GE2025 Hatma ya Watanzania wanaoishi diaspora kushiriki uchaguzi mkuu 2025 bado haieleweki

GE2025 Hatma ya Watanzania wanaoishi diaspora kushiriki uchaguzi mkuu 2025 bado haieleweki

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa 2025 unakaribia kwa kasi, lakini bado Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanaendelea kutengwa na mchakato wa kidemokrasia. Pamoja na miaka ya mijadala na ahadi kutoka kwa viongozi wa kisiasa kuhusu mageuzi ya uchaguzi, hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa kuwezesha Watanzania wa diaspora kupiga kura bila kurejea nyumbani

Kinachochosha zaidi ni wanahusishwa kwenye uchumi wa taifa kupitia mchango wa fedha za ughaibuni, uwekezaji, na ushawishi katika maendeleo ya jamii kwa kiwango kikubwa, lakini haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi bado haijatambuliwa kisheria

Ni jambo la kushangaza kuona kuwa Tanzania bado haijaanzisha utaratibu wowote wa kuwawezesha wananchi wake waishio nje kushiriki uchaguzi, tofauti na nchi nyingi za Afrika kama Kenya, Ghana, na Afrika Kusini ambazo tayari zinatekeleza mifumo ya upigaji kura kwa diaspora. Serikali inaendelea kuhimiza ushiriki wa diaspora kwenye maendeleo, lakini si kwenye maamuzi ya uongozi wa taifa

Kwa hali ilivyo sasa, ni wazi kwamba hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya kisheria kabla ya uchaguzi wa Oktoba 2025. Hata hivyo, sauti kutoka nje ya mipaka ya nchi inaendelea kuwa kubwa na yenye ushawishi. Ni wakati wa kufikiria upya nafasi ya diaspora katika mchakato wa demokrasia hasa haki ya kushiriki kuchagua viongozi
Na hata Tume huru ya uchaguzi taifa imeshindw kweli kuunda sera za kuwawezesha kushiriki kwenye uchaguzi, ina maana wao siyo watanzania? Ni muda sana tangu diaspora ilipoomba mabadiliko lakini tume bado imeshindwa na viongozi wetu wamekatili

1754054642954.png
 
Hata watanzania wa upinzani (chadema) waliomo ndani ya mama Tanzania, hatima yao kushiriki uchaguzi bado Iko njia panda
 
Back
Top Bottom