GE2025 Hatma ya zuio la shughuli Kisiasa kwa CHADEMA kujulikana leo Agost 18, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Kesi ya madai dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na Katibu Mkuu wa chama hicho inatajwa leo, Agosti 18, 2025, katika Mahakama Kuu.

Shauri hilo Na. 8323/2025) linahusu zuio la kufanya shughuli za kisiasa lililotolewa na Mahakama tarehe 10 Juni 2025, ambapo baadhi viongozi wa CHADEMA walizuiwa kutekeleza shughuli za utendaji na kutumia rasilimali za chama.

Upande wa walalamikiwa (Katibu Mkuu na Bodi ya wadhamini) umeliwasilisha maombi ya kutengua zuio hilo kwa hoja kuwa lilienda kinyume cha haki ya kikatiba ya kushiriki siasa, na pia walinyimwa haki ya kusikilizwa hivyo uamuzi huo ulizingatia upande mmoja.

Upande wa wajibu maombi umepinga hoja hizo, wakisisitiza kuwa walalamikiwa hawakunyimwa haki bali walishindwa kwa uzembe wao kufuatilia mwenendo wa shauri, ambapo waliomba hoja zao kukataliwa.

Kufuatia hoja hizo Mahakama leo inatarajiwa kutoa uamuzi ambao utaamua iwapo zuio hilo litaendelea au vinginevyo.

Soma zaidi
 
Zuio liendelee mpaka kesi ya msingi itakapo malizika,huu ni ugomvi wa wanandoa.
 
Ktk serious inavyoenda itakuwa sawa na kesi ya mashahidi wa siri kesi ya Lissu
 
Tunaomba Mungu Aingilie Kati
Chadema Wafunguliwe.
Ila Kwa Jinsi CCM Wanavyoiogopa Chadema, Sidhani Kama Kuna Kuruhusiwa Kufanya Siasa Kwasasa Labda Baada Ya Uchaguzi Kupita.

Maana Chadema Wakifunguliwa Basi Ccm Inaenda Kupotezwa Mwaka Huu
Kitu Ambacho Ccm Nao Wameshakiona Na Ndio Maana Wameamua Kutumia Mbinu Chafu.
 
Amen, utekaji na kuua bado hakujasaidia hawa mbwa
Kabisa, na sasa wanazidi kugalagazwa kote kote..

Jaji hawezi kutokea ..

Jaji anamajukumu mengine ya kichama...(CCM wanaanza vikao vya kuteuwa wagombea ubunge)
Hivyo basi lazima afuatilie kwa umakini vikao hivyo
 
Back
Top Bottom