Hatoi matumizi ya mtoto, kaomba nimkopeshe pesa

Maisha ni kusameheana,kusaidiana na kurekebishana.Binafsi nakushauri kama unao uwezo mkopeshe tu huyo ni mzazi mwenzio hata kama utamchukia vipi ila mwisho wa siku ni mzazi mwenzio tu..cha msingi mueleze ukweli kuwa anakosea sana anaposhindwa kumlea mwanae,anamnyima haki yake mtoto..
 
Pole sana kwa unayo yapitia.

Lakini umeeleza sana upande mmoja wa mapungufu ya huyo jamaa lakini siamini Kama anamabaya tupu tu kwako naamini Kuna mema mingi tu aliyo kufanyia nyakati za mahusiano yenu.

Ni kwanini/ Nini kilitokea hadi akakataa mimba?
Mwanaume kukataa mimba sababu zaweza kuwa mbili
1 kuto kumuamini mwanamke aliye naye (anawanaume wengi). Hukuwahi kuwa msaliti kwake na akajua au hata kuwa na mashaka na wewe? ( Alikuwa na hofu ya kabambikiwa mimba coz labda anajua tabia za mwanamke aliye naye ndo mana akataka DNA.)

2 Sababu za kiuchumi ikiwa maisha yake hayaelewi na hana uhakika wa kumudu majukumu. Lakini wewe mwenyewe umesema kuwa ana kazi nzuri means pesa anazo kwahiyo alikuwa na sababu nyingine nje na hiyo.

Je mliwahi kugombana na Kama mligombana chanzo Cha ugomvi wenu kilikuwa nini?

Baada ya kujua mtoto ni wake alihudumia kwa miezi mitatu kisha akaacha then anakuja kukuomba umkopeshe pesa ilihali unajua kuwa ana kazi nzuri, je unajua nini kilimkuta?

Ana kazi nzuri, kwanini akupigie kukopa pesa kwako unadhani alikuwa na lengo la kukudhihaki au kukutapeli?

Mimi nadhani hapo Kuna kitu hakipo sawa kwake tofauti na wewe unavyodhani mkuu. Zungumza nae vizuri labda Kuna jambo halipo sawa japo simtetei kwa kukataa mimba.
 
Sawa mkuu asante kwa ushauri. Ningekua nayo ningempatia. Sipendi kuona binadamu mwenzangu anapitia wakati ngumu
 
Hapana my dear
Ok ila nakushauri either mfungie vioo jumla au ukubali akuendeshe hisia. Unadhani ana shida na hiyo hela? Hapo kakutega aone kama bado una upendo juu yake. So jibu sina lina maana ungekua nayo ungempa kitu kinachoashiria kuwa bado ana nafasi kwako.
Ulipaswa kumjibu kavu tu ili ajue huna mpango nae.
 
Pole sana usimpe hata senti moja labda kama unataka kutoa sadaka.
 
Pole sana kwa unayo yapitia.

Lakini umeeleza sana upande mmoja wa mapungufu ya huyo jamaa lakini siamini Kama anamabaya tupu tu kwako naamini Kuna mema mingi tu aliyo kufanyia nyakati za mahusiano yenu.
Mambo ni mengi mkuu ila isiwe sababu ya mtu kushindwa hata kumletea mtoto sukari ya uji..Wanaume kuna wakati wanajiendekeza sanaaaa...Kulea mtoto siyo lazima uwe na mamilioni pia kila mtu ana matatizo isiwe sababu ya kukimbia majukumu..Anyway I am not complaining
 
Hilo jibu kavu linajibiwaje mkuu?
 
Ningekua nayo ningempa. Mimi sina roho mbaya kama yake
Hata kama huna roho mbaya shoga usimpe..acha apambane tuu na hali yake halafu hawezi barikiwa hata angekuwa anafanya kazi juu ya anga hizo ni laana na ukimpa utageuzwa bank,hiyo laki tano bora umuwekee mwanao kwenye account itawafaa siku mkikwama,.kuna wanaume hawana haya jamanii khaa!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…