Mkuu Farolito, shukrani kwa pongezi.The Consult,asante sana kwa kutuelimisha,naomba nisaidie mambo yafuatayo
1.Je project unayoandikia proposal kwa ajili ya kuombea funding ni lazima iwepo(existing)?au in hata wazo tu mfano nataka kuanzisha Hospitali nikaamua kuandikia proposal?
2.Kuna mahali nimekuta masharti mojawapo katika kuomba fund in kwamba kwenye proposal yako kuwe na
'Strong public diplomacy component' Je ni kitu gani naomba maelezo nielewe.
3.Pia walisema Iwe na' project monitoring &reporting plan covering the entire project time plan.(hapo pia wanataka nini)?
Mwisho naomba kama una sample ya project proposal ya kuomba fund nirushie PM
Asante.
Unaweza kufanya editing, ila uwezekano wa andiko lako kufanikiwa utakuwa mdogo sana, hii ni kwa sababu;Hivi naweza nika edit proposal kutoka google na kujaribu bahati yangu
Asante,kweli mambo ni mengi mpaka uwe na taasisi tena ,nilikuwa nataka niwajaribu wa Malta flani hivi huwa wanatoa fund za miradi tena wanakuja kusimamia wenyewe kama labda kujenga ,wakimaliza wanasepaUnaweza kufanya editing, ila uwezekano wa andiko lako kufanikiwa utakuwa mdogo sana, hii ni kwa sababu;
1. Wafadhili wengi hawapendi hiki kitu
2. Matatizo, mazingira, wahusika hutofautiana kati ya sehemu moja na nyingine ambapo kwa kiasi kikubwa hu-determine contents and structure of the proposal.
Ili uwezekano wa andiko lako kufanikiwa, unapswa;
1. Kumtambua na kumjua vizuri mfadhili, na uhakikishe ana interest juu ya mradi wako
2. Kufuata utaratibu (guidelines) uliowekwa na mfadhili.
3. Kuhakikisha uzoefu na uwezo wa Taasisi yako unaendana na kiasi cha fedha unachotaka kuomba.
4. Kuhakikisha una-develop a good relationship with the one who provides that fund katika hatua za mwanzo kabisa kabla ya utoaji wa fund. (Hii relation inaweza kuwa: kwa kuhudhuria trainings zao, n. k) Hapa ikiwa mfadhili ni wa ndani.
5. Na mengineyo.
The Consult
Ufadhili upo wa aina mbili Mkuu;As
Asante,kweli mambo ni mengi mpaka uwe na taasisi tena ,nilikuwa nataka niwajaribu wa Malta flani hivi huwa wanatoa fund za miradi tena wanakuja kusimamia wenyewe kama labda kujenga ,wakimaliza wanasepa
Ufadhili upo wa aina mbili Mkuu;
1. Kuna wafadhili wanaotoa fedha kwa vikundi/taasisi zilizo na usajili. Kwa kiasi kikubwa ndio nilikuwa nikiwaelezea. Na miradi inayotumwa kwao ni ile yenye kuhusisha namba kubwa ya beneficiaries, na hata project team ni kubwa kiasi. Hawa wapo wengi zaidi ukifananisha na hawa nitakaowaelezea hapa chini.
2. Kuna wafadhili wanaotoa fedha kwa mtu mmoja mmoja. Hawa mara nyingi hufadhili miradi yenye sifa zifuatazo.
-Mara nyingi ni for profit making projects, ila iwe na great social impact, kwa mfano UBER Project and the likes(Ila unaweza ukajuana na mfadhili personally, akaamua kukufadhili katika mradi wako hata kama si wa profit making, mfano ujenzi wa shule kwa ajili ya watoto wasiojiweza/vilema n. k)
-Hufadhili miradi iliyo na ubunifu ndani yake.
Ahsante.
Mkuu asante sana,Mkuu Farolito, shukrani kwa pongezi.
Ningependa nikujibu maswali yako kama ifuatavyo;
1. EXISTING katika project. Hii kwa jina jingine hujulikana kama PROJECT TERMINATION na ni hatua ya mwisho kabisa katika mzunguko wa mradi (Project Cycle). Kila mradi lazima uwe na mwisho, na hapa ndipo unapopata tofauti kati ya "PROJECT" na "OPERATIONS". Mradi hufikia tamati/mwisho pindi;
Unapokuwa na wazo la mradi wa ujenzi wa hospitali, kutokana na sababu za hapo juu, bado mradi wako utapaswa kufika tamati.
- Malengo ya mradi yanapofikiwa (attainment of project objectives)
- Uelekeo wa mradi unapobadilika na hatimaye kusababisha uongezakaji wa gharama. Katika hatua ya utekelezaji wa mradi (Project Execution) inashauriwa kuwa na 'documents" mbili za mradi; ORIGINAL PROJECT PLAN na ACTUAL PROJECT PLAN. Katika kila hatua ya utekelezaji lazima kufanyike uoanishai wa hizi plans. Sasa huwa kuna wakati project goes too far beyond its original design, na kuirudisha itachukua gharama kubwa, na ukisema kuendelea nao, utatimiza malengo tofauti na yaliyokusudiwa, katika hatua hii, ni vyema kuhitimisha mradi.
- Kipaumbele cha Taasisi kinapobadilika. Hii hutokea katika miradi inayotekelezwa na Taasisi za kibiashara (For-profit making org). n.k
2.STRONG PUBLIC DIPLOMACY COMPONENT, kipengele hiki hupatikana sana katika miradi inayofadhiliwa na serikali ya Marekani. Maana yake hapa ni kwamba; katika proposal yako utakoyoiandaa ni lazima uhakikishe kuna 'American component/aspect" kwa mfano kumtumia Mtaalamu kutoka katika ubalozi wa Marekani kama trainer/facilitor/speaker katika mradi wako ikiwa kama mradi ni wa ujengaji uwezo, kutumia mtaala ulioandaliwa na Taasisi ya Kimarekani, au kama kuna "exchange program" ilifanyika; kutumia ujuzi huo katika uandaaji wa proposal yako.
3.PROJECT MONITORING & REPORTING PLAN, ni mpango ambao unaonyesha namna ambavyo ufuatiliaji na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Mradi utakavyofanyika. Mpango huu utapaswa kuonyesha malengo yanayohitaji kufikiwa, viashiria kupima ufikiaji wa malengo, chanzo cha taarifa juu ya ufikiaji wa malengo, kipindi cha ukusanyaji wa taarifa juu ya utimilifu wa malengo, mhusika, namna ya uwasilishaji wa taarifa n.k
4. Kuhusu sample Mkuu, nilizonazo ni za wateja wangu na huwa sina utaratibu wa kuzi-share pasina ruksa yao. Cha kukusaidi tu, labda nikuandalie FORMAT ya project proposal.
The Consult
Karibu Sana Mkuu.Sawa nimekuelewa ,nitafanya nione
Karibu Mkuu.asante kwa elimu .Imenisaidia kupata kitu
Hata mie ninahitajiAhsante, The Consult .
Una mifano mbalimbali ya Andiko la mradi katika Portable Doc Folder unisaidie?.
Natanguliza shukrani za dhati.
Asalaam.
Mkuu.Nitakutafuta kwaajili ya kupata proposal..je nawezaje pata mfadhili kama proposal teyari ninayo baada ya kuniandalia kwa project lengwa?
Okay project yangu ni kunenga shule nursery and primary angalau nianze kidogo then ndio nitafute mfadhili..bado sina idea katika case ya kuwa chini ya mwamvuli wa taasisi...kama mimi as individual itawia ugumu..nyie mnatoa muongozo wa kuweza ku direct taasisi kwa mtu anaehitaji?Mkuu.
Ufadhili kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi unapatikana, ila ; wafadhili wengi (karibia 95%) hutoa ufadhili kwa Miradi inayotekelezwa chini ya mwamvuli wa Taasisi. Ufadhili mchache sana hupatikana kwa Miradi inayotekelezwa na mtu mmoja mmoja. Pia ili kuongeza uwezekano wa kupata huo ufadhili; malengo ya Mradi yanapaswa kuendana na vipaumbele vya Wafadhili.
Mfano, kwa sasa vipaumbele (thematic areas) vya wafadhili wengi ni;
-Uboreshaji wa Maisha ya Watu wenye Ulemavu.
-Uwezeshaji wa Wanawake
-Utawala Bora
-Upatikanaji wa elimu bora. n. k
Kimsingi vipaumbele vya wafadhili wengi hutokana na Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Goals)
Sasa, sijajua huo Mradi wako unataka kuutekeleza chini ya mwamvuli wa Taasisi au wewe as an Individual.
The Consult.