Hatua 3 nilizopitia kufanya Market Research na kuanzisha mradi simple

Hatua 3 nilizopitia kufanya Market Research na kuanzisha mradi simple

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
1,414
Reaction score
2,181
Habari mkuu.

Leo napenda share nanyi mradi simple niliouanzisha mwezi September 2020 na hadi November hii inaanza umeonesha mafanikio endelevu nikipitia hatua 3 muhimu.

Hatua 3 muhimu nilizopitia ni :

1. Nilijiuliza wateja wangu ninaowalenga ni akina nani?

Nikaona ni wanawake walioathirika ngozi zao kwa vipodozi na wanahangaika kurudi ngozi zao asilia. Wengi wametumia gharama kubwa, muda na wengi kufikia hatua ya kukata tamaa.

2. Wapi wanapatikana wateja ninaowalenga?

Mara nyingi nakutana nao wakienda maofisini au biashara. Kwa kifupi ni watu wa kipato kikubwa na cha kati.

3. Nitawafikia kwa njia gani na hali ya kuwa wapo nchi nzima?

Kwa kuwa ni watu wanaomiliki smartphone , online ndiyo njia sahihi. Lakini online wapo wanaume na wanawake, wanafunzi n.k, sikutaka kupoteza muda wa kupost na kuishia likes bila kupata wateja, ili nichuje, nikatumia Adsmanager ya facebook, yaani nawalipa facebook pesa ya tangazo ili walitume kwa wanawake walioathirika ngozi kwa vipodozi, kisha wakigusa link kule facebook wanifuate whatsapp kwa maelezo zaidi. (Naona Video inashindwa upload , piga 0713039875 au whatsapp message utaiona program hii)

Thahamaki ndani ya siku 60 nikawa na group la watu 200 wakiulizia bidhaa. Kisha nikaunda group la ushauri na mrejesho kwa walionunua bidhaa zetu, ambapo robo ya hao 200, wamenunua na kuhamia group la kuleta mrejesho huku wakifurahia ngozi zao.
Hivyo, fanya research yako, Ingia kazini.
 
Kiongozi,unaonaje ukiongezea na website ambayo itakuwa inaorodhesha bidhaa zako zote na matumizi yake pamoja na ushauri mbali mbali,pamoja na blog kwa ajili ya kubadilishana mawazo na experiences baina yako na wateja wako pia baina yao wenyewe?

I believe itakuongezea ufanisi na kuvutia zaidi wateja.

Hii kazi naweza kuifanya mkuu ,mm ni Software Engineer mwenye uzoefu wa kutosha.karibu tuwasiliane.
 
Kiongozi,unaonaje ukiongezea na website ambayo itakua inaorodhesha bidhaa zako zote na matumizi yake pamoja na ushauri mbali mbali,pamoja na blog kwa ajili ya kubadilishana mawazo na experiences baina yako na wateja wako pia baina yao wenyewe ?
I believe itakuongezea ufanisi na kuvutia zaidi wateja,
Hii kazi naweza kuifanya mkuu ,mm ni Software Engineer mwenye uzoefu wa kutosha.karibu tuwasiliane.
Ntafanyia kazi mkuu
 
Biashara za kisasa hizo,
Sisi tumezoea nanunua dukani nakuja road napiga kelele weee huku nikitembea kidogo ndio nitapata wateja
 
Dola 5 kwa siku? aisee mbona ghali sana. Hio ni gharama ya kula na transport kwa siku 2
Dola 5 ni tzs 12,500 Kama unapata wateja watarajiwa ( leads) 50 na baada ya kuwaelimisha ndani ya whatsi group, hata wakinunua watano, big deal kwa bidhaa zinazoanzia elf 20 kwenda juu
 
Dola 5 ni tzs 12,500 Kama unapata wateja watarajiwa ( leads) 50 na baada ya kuwaelimisha ndani ya whatsi group, hata wakinunua watano, big deal kwa bidhaa zinazoanzia elf 20 kwenda juu
Kwa hapo sawa
 
Back
Top Bottom