#COVID19 Hatua kali za udhibiti wa maambukizi bado ni njia bora zaidi ya kukabiliana na COVID-19 nchini China

#COVID19 Hatua kali za udhibiti wa maambukizi bado ni njia bora zaidi ya kukabiliana na COVID-19 nchini China

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111376768967.jpg

Hivi karibuni, mlipuko wa wimbi jipya la COVID-19 katika miji kadhaa nchini China ikiwemo Shanghai na Beijing umefuatiliwa na vyombo vya habari na jamii ya kimataifa. Watu wengi wanashangaa kwamba, wakati kirusi kipya cha Omicron, ambacho kinaambukiza kwa kasi zaidi na bila ya sumu kali, kimekuwa kirusi kikuu cha Corona, na nchi nyingi duniani zimeamua kulegeza hata kuacha kabisa hatua za kukinga virusi, kwa nini China bado inatekeleza hatua kali za kudhibiti maambukizi?

Hatua hizo ni sera kuu ya China katika kuzuia na kudhibiti janga la COVID-19. Uzoefu wa China wa kukabiliana na janga hilo katika zaidi ya miaka miwili iliyopita umethibitisha kuwa sera hiyo inaweza kulinda vizuri afya na usalama wa maisha ya watu wa China, na kupunguza athari za janga hilo kwa maendeleo ya uchumi na jamii nchini China.

Kwanza, China yenye watu bilioni 1.4 ni nchi ya kwanza kwa idadi ya watu duniani. Virusi vya Corona ni virusi vipya, ambavyo binadamu bado hawajavielewa na kuvidhibiti vizuri, hivyo usalama wa maisha ya watu umezingatiwa zaidi na China. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani, katika miaka ya 2020 na 2021, janga la COVID-19 lilisababisha vifo vya watu milioni 15 duniani. Wakati huohuo, idadi ya vifo vya watu kutokana na janga hilo nchini China ilikuwa chini ya 20,000 tu. Ingawa baadhi ya mashirika ya utafiti yanaona kuwa makali ya Omicron yamepungua, lakini ripoti iliyotolewa na jarida maarufu la Tiba ya Asili inaonysha kuwa, ikiwa China itaacha hatua kali za kudhibiti virusi, ndani ya miezi 6, China itashuhudia kesi milioni 112.2 za maambukizi ya virusi vya Corona, na kusababisha vifo vya watu takriban milioni 1.55.

Pili, idadi kubwa ya wazee nchini China imezidisha tishio na changamoto zinazoletwa na janga la COVID-19. Tofauti na nchi za Afrika zenye vijana wengi zaidi, China inaingia kwa kasi katika jamii inayozeeka, na ina takriban wazee milioni 200 wenye umri wa zaidi ya miaka 65. Licha ya hayo, China pia inakabiliwa na changamoto za ukosefu wa uwiano wa maendeleo kati ya sehemu tofauti, na upungufu wa rasilimali ya huduma za afya katika baadhi ya sehemu. Kama China ikilegeza sera yake ya kukabiliana na virusi, idadi kubwa ya wazee wataambukizwa ndani ya muda mfupi, na kisha idadi kubwa ya vifo itatokea.

Tatu, China ni nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani, na pia ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani. Kudumisha utulivu wa maendeleo ya uchumi wa China ni muhimu kwa China na dunia nzima. Virusi ndio chanzo kikuu cha msukosuko wa uchumi, na kudhibiti vizuri virusi ni mazingira ya lazima kwa maendeleo ya uchumi. Katika zaidi ya miaka miwili iliyopita, sera ya China ya “hatua kali za kudhibiti maambukizi” imedumisha utulivu wa maendeleo endelevu ya uchumi. Mwaka wa 2020, China ilikuwa nchi pekee ambayo uchumi wake ulikua kati ya nchi kubwa za kiuchumi. Mwaka 2021, pato la taifa la China liliongezeka kwa asilimia 8.1 ikilinganishwa na mwaka 2020. Katika robo ya kwanza ya mwaka huu, pato la taifa la China lilikua kwa 4.8% licha ya athari za wimbi jipya la janga la COVID-19.

Katika kukabiliana na janga la COVID-19, nchi mbalimbali duniani zinapaswa kuchagua sera inayofaa kwa kulingana na hali yake halisi. China ina imani thabiti ya kushinda vita dhidi ya janga la COVID-19, na itaendelea kutoa mchango zaidi kwa juhudi za kimataifa za kukabiliana na janga hilo.
 
Back
Top Bottom