Hatua hii ya Kenya itaiimarisha EAC

Hatua hii ya Kenya itaiimarisha EAC

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
membe_amina.jpg

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe akimsindikiza mgeni wake Waziri mwenza wa Kenya, Amina Mohammed baada ya waziri huyo kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari Dar Salaam.PICHA|EMMANUEL HERMAN

KWA UFUPI
Hotuba ya Rais Kikwete ilifikisha ujumbe kule kulikotarajiwa. Ikiwa ni siku nne baada ya Rais kulihutubia Bunge akilalamikia nchi hizo kuitenga Tanzania, Kenya imemtuma Waziri wake wa Mambo ya Nje, Amina Mohamed kuja hapa nchini kuwasilisha ujumbe wa Rais Uhuru Kenyatta kwamba nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania kwa kutambua umuhimu wake kama moja ya waanzilishi wa Jumuiya hiyo.

Bila shaka hakuna Mtanzania hata mmoja ambaye hakuipongeza hatua ya Serikali ya Kenya kutuma ujumbe wa kuunga mkono msimamo wa Tanzania wa kutojitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), licha ya nchi za Uganda, Kenya na Rwanda kufanya mikutano kujadili mipango na masuala yanayohusu jumuiya hiyo pasipo kuihusisha Tanzania, kinyume kabisa na Mkataba wa Jumuiya hiyo.

Tanzania ilipinga kwa nguvu zote hatua ya nchi hizo kuitenga hata katika masuala yaliyo chini ya jumuiya hiyo, ambayo kwa mujibu wa mkataba huo yanapaswa kujadiliwa na kutekelezwa kwa pamoja na nchi zote wanachama. Rais Jakaya Kikwete alilazimika kulihutubia Bunge wiki iliyopita na kuelezea kwa kirefu ukiukwaji wa mkataba huo na athari za kuzitenga Burundi na Tanzania katika mikutano inayojadili masuala ya EAC.

Pamoja na kuzikosoa na kuzilaumu vikali nchi hizo tatu kwa kukiuka mkataba huo pamoja na itifaki zake mbalimbali, Rais Kikwete aliweka wazi msimamo kwamba Tanzania kamwe haitajitoa katika Jumuiya hiyo na itaendelea kuwa mshirika mwaminifu wa Jumuiya hiyo pasipo kutetereka. Msimamo huo bila shaka uliondoa hofu iliyokuwa imetanda miongoni mwa wananchi katika nchi zote wanachama wa EAC, kwamba Tanzania ingejitoa katika Jumuiya hiyo kutokana na kutengwa na nchi hizo tatu zilizokuwa zikiunda kile kilichoitwa ‘Coalition of the willing’ (Ushirikiano wa wenye hiari).

Hotuba ya Rais Kikwete ilifikisha ujumbe kule kulikotarajiwa. Ikiwa ni siku nne baada ya Rais kulihutubia Bunge akilalamikia nchi hizo kuitenga Tanzania, Kenya imemtuma Waziri wake wa Mambo ya Nje, Amina Mohamed kuja hapa nchini kuwasilisha ujumbe wa Rais Uhuru Kenyatta kwamba nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania kwa kutambua umuhimu wake kama moja ya waanzilishi wa Jumuiya hiyo. Waziri huyo alisema kuwa, kuja kwake hapa nchini kunafuatia Serikali ya Kenya kusoma kwa undani hotuba ya Rais Kikwete ambayo alisema, ilikuwa nzuri na ilitolewa kwa nia njema tu ya kuimarisha Jumuiya hiyo na siyo kuidhoofisha.

Sisi tunadhani hatua ya Kenya ya kutafuta maridhiano na Tanzania ni ya kupongeza, hasa tukitilia maanani ukweli kwamba moja ya sababu kubwa zilizosababisha kuvunjika kwa EAC mwaka 1977 ilikuwa ni kutokuwapo utamaduni wa nchi wanachama kujikosoa na kuona umuhimu wa kumaliza tofauti zao kwa njia ya mazungumzo. Hatua hiyo ya Kenya yafaa iwe mfano kwa nchi nyingine ndani ya Jumuiya hiyo, kwamba zijisahihishe pale zinapojiridhisha kwamba zimekosea hapa au pale.

Hapa hatuna maana kwamba Tanzania haikuchangia lolote katika kufikiwa kwa hali hiyo ya kutengwa. Kwa mfano, mbali na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi imekuwa ikilalamikiwa na nchi nyingi jirani zinazotumia Bandari ya Dar es Salaam. Yamekuwapo malalamiko mengi na ya muda mrefu kuhusu ucheleweshaji wa kupakua na kupakia shehena za mizigo, ukubwa wa tozo za bandari na barabara pamoja na uchakachuaji wa mafuta. Ndiyo maana baadhi ya nchi hizo zimeamua kutumia Bandari ya Mombasa.

Ni matumaini yetu kwamba nchi wanachama wa EAC zitachukulia mvutano uliokuwapo kati yao na Tanzania kama changamoto ya kuzisukuma kushirikiana zaidi ili kujenga Jumuiya yenye nguvu kubwa kiuchumi. Wakati huohuo, hatua hiyo ya Kenya ni ya kijasiri, siyo udhaifu.Chanzo. Hatua hii ya Kenya itaiimarisha EAC - Uchambuzi - mwananchi.co.tz
 
Wewe acha zako hizo za kipimbi hao unawachukia nn?wanakupunguzia kitu gani au walikuchukulia mkeo?Sasa kwa taarifa yako nikwamba Cc watz tupo wengi sana kenya kuliko unavyowazania kwamba wao ndo wengi huku.Lazima tushirikiane.Walianza mababu ww utazuia kitu gani?nenda kapoteze muda wako ktk vijiwe vya kahawa.
 
Na kama huamini nakutajia makazi ya watz kenya najua kwa wakenya utataja sana sana Arusha.Haya tuanze.Mji wa mombasa(mwembetayari,likoni,changamwe,kisauni,ganjoni,majengo na malindi ndo wamejaa wapemba.Nairobi(mlolongo,Gikombaa,ngara road,kitengela,eastleigh.kisumu ndo husiseme wamejaa watu kutoka ktk mkoa wa mara na hata eldoret watz ni wengi.wewe hao umejikalia ninawachukia wa ke!???elimika baba!!!!!!!
 
Humu ndani kuna baadhi ya watu wao kazi zao ni kueneza chuki tu baina ya jamii.Haipendezi jamani.
 
Deep down my heart i hate Kenyans, hata aje kiumbe gani, i will still hate them.

Hate is such a strong word when you are talking about 40 million people, what has an ordinary Kenyan ever done to you to justify your hatred?
 
Naipongeza kenya kwakuwa waungwana katika hili japokuwa mnafiki ni mnafiki tu.

True.. they'r economical potential hatutawatupa ila we'r dealing wth them under the strict EYE..!!! Na wao wanajua sisi ni muhimu kwa uchumi wao lazima wamaintain good neighbourhood.
 
Wewe acha zako hizo za kipimbi hao unawachukia nn?wanakupunguzia kitu gani au walikuchukulia mkeo?Sasa kwa taarifa yako nikwamba Cc watz tupo wengi sana kenya kuliko unavyowazania kwamba wao ndo wengi huku.Lazima tushirikiane.Walianza mababu ww utazuia kitu gani?nenda kapoteze muda wako ktk vijiwe vya kahawa.

Thank you so much for this comment. The only way we as Africans can be competitive in the world market is by building trading blocks, not tearing them down. Disagreements are normal in negotiations and our nations should come up with solutions to prevent future deadlocks and not fuel xenophobic sentiments. We have so much to gain from this federation than we have to lose, hayo mambo ya mashamba hatuyataki if that is what is holding us down.
 
Unajua Africa tukikaa hivi kwa chuki na utengano mwisho wa siku tutabaki kua kama slaves tu kwa hawa jamaa wa western countries, nipo nje kuna stores flani zinaitwa 7/11 kwa walioishi nje watakua wanazijua zipo nyingi sana, ukiingia kuna bango flani hivi la sigara wameonyesha Africa afu sokwe ndio kashika mic anatangaza habari, afu wameandika "This is Africa" yani a direct hit nje tunadharaulika.. Tufikirie kuungana hasa kwa mazuri, kichwani iwepo kunyanyua uchumi kama nchi moja vile ila sio kufikiria kila mtu kufaidika kivyake, at the end kama ilivokua vision ya Ghadhafi Africa ingekua moja tungekua na nguvu sana, we have everything we need na kama huamini hata scientist wapo vichwa vya kutosha tu, hapa nlipo nafahamu lecturers wanne wanafundisha vyuo vikubwa sana duniani ni watanzania, je wa nchi nyingine? We can do everything ourselves ila muungano tusiupuuzie, why hate Kenyans or Ugandans?? i have Kenyan friends, Ugandan friends mbona ni watu wazuri tu, alichokufanyia mkenya moja sio wakenya wote, kwani mtanzania mwenzako hajawahi kufanyia ubaya? si uchukie watanzania wote sasa kama ni hivo. Think of realizing your dreams n not hatred, that way utakua angalau umepunguza shida moja kwenye taifa lako..
 
... hayo mambo ya mashamba hatuyataki if that is what is holding us down.
Mkuu, umekuwa msemaji wa serikali ya Kenya? Hata hivyo, bila unafiki, naipongeza sana Kenya kwa kuwa waungwana!
 
You don't need to be a certified psychologist to play with akili ya watanzania............wewe wasifie tu.............watasahau kila kitu
 
Mkuu, umekuwa msemaji wa serikali ya Kenya? Hata hivyo, bila unafiki, naipongeza sana Kenya kwa kuwa waungwana!

its just an opinion jabulani, we must get rid of whatever is holding us back from development ama you thinking otherwise?
 
Hatred (or hate) is a deep and emotional extreme dislike that can be directed against individuals, entities, objects, or ideas. Hatred is often associated with feelings of anger and a disposition towards hostility. Commonly held moral rules, such as the Golden Rule, oppose universal hatred towards another.
Your hatred is misdirected! Wakenya wamekufanyia nini mbaya wewe binafsi?
 
True.. they'r economical potential hatutawatupa ila we'r dealing wth them under the strict EYE..!!! Na wao wanajua sisi ni muhimu kwa uchumi wao lazima wamaintain good neighbourhood.

It is not a one way traffic though, Kenya too is important for the economic well being of TZ.
 
Back
Top Bottom