubwa ya grenedi zake; ilhali mizinga mingi ni za Kirusi za mm 152, Ukraine haiwezi kutumia grenedi za NATO 155 mm kwa mizinga hii. Hapa changamoto kupata mizinga ya kutosha kutoka nchi za NATO pamoja na grenedi(ambazo no bora kuliko ile ya Urusi). Na pia kujifunza kuzitumia - kwa zile Panzerhaubitze 2000 kutoka Uholanzi na Ujerumani wanajeshi wa Ukraine walifundishwa mwezi 1 kule Ujerumani.
Urusi ina akiba kubwa sana, hata kama ni silaha za zamani.
Tutaona kama muda unatosha kupata silaha mpya na kufundisha matumizi yake, maana jinsi ilivyo Putin atandelea kusogea mbele polepole akiharibu kila kitu kilichopo njiani.
 
Subiri ngoma bado mbichi July hii Putin ataanza kupata majibu yake

Maandalizi ya kivita ya uhakika huchukua muda mrefu .Kuanzia julyl hii Putin lazima ataita maji mma
hatimaye July imeisha sasahivi ni september tunaingia October mzee baba the Putin anaenda kuikalia rasmi Donbass
 
hatimaye July imeisha sasahivi ni september tunaingia October mzee baba the Putin anaenda kuikalia rasmi Donbass
Anaikalia wakati wanajeshi wake wanakimbia kama wehu kutoka vita kwa kipigo cha makombora ya Himars. Yaliyotolewa na Mmarekani
 
Na Masudi Rugombana June 27, 2022. Goba, Dar es salaam.

Tarehe 21 February 2022 Rais Vladmir Putin wa Urusi alitangaza kutambua uhuru wa eneo la Donbass, Jimbo la Mashariki ya Ukraine linaloundwa na mikoa miwili ya Luhansky na Donetsky, mikoa inayokaliwa na idadi kubwa ya Raia wenye asili ya Urusi. Mikoa hii ilijitangazia uhuru kutoka Ukraine mwaka 2014 kutokana na kura ya maoni iliyoongozwa na makundi ya wapiganaji kufuatia mgogoro wa kisiasa uliozusha maandamano makubwa yaliyomuondoa madarakani Rais Viktor Yanukovych kiongozi aliyeegemea zaidi upande wa Urusi hatua ambayo Rais Vladmir Putin aliifananisha na mapinduzi ya kijeshi. Kuondolewa madarakani kwa Victor Yanukovych kulifuatiwa na maandamano makubwa ya makundi ya watu wanaounga mkono Urusi huko Mashariki na kusini mwa Ukraine ambapo mkoa wa Crimea wenye idadi kubwa ya Raia wenye asili ya Urusi uliitisha kura ya maoni iliyopelekea wakazi wake kuchagua kujiunga na Urusi hivyo kuipa uhalali Urusi kuitwaa Crimea na kuifanya eneo lake.

Tangazo la Putin kutambua uhuru wa Donbass lilifuatiwa na uingiliaji kati kijeshi tarehe 24 February 2022 katika Operesheni inayokusudia kuvunja nguvu za kijeshi za Ukraine na kuondoa matendo ya kikatili yanayofanywa na wapiganaji wa jeshi la Ukraine wenye siasa kali za kizalendo zilizogubikwa na fikra za kinazi ( Operation demilitalize and denazify). Kiuhalisia, uvamizi wa Urusi nchini Ukraine una malengo mapana zaidi ya hicho kinachoitwa ukombozi wa Donbass. Ni uvamizi unachagizwa na mambo mengi ya kiusalama na kimaslahi yanayohusu Urusi zaidi ya kusudio la kuikomboa Donbass.

Baada ya umoja wa kisoviet kuanguka mwaka 1990, Umoja wa kujihami wa nchi za Ulaya Magharibi (NATO) ulijitanua kuelekea upande wa Mashariki na hatimaye kuyachukua mataifa ya eneo la Baltic, Jamhuri za Lithuania, Latvia na Estonia ambazo zilikuwa sehemu ya umoja wa Kisovieti (Soviet Union ) na kupeleka umoja huo wa kijeshi kujisogeza karibu na Moscow kwa kupakana moja kwa moja Urusi. Mwaka 2008 NATO iliweka wazi mipango yake ya kutaka kuisajili Ukraine. Ikumbukwe kuwa Rais Vladmir Putin aliwahi kusema kwamba kusambaratika kwa umoja wa Kisovieti lilikuwa ni janga kubwa katika karne ya ishirini lilipelekea Urusi kuporwa haki yake kama mojawapo ya Mataifa yenye nguvu kubwa Duniani. Putin ametumia miaka 22 madarakani kujenga upya jeshi la Urusi kwa lengo la kurejesha nguvu yake ya kiushawishi kwenye siasa, ulinzi pamoja na mahusiano ya kimataifa (Geopolitical clout).

Putin alishaweka wazi kuwa kujitanua kwa NATO kuelekea Mashariki sambamba na mkakati wake wa kuisajili Ukraine kwamba ni kitisho kisichovumilika dhidi ya Urusi, akilaumu uwepo wa vikosi vya Marekani na makombora yao kibalistic ya masafa Marefu nchini Ukraine, huku akisisitiza kuwa Ukraine ni sehemu muhimu ya Urusi kisiasa na kiutamaduni.Hivyo basi kutokana na tishio la NATO, Urusi iliamua kuongeza nguvu za kijeshi kuelekea upande wa Magharibi kwenye mpaka wake na Ukraine kwa lengo moja tu ambalo ni kufanya shambulizi (Pre-emptive strike) dhidi ya Ukraine kwa lengo la kujihami dhidi ya kitisho cha NATO. Katika jithada za kuepusha vita, NATO na Ukraine walitaka Urusi kuacha kujijenga kijeshi kwenye mpaka wake na Ukraine hivyo kufungua meza ya majadiliano baina ya pande mbili. Urusi ilitoa masharti makuu matatu ili ombi hilo la NATO liweze kutekelezwa.

1. Ipewe hakikisho kwamba Ukraine haitajiunga na NATO.

2. NATO iondoe vikosi vyake katika nchi za Ulaya Mashariki.

3. Jeshi la Ukraine Kusitisha mapigano kwenye eneo la Donbass kwa mujibu wa makubaliano ya Minsk ya mwaka 2015 ambayo yaliweka masharti ya kuondolewa kwa silaha nzito kutoka kwenye uwanja wa vita, kuachiliwa kwa wafungwa wa pande zote mbili, na marekebisho ya katiba nchini Ukraine ikiwa ni pamoja na utoaji wa uhuru kwa mikoa ya Donetsk na Luhansk.

NATO na Ukraine waliyakataa madai yote ya Urusi, hivyo kupelekea Urusi kutokuwa na namna nyingine zaidi ya kulinda usalama wake kwa kuivamia Ukraine katika kile kinachoitwa oparesheni maalum ya kijeshi ( Special military operation) ili kuzuia isijiunge na NATO. Ni uvamizi mkubwa wa kijeshi barani Ulaya tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya Dunia. Lengo kubwa la Rais Vladmir Putin katika operesheni hii ni kurudisha Usawa baina ya Urusi na Marekani kwa kupunguza kitisho cha NATO.

Urusi chini ya Putin ikisimama peke yake dhidi ya Ukraine inayoungwa mkono na NATO kifedha na kijeshi inapigana kwa tahadhari kubwa, akili nyingi na kwa mipango na mikakati ya kueleweka. Jeshi lake linasonga mbele taratibu lakini kwa uhakika, likipiga hatua tatu mbele na kurudi hatua moja nyuma pale uwanja wa mapambano unapokuwa mgumu. Urusi inashinda kwenye uwanja wa vita, inapambana kwenye uwanja wa Diplomasia na inashinda kwenye kampeni kali ya vikwazo dhidi ya uchumi wake na hivyo kumkatisha tamaa Rais Volodymyr Zelenskyy na washirika zake kutoka NATO na Umoja wa nchi za Ulaya ambazo kwa kiasi kikubwa uchumi wao umeathirika vibaya kutokana na vikwazo vyao wenyewe wanavyoweka dhidi ya Urusi.

Kutekwa kwa miji muhimu kama Kherson na Mariupol lilikuwa pigo kubwa kwa Zelenskyy na NATO, lakini kudondoka kwa jiji la Severodonetsky, mji mkuu wa wakazi wa mkoa wa Luhansky wanaopinga kujitenga na Ukraine kunatuma ujumbe kwa Zelenskyy na mabwana zake wa Magharibi kuhusu uimara wa jeshi la Urusi na hatari ya Ukraine kugawanywa vipande viwili katika siku za usoni.

Kuna kila dalili kuwa Ukombozi wa Donbass hautakuwa mwisho wa uvamizi wa kijeshi wa Urusi nchini Ukraine, kwani lengo hasa la Putin ni kuhakikisha sehemu yote ya Mashariki na kusini mwa Ukraine inakuwa chini ya Urusi, hivyo basi kutekwa kwa mikoa mitano ya Kharkiv, Dnipropetrovsk, Zaporizhia, Mykolaiv na Odesa kuelekea Tranistria ni mojawapo ya malengo yajayo ya operation maalum ya kijeshi ya Urusi inayoendelea nchini Ukraine. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa mapigano kuendelea kwa muda mrefu.

Hatima ya Ukraine itaamuliwa na Urusi baada ya kuteka eneo la Mashariki na kusini mwa Ukraine, hapo ndipo itajulikana kama Ukraine itamegwa na kuanzishwa taifa jipya ama eneo hilo kuwa sehemu rasmi ya Urusi. Katika sakata hili la Ukraine ni dhahiri kuwa aliyeanzisha mapigano ndiye huyo huyo atakayeyamaliza mapigano naye siye mwingine isipokuwa ni Vladmir Putin.

Ukinakili Makala zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
[emoji2398] Copy rights of this article reserved
[emoji2400]Written by Masudi Rugombana

Napatikana kupitia[emoji116][emoji116][emoji116]
Email: masudirugombana@gmail.com
Simu: 0743 184 044
Unakili ujinga huu...Bora ungetoa jina ili kulinda heshima yako
 
Anamlinda au anamuogopa?
Biden ajaribu kutoa agongwe za uso.

Tunaenda kuchukua Oddessa
"Tunaenda kuchukua Oddessa" Alisikia mrusi mmoja kutokea kiwalani bombom

Ambae akisikia Panya road hao na bisibisi anatoka nduki ndala mkononi
 
Wanajeshi 44 wa urusi wauwawa huko Kherson siku ya jana tu🤔
The Ukrainian military said its forces had killed 44 Russian soldiers in the past 24 hours and had destroyed an ammunition depot. Chechen leader Ramzan Kadyrov admitted 23 of his soldiers were killed and 58 wounded in battle field
ukraine-kherson-russia-reinforcements-counteroffensive/32105018
 
Back
Top Bottom