FUATA HATUA ZIFUATAZO
1. Andika barua ya KUOMBA NAFASI (SIYO YA UHAMISHO) katika Shirika la Umma unalotaka kuhamia ipitie kwa Mwajiri wako wa sasa.
2. Ukijibiwa kuwa nafasi ipo.
3. Andika barua ya KUOMBA UHAMISHO kwa Katibu Mkuu UTUMISHI kupitia kwa Mwajiri wako wa sasa ukiambatanisha na barua uliyopewa na Mkuu wa Shirika unalotaka kuhamia (Ile barua uliyojibiwa nafasi ipo).
4. Posti halafu subiria majibu au unaipeleka kwa Mkono unaenda KU-PUSH Wizarani UTUMISHI maana ukisubiri barua ikufikie utakaa sana hata mwaka na zaidi au inaweza kuja Mwajiri aka-MuTE nayo.
NB: Kuna baadhi ya Wakuu wa Taasisi kutokana na UHITAJI wao (Maana JPM alizuia ajira kwa muda mrefu) wakipata barua yako ya ya kuomba nafasi iliyopitishwa na Mwajiri wako wa sasa KUOMBA NAFASI wanamaliza wenyewe na UTUMISHI. ila ni wachache sana
Kila la heri mkuu kwa kutaka kukimbia TGS.