Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Safi sana mkuu nimepata kitu kitanisaidiaNo1: Hakuna biashara nzuri wala mbaya. Taarifa sahihi ya kile unachotaka kufanya ni hundred times better kuliko mtaji na idea yako. Mara nyingi unaweza kuwa uko-stucked mahali fulani kwa sababu ya ukosefu wa taarifa sahihi ya how that thing is done. So, jifunze kuinvest kwenye knowledge. Mwl wangu mmoja aliwahi niambia, 'Unajua inawezekana kabisa mengi ya matatizo unayopitia katika maisha yako kuna mtu alikwisha yapatia majibu na akayaandika kwenye kitabu ambacho hujawahi kisoma??' Hiyo sentence ili badili maisha yangu na kuongeza hamasa ya kuitafuta knowledge through books, attending seminars etc. Hivyo, before anything else, get quality information first about kile unatakakufanya.
No2: Take risk. Take control of your emotions. Management ya biashara inahitaji emotional maturity. Ni muhimu kuwa tayari kupoteza ulichotayari kukipoteza. Namaanisha kwamba, sio tu kwenye stock or forex Investment ila pia kwenye Investment nyinginezo, don't put your money if you can't afford losing it. Warren Buffet aliwahisema, 'if your too emotion about investing in business, you'll never do well. You can have all the feelings about business but the business will have no feeling about you."
No3: When the deal is too sweet, think twice. Usiamini kila unachoambiwa kuhusu mafanikio katika biashara fulani. Sometimes folks lie to encourage others to eat what ate them. Na ni hapa knowldge and quality information seeking inapokua muhimu. Kila mara, kila wakati jifunze na kamwe usiamini sana unachoambiwa kabla hujachunguza mwenyewe.
No4: Weka mikakati yako vizuri. Kuwa na definition yako mwenyewe ya mafanikio na ifuate. The cost of not following what you've planned for your business is living the rest of your life wishing you had. Usiilinganishe biashara yako na ya mtu mwingine coz ni wewe mwenyewe ndo unajua how far you want to go na nguvu kiasi gani uko tayari kuwekeza kwenye hiyo business. Sio mbaya kujifunza kwa wengine ila the moment u start defining your business kwa kuwaangalia wengine, you'll lose focus na utafail.
No5: Biashara inahitaji nidhamu sana sana, pesa ya biashara sio yako ni ya biashara that's why inaitwa 'pesa ya biashara'. Kuwa na your own rules. Kwenye biashara yako, kamwe usikopeshe fedha kama hufanyi biashara ya kukopesha fedha. Itakugharimu sana. "Before you loan any man a thing, assure yourself his ability to pay and his reputation of doing so, so you don't make a gift yiur hard earned money" - Arkad, pg 34 na hii ina-include wewe mwenyewe, kama hunaga tabia ya kurudisha pesa, usijikopeshe.
No6: Usiplan pesa ya biashara ndo i-run maisha yako hasa kama ndo unaanza biashara yako. Utajikuta unachukua fedha ya biashara na kujitia moyo kwamba utarejesha pesa hiyo kesho na hivyo ndivyo biashara yako itakavo kufanya kifo cha mende. Hakuna uchawi, wala mchawi hapo.
No7: Usianze kujitangaza sana na kutaka media coverage ukiwa bado unaanza. Jifunze kutumia vizuri eneo unalo limiliki kibiashara kabla hujataka kuanza kuvuka mipaka. Ni rahisi kuwastua wale giants wanaoa fanya biashara kama yako wakidhani wako alone. Unaweza jikuta unarudi ulipotoka kisa umeanza tu kuseek kujulikana at wrong stage. Sio mbaya kuwa known ila muhimu kujua kwanza ins and out kuihusu biashara yako like, who is doing what and how kabla hujaanza kutaka kuwa Bilget wa eneo lako. Wekeza kwenye kupata taarifa sahihi and always keep your next move to yourself.
No8: Ukianza fanikiwa kwenye business yako, kuwa makini sana na epuka kwenda katika kila eneo linalotangaza fursa, hasa kama u know for sure kwamba that might not be a fursa kwako. Ni hivi, kila mtu anataka kuwa karibu na business /mtu aliefanikiwa ila mara nyingi huwa tunasahau kuwa unapokua invited kwenye fursa/opportunity ambayo hucontribute chochote au mchango wako utakua mdogo(coz they only need to let you know about them and what wanafanya), elewa kwamba wewe uliekuwa invited ndio fursa. You might end up dying thinking you're making it up. Hivyo Jiridhishe kwanza kabla huja-attend fursa.
No9: Uvumilivu ni muhimu sana katika maisha ya biashara especially kwa start-ups. Usidanganywe na media wala inspirational talks, ukweli ni kwamba, handling a business is hectic in an early stages..you will be broke, depressed, you'll feel pain, people will hate you for no reason but don't quit. Warren Buffet aliwahisema sema, “No matter how great the talent or efforts, some things just take time. You can’t produce a baby in one month by getting nine women pregnant.” Hivyo uvumilivu ni muhimu sana na hasa ukiwa unajua why unavumilia.
No10: It is possible to do something good which is 100% wrong for your business existence. Usifanye kila kinachowezekana, fanya kila kinachowezekana ambacho ni sahihi. Kuna jamaa yangu aliwahi funga business yake kisa wateja waliamua kumuhama kwa kosa dogo sana. Alikua na contract ya kudeliver fresh mushrooms kwa baadhi ya restaurants, sasa ikatokea baada ya muda akaona atashindwa kudeliver quantity inayohitajika kwa wakati, so akaamua ku-outsource, too bad hakukumbuka quality ya uyoga wake ilikua tofauti na aliokua anachukua kwa wakulima wengine. Mara customers wa restaurants wakaanza kulalamikia ladha ya uyoga, jamaa alipoulizwa akasema ni kweli ule uyoga halimi yeye. Akaulizwa kwanini hakutoa taarifa, akajibu alitamani kuendelea 'ku-meet' order wakati akishughulikia uzalishaji katika shamba lake.
Kiuhalisia alichofanya kilikua kizuri, ila alisahau kuwa hakutakiwa ku-meet tu 'quantity' bali pia ku-maintain 'quality'.
Nice time.