Hatua 5 anazopitia graduate baada ya kuhitimu chuo

Hatua 5 anazopitia graduate baada ya kuhitimu chuo

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
HIZI HAPA HATUA TANO ANAZOPITIA GRADUATE WA KITANZANIA ANAPOMALIZA CHUO.

1. Mwaka wa kwanza baada ya kugraduate.Hapa bado kitaa hakijachanganya, anakua na hope kwamba atapata kazi muda wowote. Anatuma maombi sehemu mbali mbali, bado nguo za chuo na suti mbali mbali anazo, bado anang'aa, pengine anatumia muda huo kusalimia ndugu jamaa na kuzunguka mjini.

2.Mwaka wa pili baada ya kugraduate.Mambo ni magumu, nguo zimeisha, nyumbani anaanza kuonekana mzigo, anaanza kuwaza kujitolea, anapiga kazi yoyote inayokuja mbele yake. anatuma applications hamsini kwa siku na haitwi hata moja.

3. Mwaka wa tatu baada ya kugraduate.Hali ni mbaya zaidi, hakuna kinachoenda, matumaini yameisha, anaingia kwenye biashara, anafanya boda, anafanya bajaji etc. hapo lolote linalokaa mbele linafanywa ilimradi mkono uende kinywani.

4. Mwaka nne Baada ya kugraduate.Mawazo ya kuajiriwa yameisha, anafanya kazi zake za kujitegemea, ameanzisha familia, pengine amekua boda mzoefu, au winga mzoefu kariakoo na ameanza kufikiria maisha nje ya box. Akili zimeanza kukaa sawa sasa.

5. Mwaka wa Tano baada ya kugraduate. Mungu anajibu maombi, kama biashara zinaenda, au anapata kazi yake ya kwanza, anaingia kwenye ndoa, pengine anapata na kigari cha kutembelea. the rest inabaki kuwa ni historia.

Huyu ni Mtanzania wa kawaida, asiekua na connections.
 
Sema yote ni mipango ya mungu tu.Ukiona giza nene ujue kumekaribia kukucha
Sasa kwanini tuhangaike kuibadilisha ?

Hii Opium of the Mass inasaidia kutokuleta fujo kitaa ila atleast Kuuliza sio Ujinga jaribuni kuuliza Watumishi wenu....



 
Hizi stages zinaweza kwenda kinyume pia. Kuna graduate anamaliza,kazi anapata,familia inafuata.Mpira unageuka sasa kazi mkataba wake unaisha,anakimbia familia kutafuta,anafanya chochote kilichopo mbele yake,Mungu anasaidia anapata kazi tena ,mwisho anarudia familia yake.Maisha ya mtanzania kazi kweli kweli
 
Huyo ni kijana mjinga asiye na malengo, mi nimeua mwaka jana tu mwezi wa10 , sasa hivi nasukuma bajaji nimejifunza wiki1 tu, hiyo miaka mitano ntakuwa wapi?

Tatizo wanaleta ushua mwingi sana!!
 
Kuna wadada flan nawafahamu wawili,,,ni graduates ila mi bar maids,,, ! 100k kwa mwez, mtu ana mtoto, single mama, kapanga na ana mdada wa kukaa na mtoto let's say ni ndugu ama anamlipa 50/60k per month,,,,,,na tukumbuke mshahara wa huyu graduateni 100k ! Ama wanajiongezamo? Msingi kiuno ?
 
Back
Top Bottom