Hatma ya Warioba mikononi mwa JK

The spectre of corruption thrown upon the unimpeachable person of Judge Warioba is not only regrettable, but also shamefully opportunistic.

The folly of this witch-hunt,apart from the fact that it is a thinly concealed fabrication, is that the Kikwete administration need Judge Warioba more than Judge Warioba need the Kikwete Administration.

Judge Warioba, a person of distinguished modesty, world class caliber of professionalism and renown integrity, is at the risk of being sacrificed at the political altar.

In Tanzania, people of the distinction of Judge Warioba are the last of a dying breed. Instead of using their experience and wisdom in the crucial matters of the country (e.g East African integration etc) we risk alienating these distinguished public servants with these petty unfounded and extremely regrettable charges.

Eti Umoja Entertainment! How sad!

Kikwete and his government, if at all this charade originates with them must know that they cannot gain credibility by these puppet show witchhunts, instead they must focus on the real issues, like bringing to court the Rostam Aziz's of thios country.

But that will never happen, since as amptly reported by the internationally reliable "African Intelligence" in 2005, Rostam Aziz bankrolled the Kikwete campaign and election with millions of US dollars.Kikwete has no moral standing to bring Rostam Aziz to justice and instead is attempting all types of circuses distract attention from this real issue.

On the other hand, this article being from Kubenea, and the officials not even acknowledging the charges, much is left to be desired.
 

Jasusi,
Kama umenisoma vizuri ni nimesema kabisa kuwa pale ambapo ushahidi wa kumfikisha mahakamani mtuhumiwa yeyote upo bila ya kujali sura yake ni vema tukapongeza hatua hiyo. Nitakuwa mnafiki leo hii nikisema kuwa Warioba asifikishwe mahakamani kwa sababu tu kuna mtu fulani hajafikishwa, no! Kukamilika kwa ushahidi wa Warioba kusiwekwe pembeni ati tu kwa sababu tunaowataka sisi bado. Tumwachie Mzee Warioba akajisafishe huko kwa pilato, na wengine watafuata.
 
Sioni sababu ya watu kupiga kelele na kuweweseka kwa Taarifa za kupelekwa Mahakamani Mzee Warioba...Inaweza kuwa ni kweli Warioba alikuwa anapiga kelele kuhusu Ufisadi kwa kujua kwamba yeye hatofikiwa na dhoroba hilo...."Hakuna asiyejua ushiriki wa Mzee Warioba kwenye Mwananchi Gold". Tukae kimya na tuone nguvu ya Mahakama...kwangu mimi najua Warioba atakwenda Mahakamani na kesi itapigwa dana dana bila kuisha,Lakini kwenda kwake tu Mahakamani litakuwa pigo jingine kwa CCM kwa sababu mambo mengi tuliyokuwa hatuyajui yatawekwa wazi huko.....Walio karibu na Mzee Mkapa na Vicent Mrisho wawaambie wakae sawa,nao watapitiwa na dhoruba hili!!Hakuna aliye juu ya sheria.
 

- Mkulu Mwawado, heshima mbele sana, hapa umenena neno la msingi sana, similar na alilowahi kuniambia waziri mmoja, kwamba the ishu sio kufunga wakina Warioba na the likes, isipokuwa ni kuleta heshima kwa utawala wa sheria, viongozi wetu walikuwa wamejisahau sana sasa ni vyema wakumbushwe kuwa Tanzania hakuna aliye juu ya sheria, ishus za sheria sio za majukwaa ya siasa ni sheria tu kupitisha mkono wake regardless of what are the politics of Warioba as a person or as a retired leader.

- Ujumbe ni hakuna aliye juu ya sheria.

Respect.

FMEs!
 
Hatma ya JK haimo mikononi mwa mtu yeyote bali wananchi wa Tz.No body is bigger than wananchi wa Tanzania na anayefikiria hivyo anajidanganya.
 

Mkuu wewe ni objective lakini hapa sikuelewi. Kwa nini unataka tutumie double standards kwa kosa lile lile? Unasema Warioba alikuwa mwenyekiti wa Tume ya kupambana na rushwa, do you think that makes him clean? Mkuu I personally simhukumu Warioba lakini..tujiulize...huyu mzee partner wake kibiashara ni Mahalu...ambaye sasa anatuhuma nzito za rushwa...show me his friends, I will tell who he is..the saying goes. Ukiangalia ukweli hii kampuni ya Mwananchi gold inaacha maswali mengi kuliko..majibu. Na in anycase..kwa nini tulie leo Mkapa au Lowassa wapelekwe Mahakamani, Lakini tutumie vigezo tofauti kwa wengine? Hatujawahukumu..waende wajisafishe mbele ya vyombo vya sheria.

Warioba kama hana kosa, he has nothing to fear but fear its self.

Ofcourse hakuna anayependa mtu makini kama Warioba ahusishwe na rushwa..lakini ndo hivyo nchi yetu imefika level hata tuliowaamini kuliko wote kama wakina Mkapa ndo wametutenda..sasa sioni kwa nini leo tuone Warioba kutuhumiwa iwe ni taboo. Anything can happen. And the court will give the verdict.

Hakuna anayesema kwamba Warioba ni guilty. The greatest thing we can do, ni kuvipa heshima yake vyombo vyetu vya sheria kuamua hatma ya mashauri kama haya. Tusiwe waoga. Tunavyolilia utawala wa sheria, wakina Warioba kupewa haki yao mbele ya hivi vyombo ndo sheria yenyewe. Kwamba RA et al hawajapelekwa mahakamani..halihusiani na Warioba. Nao siku yao itafika. Kwa sasa let the law take its course.

Masanja,
 

Ni vyema kuheshimu mawazo ya wenzetu lakini naamini mawazo kama haya hayatujengi. Jamani eti KIKWETE (rais wa watanzania) anamhitaji Warioba than the way he needs him? Please......Who is Warioba? Man, no pun intended..Lakini Joe is just another private citizen who did his part in serving our country when he had a chance to do so. He is neither indispensable nor irreplaceable. Hakuna kiumbe indispesable katika nchi yetu. Hayupo. Hata ukifa leo watu watalia leo na kesho na utakuwa historia.

Kama alivyosema Mwawado, wazee kama hawa hawakujua iko siku sheria walizozipitisha zitawashughulikia wao. Hakuna which hunt hapa..swala ni kwamba wazee wanagawiana mali za watanzania kama za kwao kwa sababu wanajua hakuna wa kuwagusa..I tell you..malipo ni hapa hapa ulimwenguni..na huu ndo ukweli si dua la kuku.

Let Warioba be cleared by a competent Court. Tuache kusentimentalize hii issue. Let the law do its things.
 

Usitake kumsafisha Warioba kana kwamba wewe ndio Papa Paulo mtangaza watakatifu. Warioba alishawahi ku trivialize vita vya ufisadi. Na akadai viongozi ni sacrosanct, hatutakiwi kuwatuhumu. "Unimpeacheable" my foot!

JOSEPH WARIOBA: “Unapomtaja rais kama fisadi unakuwa na unataka kufanya wananchi wakose imani na serikali yao, suala ambalo ni hatari, wananchi watakimbilia wapi kama wanayetaka kumkimbilia naye anachafuliwa?... Mengine yanashitusha. Umoja wa nchi hii unaweza kufika mahali pabaya. Yaani rais anaitwa fisadi kwa sababu hizi na zile tu...

“Tunaanza kuwa na utamaduni wa kutafuta dosari hasa za viongozi na kusahau mambo ya msingi ya kulisaidia taifa....”
 

Jasusi, hao mapapa wa mafisadi akina Manji, Rostam, Subhash, Chavda hawawezi kuguswa kabisa maana wanajua uchafu wote uliofanywa na Kikwete na wanamtandao katika kutoa rushwa kwa wajumbe ili kuhakikisha Kikwete anaingia Ikulu.

Wahindi walivyokuwa smart kwenye kutunza nyaraka muhimu watakuwa na ushahidi wote na pindi wakiguswa tu na wao kuamua kuondoka na mtu basi pale Ikulu patakuwa hapakaliki ndiyo maana bado wanaendelea kupeta uraiani bila matatizo yoyote.

Sijui ni kigezo gani alichotumia Mkurugenzi wa Mashitaka mpaka kufikia uamuzi wa kuifikisha mahakamani kesi ya Warioba kwanza kabla ya ile ya Kagoda. Warioba inasemekana alichota bilioni 6 na Kagoda ilichota bilioni 40 ambazo ni zaidi ya mara 6 ya zile zinazosemekana kuchotwa na Warioba.

Kwa maoni yangu kesi ambayo ingepewa priority ya kuifikisha mahakamani kati ya hizi mbili ingetakiwa iwe ya Kagoda kutokana na kiasi kikubwa kinachohusiana na ufisadi wa Kagoda. Labda DPP huwa anaamua tu kesi ipi ifikishwe mahakamani bila kujali uzito wa kesi alizonazo.
 
Is it possible kwamba Warioba anakataa mahojiano na kubenea? Mbona mara zote habari za kupelekwa mahakama kwa warioba zinatokea kwa kubenea? Inawezekan kuandika habari ya upande mmoja ukawa hujavunja maadili ya uandishi? je mahakama ya Tz iko mbali kiasi gani mbona wafuasi wa chikawe hawafiki, siku zote KUPELEKWA, KUPELEKWA?

Wanajamii! Hili swala halifai kutugonganisha vichwa, tulisuburie lifike mahakamani.
 


Wakuu naheshimu sana maoni yenu. Lakini kama tukiwa tunaitakia mema Tanzania lazima tuwe wakweli na tusiwe wanafiki. Ni kweli katika hali ya kawaida inatakiwa kusiwe na alie juu ya sheria, lakini ukweli ni kuwa kuna wachache waliojuu ya sheria. THIS IS A FACT, inaonekana kuwa Warioba si mmoja wa aliyejuu ya sheria. Kama kuna waliotuhumiwa kama yeye, na kuna ushahidi wa kuwafikisha mahakamani kama yeye ili wa-prove innocence yao, ambao walianza kuchunguzwa before Warioba, kwanini yeye awe wa kwanza kufikishwa mahakamani? Kwanini yeye apewe nafasi ya ku-prove innocence kabla ya mapapa wengine waliochunguzwa mwanzo na mafaili yao yako mezani hawajapewa nafasi ya ku-prove innocence? Au kwa sababu yeye hakuwa mwanamtandao au vipi, au kwa sababu alinza kuwakemea mafisadi?.

Tunafahamu kuwa utawala wa sheria Tanzania una apply pale vidagaa vinapokuwa na matatizo, ukiiba kuku au ukiiba mbuzi au ukikanyaga nyanya ya watu, lakini ukikwapua mabilioni kama walivyofanya mafisadi wachache hakuna utawala wa sheria kuna "utawala wa sheria". Tunakumbuka simple case ya Ditto, nani asiyejua kuwa sheria ilibanangwa, kuna jambazi moja lili-confess kuwa ni jambazi eti likasamehewa, kuna kijana alimpiga kofi mzee mwinyi alihukumiwa kwa vipigo palepale, mbele ya kadamnsai, ndio utawala wa kisheria huu?

Sitaki kusema kama Mzee Wariona ni innocent au hapana. Lakini tusiseme kufikishwa kwake mahakamani kutaonesha jinsi tunavyofuata kanuni ya utekelezaji wa sheria kwa usawa.
 


- Mkuu siku hizi vipi mbona huyu kama sio wewe? Yona na Mramba wameshatinga Kisutu, njia imeshafunguliwa sasa hakuna wa kupona na it is just a matter of time, kabla wengine wote hawajatinga Kikwete hatawakuwa rais wa milele kesho anaweza kuja rais mwingine akaendeleza mapigo acheni kuangalia taifa kwenye ufinyu wa mabox yenu tu this thing is bigger than Warioba, msingi umewekwa hii ni mara ya kwanza Balozi kufukuzwa kwa wizi,

- Mawaziri wawili wa zamani kusota Keko Rumande, ndio tumeanza hivyo nani atakuwa next it does not matter, lakini ninasema hivi hawa viongozi wezi wote siku moja inakuja karibuni sana, watajikuta Kisutu na rumande Keko, hakuna aliye juu ya sheria kama wapo ni temporary tu and they know it!

Respect.

FMEs!
 
sielewi kwa nini wanajf tunataka warioba asifikishwe mahakamani wakati mwanancho gold ilijichotea mapesa.
kama yeye sio fisadi, akifikishwa mahamani atatutajia hao mafisadi wenyewe.
haki ipite ....tusiseme tu mtu msafi tukamalizia hapo ....mahakama kazi yake nini?
 

Mkuu hapa umenena, hiyo siku naisubiria sana. At least na wewe umeona kuwa kuna waliojuu ya sheria kwa sasa. TEMPORARILY. unajua kufikisha vidaa mahakamani huku mapapa yakiwa yanaangalia tu na kutuzuga inasikitisha sana, inauma kuona hata mashitaka yanafunguliwa kiujanja ujanja ile baadaye yabatilishwe na watu kutoka kiujanja ujanja na ku-operate kupindisha hiyo sheria.
NI machungu tu mkuu. Ni mimi mwenyewe wala sijaibiwa password yangu. Bado nafuatilia sana issue hii nzima, nikiwa na matumaini kuwa mkono wa sheria utafuatwa kwa kila mtanzania anayeihujumu nchi yake.
 
  1. Ni kwa nini vigogo wanaobanwa ni wale tu ambao wako mbali na Wanamtandao?
  2. Ukiangalia utaona kuwa wote wanakomaliwa, kesi zao ni nyepesi nyepesi ambazo sio ajabu serikali itashindwa, ndio maana yule mbunge akahoji ni kwa nini serikali inashindwa kwenye kesi zake nyingi?
  3. Kesi zenye ushahidi kibao kama za akina RA, Lowassa, Chenge n.k. hazipelekwi mahakamani, kwa nini utumiaji wa sheria uko selective?
Haya ni maigizo tu ya kuwaonyesha wahisani wanaochangia bajeti kuwa JK yuko serious na pia kuwakomoa wale wasiompigia magoti huyu mkuu na wala sio sheria msumeno.
 
Mahakamani usije ukafikiri kuna kujisafisha kule. Siku hizi watu wanatoka mahabusu na kesi kufutwa kwa kutumia 'legal technicalities', kesi ya msingi inaachwa bila kusikilizwa. Warioba ni Jaji na analijua hili ndio maana anaogopa. Unaweza kutiwa hatiani au kuachiwa huru kwa hizo 'legal technicalities'. Duniani hapa zipo sheria tu, lakini haki iko mbingun!
 


- Sio kweli mkuu yona alikuwa ni mtandao namba moja, infact yeye na Rostam kwa pamoja wanamiliki Gas Station kubwa sana kule Bagamoyo, kwamba wasio Mtandao peke yao! hapana sio kweli mkuu!

- Wamefikishwa mawaziri wawili, Yona ni Mtandao Mramba sio, eti hapo hakuna balance? Labda kwa mengine mkuu lakini sio hili.

Respect.

FMEs!
 
Kwa mara nyingine

(1) watu wameshachukua side! kama vile majaji, mimi wa warioba mimi wa serikali

Mambo yakishaiva unaona wengi humu wanakimbia hawataki tena kuchangia!

Mwizi mwizi tu, kwa hali ya sasa waache wapelekane mahakamani! kila kitu kitajulikana huko after all, warioba ni nguli wa sheria!

KAMA KUNA WEZI WA EPA WAKO HURU no PROBLEM, KAMA KUNA WEZI WENGINE no problem! swala ni kuwa kila mtu anatakiwa kuwa msafi, sio kusema mimi niliiba lakini niw wa mwisho kupelekwa mahakamani! waanze wale pale!!!!!!!!!!! huu ni utoto, (oh wakati wa kupigana hakuna kuvaa viatu, wala kuokota jiwe)!

Akipelekwa mahakamani, kuna nafasi nzuri ya wengine wengi kupelekwa wizi sio EPA tu hapa! sidhani kama walio upande wa warioba watakubali!

Kila mtu anatakiwa awe msafi jamani,sheria huwa haina nani alianza kwanza au nani ana priority ya kushtakiwa!

Huyo huyo warioba si yuko ndani ya CCM?? kinamweka nini kule maana kwangu mimi CCM ni dampo!

wanakaa meza moja wote hawa!
 

hata kama si wanamtandao lakini wezi wapelekwe tu mahakamani, jamani mbona hakuna hoja hapa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…